Dah kweli Maisha magumu na muda hautoshi.

LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,014
578
Niko kwenye daladala natokea kwenye pilikapilika za kutafuta mkate wa kila siku.

Pembeni yangu kakaa mama mmoja anayeonekana katoka kutafuta mkate na yeye. Mama huyu amechoka, anaonekana pia hana furaha ya kutosha. Mara amefungua mfuko wake katoa mboga za majani anaanza kuchambua. Dah nkimwambia mama umeona urahisishe mambo eeh! Akanijibu kwa upole acha tu dada angu, maisha haya. Tunavyohangaika hata muda hautoshi.

Mama huyo hapo ukute watoto wamekaa mlangoni wanasubiri mama arudi.
 
Mhhh ..........lakini ungemwambia afadhali wewe hata mchicha unapata wengine hata mboga hawana...
 
Maisha yanakabili kila mtu kwa sura tofauti,tumwombe tu MUNGU atusaidie na tuongeze juhudi ktk kila jambo tunalofanya.
 
Aisee Voice ulikuwa wapi, dah usiwe unatesa nafsi za watu kiasi hicho. Uwn unaaga basi. Maisha yanakua magumu kwa sababu yako bana. Ngoja nikufate huko.
 
Hapo fikiria kuna baba na watoto wanamsubiria, yani ili wote hawa wale ni mpaka huyu mama afikishe mboga nyumbani. Halafu uliza mama katokea wapi kuelekea wapi, Ubungo/Mwenge afu tgeta. Dah mama mama!!
 
Hahahahahahahahah,

Naona hapo umekuwa mkubwa sana kajukuu kangu kazuri LD!!!! Halafu unajua huyo baba si ajabu hana shida na hiyo mboga. Shida yake ni kitu kingine kabisaaaaaaa!!!!

Hata hivyo usirudie kusema maisha ni magumu. Sema maisha yako binafsi naya huyo mama yamekwama kwenye tope. Wakati huo kuna watu wengine wanatesa kwe V8, full AC na wakifika home wanakuta menu choices kama 100 hivi. Hawana hata habari kama kuna kifo. Hao pia umewafikiria?

Usirudie tena kusema hivyo,...umesikia kajukuu???

Mzee DC!!
 
Daah
Babu nae kawa msanii siku hizi
Halafu da LD umepotelea wapi, nimekumiso balaa
 
Mh!Muda haujawahi kutosha tangu zamani,kibaya hata sisi wenyewe hatujitoshi!
 
yaaaani kila mtu analalamika

ushauri wangu ni huuu

tupunguze kuwa consumers,tuwe producers japo kidogo
 
Niko kwenye daladala natokea kwenye pilikapilika za kutafuta mkate wa kila siku. Pembeni yangu kakaa mama mmoja anayeonekana katoka kutafuta mkate na yeye. Mama huyu amechoka, anaonekana pia hana furaha ya kutosha. Mara amefungua mfuko wake katoa mboga za majani anaanza kuchambua. Dah nkimwambia mama umeona urahisishe mambo eeh! Akanijibu kwa upole acha tu dada angu, maisha haya. Tunavyo hangaika hata muda hautoshi. Mama huyo hapo ukute watoto wamekaa mlangoni wanasubiri mama arudi.

...imenisikitisha sana hii...kwakweli twatakiwa kushukuru majaaliwa tuliyobahatisha.
 
...imenisikitisha sana hii...kwakweli twatakiwa kushukuru majaaliwa tuliyobahatisha.
Yeahhh wengine mnajiuliza mwende wapi kujipendelea ..wengine wanachambua mboga kwenye daladala!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
tips za kupunguza ugumu wa maisha

1.achana na maji ya chupa,chemsha ikibidi maji yako

2.punguza vocha za simu,sms zaidi

3punguza lunch na marafiki sana

4.punguza safari zisizo za muhimu

5.punguza kununua mfano juice za supermarket,tengeneza za home

6........nunua vitu hasa vyakula kwa jumla....

7.jitahidi ukae karibu na ofisi,upunguze gharama za usafiri

8 mengine malizieni basi
 
yan hv sasa kila kukicha hujui utakula wap na utarud sa ngap na unakwenda wap? Yan maisha yamekuwa magumu kila unachokiona ni pesa na kila unachokifanya kinahitaji pesa eehee mungu we yan watu hatulali tunafikiria maisha dah! Yan tumekuwa kama mbwa utakula kutokana na miguu yako
 
tips za kupunguza ugumu wa maisha1.achana na maji ya chupa,chemsha ikibidi maji yako2.punguza vocha za simu,sms zaidi3punguza lunch na marafiki sana4.punguza safari zisizo za muhimu5.punguza kununua mfano juice za supermarket,tengeneza za home6........nunua vitu hasa vyakula kwa jumla....7.jitahidi ukae karibu na ofisi,upunguze gharama za usafiri8 mengine malizieni basi
unachokisema upo sawa ila ukifanya hayo unayoyasema ndo yana hasara zaid mfano hlo la kutengeneza juice kwanza matunda ni garama sana na mbili ni muda wa kufanya hayo hautosh so tatzo lipo pale pale
 
Aisee Voice ulikuwa wapi, dah usiwe unatesa nafsi za watu kiasi hicho. Uwn unaaga basi. Maisha yanakua magumu kwa sababu yako bana. Ngoja nikufate huko.
Mhh..... samahani nilibanana na majukumu kidogo nilijua ningeaga nisingeweza kuchukua likizo kwa jinsi ninavyowamiss..., kwahiyo nilichukua hatua ngumu kwangu ingawa nilipanga likizo ya muda mrefu zaidi lakini kwa kuwamiss nimeshindwa... na imebidi nirudi..

hapa ni nyumbani hata nikipotea kidogo mwisho wa siku lazima nitarudi... nashukuru sana kukukuta LD nyie ndio mnafanya JF iwe nzuri kama ilivyo
 
Yeahhh wengine mnajiuliza mwende wapi kujipendelea ..wengine wanachambua mboga kwenye daladala!!!

...bana weee, mnh!
where_to_go_road_signs_postcard_customizable-p239806789465352698trdg_400.jpg

Mw'Mungu ashukuriwe tu.
 
duh! Haya maisha sasa yanaelekea pabaya, mngeendelea zaidi angetoa mchele apepete.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom