Daah Ajira ngumu aisee!

kb52

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
336
109
Wajamen wana JF
Nimetumia kila mbinu kupata kazi sijafanikiwa. Nakumbuka nilikua nikitoa copies za vyeti na CV nyingi sana kama zaidi ya 200, nikaanza kua nazitembeza na kibegi changu cha kisomi huku nikiwa nimevalia nguo safi nadhifu za kiofisi. Nilikua nikiandika barua nyingi zisizokua na address ya ofisi but kila nilivyoona bango la ofisi nilikua nikikopi address yake na kwenda pembeni na kupaste kwenye barua mojawapo kati ya nilizokua nikiziandaa.

Kasheshe ilikua jinsi ya kuingia pale ofisi husika. Mlangoni getini mara nyingi nilimkuta mlinzi, "unashida gani?..unaenda kumuona nani?..sign daftari hili" hayo ni baadhi ya maswali niliyokua nikiulizwa. Nikifanikiwa kumpita japo wengine walikua wakinizuia katukatu, nakumbana na mtihani wa mwisho wa pale kwa sekretari wa boss..ofisini hapo. Hawa walikua wakiniuliza.."unashida gani?..ya binafsi au ofisi?"..ukisema ya kiofisi imekula kwako...watakuuliza "una appointment letter??"..ukisema huna basi ndio hutaweza kumuona boss. Kwani mimi nia yangu kubwa ilikua ni kumeet na mwenye mbwa tu. Mwanzon ilikua ngumu sana kumet nao sana kwani swali la kusema nna appointment na boss lilinishinda sana..nikawa nafel na kujikuta sipati fursa ya kumuona. Nikabuni mbinu ingine.

Safari hii...nilivyokua nikuulizwa na sekretari kama ni shida ya binafsi au kiofisi...nilisema shida ya binafsi, nikawa naulizwa tena. Unafahamiana na boss?..nikawa nawajibu kwa konfidens..ndio. Ananiuliza jina langu kisha boss anapigiwa simu...ngriiiii...halo boss Hamidu anataka kukuona...anasema wewe mnafahamiana..ni ndugu yako....boss nikawa namsikia anasita kidogo...Hamidu???..anyways mruhusu aingie.

Kimbembe ni kwa boss, it was funny...maboss wengi walifurahi sana, nikawa nawachana..nawaambia nyie ni wagumu sana kuwapata...na sometimes CV zetu hazifiki kwenu..ma PS au walinzi wanazichana. Niliongea yangu...wengine walikaribisha chai au chakula na wengine walinipa pesa ya nauli. But mwishoni niliwaomba Business card zao. Hapa nilipo nina zaidi ya 120 ya kadi. Wengi walinipa matumaini kua "kama wakitangaza watanikonsider"..wengine waliniambia nisubiri baada ya miezi kadhaa...etc etc blah blah kibao.

Nilikua nikiwasiliana nao kwenye namba zao za simu kuwakumbushia. Nikawa napigwa danadana tu..longolongo kibao. Wengine wakanichenjia niwape cash kidogo...na bahati mbaya sikua na chochote.

Nilikua nikitembea sana...maofisi mbali mbali ya Posta..Vingunguti na kote Dar es Salaam. Nilikua nikituma pia kwa njia ya posta barua zingine.

Nilifanya hivyo kwa njia ya analogia na digitali. Nimetuma mails nyingi sana za kazi. Hapa sasa hivi nilikua naangalia toka 2009 hadi sasa nimeshatuma mails 1999+ za maombi ya kazi bila mafanikio.

Nikajiunga na linkedin website, hapa nikameet na proffessionals wengi sana, maboss kibao...nikawanawatumia CV zangu direct. I mean..nikisikia nafasi imetangazwa...naingia linkedin..nawasiliana na mtu ambae anafanyakazi sehemu hiyo. So nakua like natuma maombi mara 3...kwa huyo jamaa...kwa mails ya ofisi na sanduku la ofisi.


Kuna mtandao pia nikifakiwa kuuona..unaitwa CEOs roundtable, hapa nilimeet na ma CEOs na kuwatumia resumes zangu bila mafaniko.

Kuna tovuti za kutafutia kazi kama zoomtanzania...proffessionalapproach. ...kazibongo...vijanatz...pataajira..kokorikoo...britermonday...mwananchi etc etc..nimekua nikizitembelea kila mara mpaka tovuti za nchi za uarabu.

Ilifikia kipindi niliamua kwenda kutafuta kazi mining, kwenda kusotea kazi. Kukaa pale getini na CV zako na kusubiria mzungu wa kampuni flani apite uchonge nae unampa CV lakin hola. Nakumbuka nilipata kazi Barrick Buzwagi kama Security Officer..siku ya kwenda kuripoti nikaambiwa jina halionekani. Daah

Kiukweli nimetumia mbinu mbali mbali sana. Hata kubeba matofali pale kona ya msamvu niliwahi kubeba pia. Niliumia mikono sana na mwili kukosa nguvu. Tofali moja kubeba ni sh. 25.

