Cyrill radcliff mwanasheria kutoka london aliyeigawanya india na pakistan

Masikio Masikio

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
1,840
3,376
Baada ya vita vya pili vya dunia uingereza kutoka na kutumia hela nyingi sana kwenye vita waliona ni mda muafaka wa kupunguza baadhi ya makoloni moja wapo likawa ni india

Kwa kipindi ambacho mwingireza ametawala india aliona itakua ngumu kwa jamii mbili za waislaimu na wahindu kukaa pamoja kwa akapendekeza kuwepo kwa nchi mbili moja ya waislamu na nyingine secular ya dini zote

Kazi hiyo ilipingwa kufanywa kwa mda wa miezi minne lakin baadae kutoka na ufinyu wa budget ikabid wafanye kwa week tano

Mfalme wa uingereza baba yake malkia elisabeth aliyefariki alimchagua mwanasheria kutoka london cyrill radcliff ambaye hakuwa kufika india katika maisha yake yote in short alikua hapajui india

Cyrill Radcliff alienda india kuanza kazi kwa sababu hakuwai ishu india na hapajui alitegemea zaidi taarifa za sensu kwenye kuchora mipaka ila eneo la kasmir na hyderbad aliiambiwa aliache kwa sababu kasmir walipewa uhuru wawe nchi au wachague wajiunge na india au pakistani

Cyrill radcliff alimaliza kazi yake baada ya week tano lakin alichora mipaka pasipo kuwauliza wenyeji ilipelekea mtu shamba lake kuwa pakistan na nyumba kuwa india. Baada ya kumaliza kazi cyrill radcliff alirudi london na hakuwahi kurudi tena india au pakistan mpaka umauti ulipomkuta- japokua alikosolewa lakin radcliff anaamini mda aliopewa ulikua mdogo kwa hiyo asilaumiwe sana

Alipomaliza india ndo ya kwanza kupewa uhuru na baada ya siku tatu mbeleni pakistan wakapewa uhuru- kulitokea umwagikaji wa damu mkubwa sana sababu kulitokea vujo hakuna takwimu za kweli kwa waliokufa ila wengi wanaamini walikufa watu wengi

Baada ya uhuru wa nchi mbili hyderbad waliiamua kuwa sehemu ya nchi ya india, ila kasmir kuna maeneo ilikua inatawalia na familia ya kihindi ile familia iliamua kukabidhi baadhi ya eneo kwa serekali ya india bila kupata idhini ya wanachi wake ambao wengi ni waislamu na eneo mpaka leo linatambulika kama india administered kasmir wale hawakukubali na mpaka leo wanataka haki yao ya kuchagua kuwa upande wanaotaka kama alivyosema mkoloni mwingireza iheshimiwe ila serekali ya india imegoma ndo maana machafuko yanaendelea mpaka leo

Upande wa magharibi kuna eneo la kasmir wao walijikabidhi kwa pakistani sababu familia iliyokua inatawala kule ilikua ni ya kislamu na eneo hilo linatambulika kama pakistani administred kasmir
 
Back
Top Bottom