Dada zetu mna mambo II- Mnaposifia waume/wapenzi wenu kwa mashosti!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Ilianza kama utani. Mashosti wawili waliokuwa marafiki wa karibu tena walioshibana na kushibana. Walikuwa na urafiki wa kushinda pamoja, kwenda kununua nguo pamoja, na kwa kweli ulikuwa ni kama mtu na dadake hivi. Ukiambiwa alikuwa shosti wake, kweli alikuwa shosti. Huyo mwingine alikuwa hakeshi kumtaja "shosti" anapopiga soga na wengine. "Nilimuambia shosti bwana, alichekaa" ndio yalikuwa masimulizi yake.

Hilo halikuwa tatizo. Tatizo ni wale mashosti wengine ambao hawakuwa na ukaribu wanamna hiyo lakini walikuwa wanashirikishwa umbea na habari za kila siku wanapokuwa pamoja. Iwe wakati wa chakula cha mchana au wanapotoka Ijumaa Wikienda kwenda kujirusha. Mmoja wao akajikuta anachumbiwa na kuolewa na marafiki zake walionekana kweli wamemfurahia sana kumpata shemeji. Na kweli walitoa ushirikiano wote kuhakikisha kuwa harusi ya shosti wao inatikisa na kutingisha jiji!

Aliyeolewa katika kuendelea ule urafiki na ukaribu alijikuta haachi kuwaambia visa vya "Mume wangu"; kila sentensi yake ilikuwa inaanza na "mume wangu". Sijui ni kitu gani lakini mara kwa mara alikuwa anawagaia marafiki zake habari za yeye na mumewe na kwa ukaribu waliokuwa nao hata kabla ya ndoa alikuwa anawapa habari hata za "chumba cha maajabu" ambapo "maajabu hufanyika".


Hakujua kuna mmoja wa marafiki zake anamtia donge. Donge ambalo lilikuwa linakaa na kutulia kwenye koo ya huyo
shosti kwa kadiri siku zinavyokwenda. Maskini shosti wa watu akaanza kuingiwa na wivu. Mbona mwanamme kama mume wa shosti hayupo? Mbona wapenzi wote aliowahi kuwa nao hawaonekani kutenda kama yule mume wa shosti. Na inakuwaje yule mwanamme anaoneakna mwaminifu hivyo kwa shosti. Maswali ya mahusiano yake yalivyozidi ndivyo na macho yake yalivyozidi kumuangalia shemeji yake kwa macho yale yaliyokatazwa. Ilianza kama utani.

Utani utani hivi hivi mara ukawa si utani. Ilikuwa kwenye tafrija moja ambapo karibu genge zima lilienda huko na wale waliokuwa na wao nao walienda huko. Sijui ilikuwakuwaje lakini kama utani, akiwa amelewa (au alionekana amelewa) shemeji yetu akaanza vimbwanga, mara amtanie shemeji yake mbele ya mkewe na mbele ya marafiki na huku wote wakicheka. Na kama aliyezidiwa na kileo akasema neno moja ambalo macho ya kundi zima yalimgeukia "shemeji miye nakumudu wewe!" alisema hivyo! Wenzie wakamzoda na wakalaumu "pombe". Wakacheka na wakajikuta wanamlazimisha kuondoka pale.

Kesho yake anampigia simu shemeji yake kumuomba radhi.

"Jamani shemeji samahani sana kama nilikukwaza jana" huku akilegeza sauti.
"Ah hamna neno shemeji, we pombe haikufai"
"Kweli shemeji sijui dadangu hapa amefikiliaje"
"Ah zungumza naye"
"Hapana shem najua atakuwa amechukia ndio maana nilitaka nikuombe msamaha wewe"
"Hamna neno"

Walidhani vimekwisha. Kumbe shosti anapiga mahesabu. Siku moja akiwa anajua kuwa mama mwenye nyumba kasafiri shemeji akajipitisha nyumbani na kujifanya amesahau kuwa shosti hayupo. Akafika pale na mavazi ya mtego kidogo lakini hakukataa; ilikuwa ni "operesheni tamanisha". Kijana wa watu akatoa taarifa kwa mkewe kuwa shosti wake alifika kutembea. Hawakujali sana.