Sasa waweza kujiuliza elimu yangu ipo vipi?..kiukweli nna elimu ya kawaida tu. Nilisoma seminary na kupata alama nzuri tu za form 4 na six vilevile, chuo nikasoma mara mbili....advanced diploma ya accounts na postgraduate diploma ya accounts.

Nasikia tu watu wanasema vijana rudini vijijini kwenu mkalime, wengine...vijana mjiajiri.....hapa ndo nachanganikiwa kabisa. Naanzaje anzaje sasa kwa mfano... hebu tuambiane wadau....wa yeyote aliyepitia situation kama yangu aseme katokaje. Kwani hapa nipo nipo tu kama lipicha la michelini au lisanamu la bunduki la pale posta. Nimeganda....
 
Kuna jamaa kama we ila yeye alisomea mambo ya insurence akasota mwaka 1 baadae akaenda kusoma diploma ya ualimu. Chuo cha serikar baada ya kupata kaz ya ualimu. Akawa anasota taratibu kusaka kaz ya fani yake mungu c athumani jamaa akaonga pesa akaingia TRA sasa hv anasoma master pale open unversity
 
Ngumu kumeza afu Noma sana!!!..boyaboya wanasonga tu. .we unabaki umeganda tu kama lipichapicha tu.
 
Duh pole mwana. Tatizo inawezekana nafasi zipo ila kwa picha ya waajiri walio wengi mtu ukiwa na accouting tu nayo ni shida. Ndiyo maana Accounting and finance inakuwa na maana zaidi kwenye soko la ajira. Suala lingine, kutuma CV kama uyoga kwenda kwa kila mtu nayo inaweza kuwa usumbufu kwa hao mabosi. Nadhani labda ungejribu kuiweka CV yako more professional, pia tafuta sehemu ya japo ujitolee bure. Ila Pole sana.
 
Muda wote naheshimu mawazo yako na nashukuru kwa mchango wako. Labda kuongezea hapo...nilikua nikituma maombi yangu kwa nafasi zilizokua zikitangazwa na pia nilikua nikituma na kuomba kazi hata sehemu ambazo hawajatangaza nafasi za ajira ili mradi tu CV yangu ibaki katika kumbukumbu zao na kuweza kupata kazi kiurahisi pindi watakapohitaji watu.


Kwa mwaka 2012...nilikua nikiitwa kwenye interview kila mwezi from january to december...na kila mwezi nilikua naitwa interview 2...na sijafanikiwa. Mfano... TCAA...NSSF..TOLL...tanesco...African Barrick....yani sehemu mbali mbali..ofisi kubwa kubwa. Nilikua nabadili aina mbali mbali ya CV na Cover letters...ambazo zilinifanya niitwe mara kwa mara. Nina vyeti vya kujitolea..sehemu kama Bungeni..dodoma...Mpwapwa District council..etc etc...ninavyeti vya safety...fire..firstaid....chemical and synide...leaderships..etc etc ambavyo nilivipata ktika trainings....so utaona ni kwa jinsi gani nilivyo. Hapa sasa ninachofanya ni kuomba kazi na zile za kuvolunteer. But majibu hayatoki...mfano za Sumatra...tra..tpdc..iita..etc etc ambazo zilitoka mwezi majuz...majibu yakunaja mavimavi tu....we acknowledge sijui nini nn...yani mavimavi tu wananijibu. Na hasira sana hapa kaka.
 
Pole sana kamanda maana Maelezo yako yanaweza kutengeneza movie ya ukweli holiwood.Mi naona mtafute Mwigulu anaweza kukuwezesha si anaandaa muswada binafs kuhusu ajira kwa vijana wasomi
 
pole mkuu kb52 maana tunashinda wote hapa JF kumbe mwenzetu bado jobless,ila usikate tamaa Bado nafasi ingalipo!
 
Last edited by a moderator:
Kaka pole sana, jitolee tu mwisho wa siku utapata kazi nzuri, kuna dada mmoja alikuwa anajitolea NSSF miaka 3 sasa kapata kazi hapo hapo hivi karibuni. Usikate tamaa ipo siku yako.
 
Tatizo mimi nipo Chadema. Jamaa hata kua na msaada kwangu.
 
Polisi sitaki kabisa kuwasikia. Jamaa waliwahi kunivuta korodan zangu. Sitaki kabisa hata hilo jina. Mavi mavi tu wale
 
Kazi nazitafutia kwenye magazeti..mitandaoni...mfano..hapa...linkeldin..zoomtanzania....kazibongo...britermonday....pataajira....vijanatz...etc etc....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom