Elections 2010 Daa ni hatari kumbe kweli JK aliiba kura....

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,739
744
Habari wana jf
ninaye mjomba wangu mjeda kikosi cha navy nilikuwa sijaonana naye tangu uchaguzi uishe.
Basi nilianza kumuuoiza kuhusu siasa wao kama wajeda wanamsimamo gani na hali ilivyo sasa? Akanza kuniambia kuwa wanajeshi wote wa ngazi za chini hawaifagilii ccm na serikali yake mengi wanakuwa commanded na wakubwa wao. Akasema hata uchaguzi mkuu jk alinguka vibaya na wajeda waligawanyika sana lakini wakubwa walikomand masanduku ya kura ya bebwe kwa kutumia magari ya jeshi kwani huwa hakuna mtu wa kuhoji.
 
Daah mjeda ANAJUA MENGI, sasa mpeleleze kama anahata picha za matukio hayo ama nyaraka hata moja kuweza kujustfy hilo.
Kwakua mimi najua waliiba , ila ushahidi umekua haba
 
Kwani hamjasikia ya Zimbabwe, kuna wapiga kura hewa milioni 2 na ushee.
Serikali za nchi za Kiafrika dugu moja
 
Muda wote huo ulikuwa hauna info? Uko dunia nyingine kabsa ndg yangu.
 
Mapungufu kabla ya kupiga kura yalikuwa wazi,watu mbali mbali waliyalalamikia bado wananchi wakajitosa kupiga kura,sasa tunalalamika nini?tulitegemea miujiza?
 
Inawezekana kweli JK alichakachua maana vurugu zinazoendelea ndani ya magamba inaonekana wazi mshikaji aliumizwa sana na matokeo hayo hadi kufikia hatua ya kutaka kujua chanzo ni nini. Lakini nawashauri muwe makini na huyo msoja maana baadhi ya wajenda hasa wa vyeo vya chini wanapenda sana fix. Msije kuingia mkenge bana. Kwani hamjasikia wanavyosimulia mafanikio yao kule Anjuane (Sikumbuki vizuri jina lakini ni Commoro) wakati inasemekana hata risasi hazikutumika kwa kuwa yule jamaa alisepa mapema.

Daah mjeda ANAJUA MENGI, sasa mpeleleze kama anahata picha za matukio hayo ama nyaraka hata moja kuweza kujustfy hilo.
Kwakua mimi najua waliiba , ila ushahidi umekua haba
 
Inawezekana kweli JK alichakachua maana vurugu zinazoendelea ndani ya magamba inaonekana wazi mshikaji aliumizwa sana na matokeo hayo hadi kufikia hatua ya kutaka kujua chanzo ni nini. Lakini nawashauri muwe makini na huyo msoja maana baadhi ya wajenda hasa wa vyeo vya chini wanapenda sana fix. Msije kuingia mkenge bana. Kwani hamjasikia wanavyosimulia mafanikio yao kule Anjuane (Sikumbuki vizuri jina lakini ni Commoro) wakati inasemekana hata risasi hazikutumika kwa kuwa yule jamaa alisepa mapema.
Ahsante sana mkuu... umenichekesha sana mbavu sina ... ni kweli. Masoja (hasa hawa wa ranks za chini wana fix sana.
 
Huo waweza kuwa ukweli, wizi ulifanyika na inafahamika hivyo ila cha kushangaza ni hao wanaosaidia kuiba kwani ni wavuja jasho kama tulivyo
 
  • Thanks
Reactions: oba
Kwani hujui kuwa magari ya jeshi ndo yalikuwa yanatumika kubeba masanduku ya kura? Yalikuwa yanakesha kusafirisha kura na ole wake mwandishi ayapige picha!
 
Jamani mbona hili jambo la JK kuiba kura si geni, ni kweli kura waliiba. Hili linadhihirishwa na baadhi ya matokea ya ubunge kutaka kupinduliwa na kukutana na hasira za wananchi. Mfano Arusha, Mwanza, Mbeya n.k. Kwa wale walioshiriki uchaguzi wa 2005 wananchi walikuwa wanasema Rais ni JK kwa 100% ila mbunge ndiyo ilikuwa inawezekana CCM au upinzani, sasa ukija 2010 ikawa kinyume chake, Rais CHADEMA, mbunge CHADEMA/upinzani au CCM. Kwa mazingira hayo asingeiba kweli leo hii Rais angekuwa Dr Slaa.
 
Habari wana jf
ninaye mjomba wangu mjeda kikosi cha navy nilikuwa sijaonana naye tangu uchaguzi uishe.
Basi nilianza kumuuoiza kuhusu siasa wao kama wajeda wanamsimamo gani na hali ilivyo sasa? Akanza kuniambia kuwa wanajeshi wote wa ngazi za chini hawaifagilii ccm na serikali yake mengi wanakuwa commanded na wakubwa wao. Akasema hata uchaguzi mkuu jk alinguka vibaya na wajeda waligawanyika sana lakini wakubwa walikomand masanduku ya kura ya bebwe kwa kutumia magari ya jeshi kwani huwa hakuna mtu wa kuhoji.
haya majungu kwa sasa hayana nafasi. leta post zenye tija na wakati uliopo.kwani hicho ni kilio cha mbwa aliyekosa,hubaki anabweka tu mbweko ambao haumsaidii boss wake.subiri ushuhudie muanguko wa ukweli kwa chama chako uchaguzi ujao.huyo mjeda huenda ulikuwa unaongea nae akiwa amepuliza msokoto wa bangi na likiwa linamkolea.jitahidi kuleta post zenye manufaa zaidi kwa mtanzania
 
Haya kaka Nape tumekusikia! Una swali la nyongeza?
 
Back
Top Bottom