Daldo wa Ngorongoro anakera, sijui nikamshitaki wapi?

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
956
120
Ramadhan karim JF.

Ndugu zangu ukitaka kufahamu viongozi vibuyu katika serikali za mitaa basi fika halmashauri ya wilaya ya ngorongoro hasa idara ya kilimo/mifugo. Huko utakutana na mama mmoja anayeitwa Maria Leshalu aliyepata cheo cha ukuu wa idara ya kilimo/mifugo kupitia kivuli cha Edward Lowasa ijapokuwa hana sifa hizo sifa. Mkuu huyo amekuwa akiendeshwa na kutolewa maamuz na subordinate wake VB KAIZA ambaye anasifika kwa ufisadi idarani hapo.

Mama huyu ambaye ametengeneza makundi na chuki miongoni mwa watumishi ndani ya idara hili kuficha udhaifu wake wa kutowajibika. Inasemekana mama huyu analindwa na kigogo Mmoja pale TAMISEMI ambapo inapelekea hata DED ashindwe kumchukulia hatua.

Nisaidieni jamani niende wapi nikamshtaki?
 
huyu mama kwa sasa anaprove failure kuwa wanawake wakipewa uongozi watazamisha hii nchi.
 
Ramadhan karim JF.

Ndugu zangu ukitaka kufahamu viongozi vibuyu katika serikali za mitaa basi fika halmashauri ya wilaya ya ngorongoro hasa idara ya kilimo/mifugo. Huko utakutana na mama mmoja anayeitwa Maria Leshalu aliyepata cheo cha ukuu wa idara ya kilimo/mifugo kupitia kivuli cha Edward Lowasa ijapokuwa hana sifa hizo sifa. Mkuu huyo amekuwa akiendeshwa na kutolewa maamuz na subordinate wake VB KAIZA ambaye anasifika kwa ufisadi idarani hapo.

Mama huyu ambaye ametengeneza makundi na chuki miongoni mwa watumishi ndani ya idara hili kuficha udhaifu wake wa kutowajibika. Inasemekana mama huyu analindwa na kigogo Mmoja pale TAMISEMI ambapo inapelekea hata DED ashindwe kumchukulia hatua.

Nisaidieni jamani niende wapi nikamshtaki?

Ukamshitaki kwa kosa lipi? Kama ni ufisadi utamshitaki kwa nani
ambaye ameprove kuwa hacheki na mafisadi?
 
Hao unaotaka kuwapelekea kesi yako nao pia ni mafisadi.
 
Halmashauri zote ziko hivyo. Wachapa kazi ndo wanaotafutiwa visingizio mbalimbali. Vilaza wanapeta. Huyo mama kawekwa makusudi ili wakubwa wake wachote. Ataendelea kupeta tu ndo maana kafichwa huko porini ili ukilaza wake uchukue muda kugundulika.
 
We wa wapi? Nani kakuambia kuwa mafisadi wanashitakiwa? Kwa sheria ipi? Na kwenye nchi ipi? Na imetokea wapi katika nchi hii mafisadi wakashitakiwa
 
Jamani Watz wenzangu hasa kwa wale wazalendo najua mnafahamu kama hamfahamu basi naomba niwafahamishe Wilaya ya Ngorongoro ndio wilaya ya pili kuchangia mapato katika fuko la taifa ukiacha ile ya ilala. ngorongoro kuna fedha nyingi zinaibwa, zinaliwa huwez amini pamoja na utajiri wote huo mpaka leo hakuna maji wilayani ikiwa chanzo cha maji kipo si zaidi ya km 3 kutoka makao makuu ya wilaya.
 
Idara ya kilimo/mifugo ndio kuna uozo mkubwa pembejeo za kilimo zinatafunwa haswa na mawakala wakishirikiana na Afisa ughani anayejulikana kwa jina la Kaiza. Idara ya kilimo/mifugo inanuka rushwa, ubadhirifu na ufisadi wa kutisha. Hv karibuni wameleta powertillers za kichina ambazo hazijadumu hata miezi mitatu zote zipo juu ya mawe.
 
miundombinu ya mifugo ndio imekufa kabisa na hata inayotengenezwa ni mibovu mpaka wakandarasi wanakimbia kazi, maengineer wa kilimo wanatoa certificate coz wamepewa 10% na si ubora wa kazi. haya yote yanatokea coz hamna public media wilaya ya ngorongoro. watz wenzangu tuiokoe wilaya hii kabla haijateketea ndani ya midomo ya mafisadi.
 
Tumeshasikia kila aina ya ufisadi katika nchi hii mara Richmond, Meremeta, EPA, Kagoda, Jairo etc etc japo ufisadi huu nilioutaja hapo ni mkubwa na unagusa sana taifa ila ni vyema tukajiuliza source kubwa ya mapato ya huu ufisadi unatoka wapi? Ikiwa halmashauri zetu zinachangia kwa asilimia kubwa ktk mapato ya serikali basi sitachelea kusema ufisadi mkubwa unaanzia kwenye halmashauri za wilaya ambazo zina vyanzo vingi vya mapato.
 
Haya ndiyo tunasema serikali goigoi au legelege ya Jk inasitahili iondoke ituachie TZ yetu mapema kabla ya 2015. Uliza uozo mwingine pale NARCO Kongwa!!! eti Manager wa Ranch ni ''msomaji'' mwenye astashahada yaani DIPLOMA....uliza anayemsaidia yaani assistant manager wake....ni msomi mwenye shahada tatu tena za nje ya nchi(PhD) ambaye serikali ilimgharamia kusoma huko. Kisa nini hawa mafisadi waendelee kuchukua mali za umma bila kuulizwa...Shame on us...shame on TZ....kama tutaendelea kunyamaza hivi tutaishia pabaya.
 
Reginanduma

Tuko pamoja mkuu ni vyema tukawaweka wazi hawa mafisadi wote bila kujali kiasi gani walichofisadi. Huku Ngorongoro kuna bwana mmoja anaitwa VB KAIZA aliachiwa akaimu idara ya kilimo/mifugo ndani ya mwaka 1 wa fedha wa kiserikali akajitengenezea posho ya jumla ya Tsh 35m peke yake.
 
Nadhani kuna tume ya maadili ya viongozi au tume ya haki za binadamu inaweza kuwa mwanzo wa kuchukua hatua dhidi ya huyo DALDO
 
Back
Top Bottom