MJUKUU WA KACHUNDU
Member
- Nov 6, 2012
- 48
- 23
Habarini waungwana,
Jana Jmos mie pamoja na Family yangu tulikwenda shambani ni katika kuitumia likizo yangu nikaona ni vema nikasaidie kazi za Shamba kidogo..na pana umbali wa kama km 72 toka nyumbani mpaka Shambani tulikwenda kuvuna mbaazi,kutokana na umbali huo na Shamba lipo polini ilitulazimu kuvuna na kuzibeba mpaka nyumbani sasa wakati tunarudi mishale ya saa 4 au 5 kasoro hivi tulikutana na polisi wa dolia wakanisimamisha wakaniomba kadi ya Gari nikawapa,leseni,nikawapa,Gari vibali vyote viko Sawa ila kama unavyojua wenzetu Hawa hawaishiwagi ngonjera... Wakaanza ooh kwann ninasafirisha mazao usiku,nikawauliza mashamba yanakuwaga mjini? Na nisingeweza kulala Shambani na familia kwasababu ni polini,pia Nina usafiri binafsi na muda haukuwa mbaya sana wa kunifanya nisirudi nyumbani,na istoshe siyo mazao ya biashara natoka kuvuna ...Mara oooh peleka Gari kituoni,Mara ooh huyo in baba yako kweli? Siyo baba yako sasa makosa mengine mapya kwa kweli..
Ila mwisho wa siku una tsh ngapi? Nkajiuliza kwa kosa lipi la mie kuvuna? Au la kutokulala Shambani? Baada ya kamzozo ka muda mrefu na nilikuwa na wanangu ndani ya Gari watu wamechoka kwa kazi za kutwa nzima nikaona isiwe Shida chukueni hii Elfu kumi tsh.10,000/= ingawa niliitoa huku roho inauma maana usawa huu daaah sijui siye wakulima twende wapi...JAMANI POLISI KUWENI NA KAUBINADAMU KIDOGO mmefanya Leo wanangu wanapigwa miayo tu kale ka 10,000/= ndiko kaliko kuwa mfukoni mpaka niuze mbaazi lini sasa...mjue Mungu anawaona jamani...daaah.