Ikaanza kama utani hivi.

Kwa ufupi, katika siku na mahali pasipotajwa mume wa mtu akatoka na rafiki ya mkewe; hapana haikuwa kama mara moja bali visafari vikaanza na mara mahusiano na mkewe yakavurugika. Maneno yakaanz akusikika, maskini mama mwenye nyumba hakujua hadi alipochelewa sana...


Ilianza kama utani; mke alimsifia mumewe kwa mambo ya chumbani kwa marafiki zake; kama sehemu ya utani tu.

Hakuwa anacheka tena. Ooh, haikuwa utani!


Maswali:
Hivi mdada unapojikuta unawashirikisha marafiki zako mambo ya ndani ya mwenzi au mpenzi wako jinsi anavyokuridhisha n.k unategemea marafiki zao waitikiaje? Waone ni burudani tu au wivu?
Hivi, ikitokea kuwa kule unakosifia ndiko unakoliwa utajilaumu hasa kama jinsi unavyosifia mapishi unafanya hata aliyeko mtaa wa tatu anuse harufu aje?
Kuna mipaka gani ambayo mwanamke anatakiwa kuwa nayo katika kulinda mazungumzo yake ya mambo ya chumbani kwa marafiki zake au akibania ataonekana kuwa si mshiriki mzuri?

Na. M. M. Mwanakijiji
 
Sjui kwanini wanawake wengine wanapenda kuongelea mambo yao ya ndani kwa mashoga,ivi huoni kama unamuuza mumeo?
nawaonea huruma sana sijui hawajafundwaa,au hulka tu yamtu na kujihashua....
 
Hapo ndipo tunapokosea kwanini mambo ya chumbani kuyatoa nje?
Kuna watu huwa wamekaa attention kukwapua mali za wenzao kama kipanga vile
Story za ushost zikomee huko huko
Na mambo ya Chumbani yabaki kuwa chumbani
Siku hizi hatuaminiani kabisa yakhe ,Ukisema cha nini mwenzio asema atakipata lini?
Unapoanza ooh mme wangu haniridhirishi ..mwenzio kimoyo moyo anasema mshenzi huyu ngoja nimtafutie nafasi mmewe nimfunze mahaba habati ndo akome
Unapoanza ooh mme wangu mjeuri mwenzio anasema moyoni saafi ushenzi wake ndo nauhitaji mie ..
Unaposema mme wangu anakibamia mwenzio anasema lah hiki kibamia nitakipataje nikitafutie dawa ya kikohozi nisijekohoa wakati wa majamboz kikachomoka..
Kwa kifupi ktk ndoa/mahusiano mambo ya chumbani yabaki kuwa chumbani
Na story za mtaani zibaki huko mtaani
Asante MM.
 
Mara nyingi inashauriwa kuwa, si jambo jema hata kidogo, kuzungumzia mambo ya ndani ya familia, hususan ya chumbani kwa watu baki. Hili limekuwa tatizo sana na wengi, wamezibomoa na wengine kuzifedhehesha familia zao kwa tabia kama hizi. Wapo baadhi ya wadada ambao wamekuwa wakitoa mpaka taarifa za "perfomance" za wenzi wao, either nzuri au mbaya bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo ni kujidhalilisha yeye na mwenzie kwa hao watu anaowasimulia.

Nakushukuru Mzee Mwanakijiji, yumkini mada hii itawabadilisha wadada (na wakaka kama wapo) wenye tabia kama hizi.
 
dah hii case inawatokeaga wengi sana, wanawake wanatakiwa kuwa makini sana haswa katika swala la chumbani kumsimulia shosti hajui kama anamtamanisha mwenzake ajaribu hafu mwisho wa siku wanafanya kweli.
 
Nilizani aliyepost ni Mimi Mwanakijiji,nikataka kumuuliza maada za cck na ccj zimeisha? Kumbe ni wewe Mzee Mwanakijiji haaaa waaambie hao madada ujumbe mzuri!
 
Wapo wanawake wanaopenda sana kujionyesha kwa wenzao kwamba wamejaaliwa waume wazuri hata kama ukweli ni kinyume.Utasikia mtu anasema kwa kujiamini
"...mi mume wangu hawezi kabisa kutoka nje, ni mwamimifu mno! Mume wangu hawezi"!
..."Unasema fulani anajipitishapitisha kwa mume wangu? Kwanza mume wangu hapendi wanawake dizaini hiyo!"

Bi dada kama wewe ni mmoja wa hao, ujue umeliwa maana hakuna anayeweza kumkania mtu! Ukizoea kujisifia ujue kuna watakaokulia timing kukuumbua.Kuna wanawake wao ni hobby kuteka "makoloni" ya watu.Jihadharini sana.Tena wanasema kabisa... sina haja naye huyo bwana, lakini nitamkomesha tu..namchukua kisha nambwaga!

Ndio maana wanaume wao hawanaga tabia za kujisifu kwa wenzao kuhusu wake zao maana wanajua lolote lawezekana.
 
Na hiii maneno huanza kwanza kwa kuongea umbeaaaaaaaaaa, wakiishiwa ndo wanaingia kwene mambo yao wenyewe. Na wanaume hatuna hiana bwana, akijilengesha, kitu na boksi!
 
kweli kabisa mkuu unayoyasema,
inaboa haswaa mtu tangu mkae kitako anamzungumzia tuu mume wake... ooh jana kanifanya iv, ooh juzi kanipeleka uku!
hakuna cha ushosti wala ushoga ki ukweli huwa hawafurahii hayo mastory ,kibaya ndos yake yy iwe inayumba mmh huyo lazima ajitahidi ayumbishe na ya kwako ili muende sawa lolz!
na ww uonje joto ya jiwe, wengi kweli yamewakuta afu wanaishia kulalamika wakisahau kuwa source ni wao wao.
limitation ni muhimu, ya chumban yaishie chumban na ya barazani yaishie barazan!
 
Sjui kwanini wanawake wengine wanapenda kuongelea mambo yao ya ndani kwa mashoga,ivi huoni kama unamuuza mumeo?
nawaonea huruma sana sijui hawajafundwaa,au hulka tu yamtu na kujihashua....
Yani we wacha tu nakumbuka zamani kabla sijaowa, nilikuwa na gf wangu lazima akanisifie navyo mfurahisha kwenye 6 x wale marafiki zake wakike nawao inabidi waje kujaribu pia :biggrin:
 
Wapo ambao wakisikia hayo maneno yao wanafanya kila wawezavyo ili wakajionee wenyewe, mwisho wa siku utasema shoga yako amekugeuka
 
Siku zote simwamini mwanamke yoyote mbele ya nimpendaye hata ndugu yangu,so ni marufuku kumpa nafasi ya kumzoea au ukaribu wa aina yoyote salam tu inatosha na hata wakishikana mkono lzm niwakazie macho ebo!!

Na hakuna cha ushosti wala urafiki linapokuja swala la wa ukweli wangu,
Tutaongea yote ya dunia hii kamwe hawatasikia kutaja jina na mpnz wangu kwenye story,
Na hata km ninalolinalonitatiza na nimekwama kudeal nalo mwenyewe mama yangu pekee ndio rafiki wa kweli ninayemshirikisha,

Namshukuru mama kwa elimu hii aliyonipatia kwan aliniambia moyo wa mwanamke unaweza kuficha mengi tofauti na akuonyeshayo uson mwake,
Asante Mzee Mwanakijiji kwa kunikumbusha tena hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom