CWT wazuiwa kumchagua Katibu Mkuu, Mweka Hazina

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,457
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imepokea ombi la zuio la kimahakama linalotaka Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) usifanye uchaguzi kwa nafasi za katibu mkuu na mweka Hazina.

Leo Alhamisi Machi 16, 2023 waliokuwa viongozi wa CWT, Deus Seif (Katibu Mkuu) na Abubakar Allawi (Mweka hazina) walifungua shauri la maombi namba 2 la mwaka 2023 kupinga uchaguzi huo.

Kesho Machi 17, 2023 CWT watakuwa na uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ambazo ni Mweka Hazina, Mweka Hazina msaidizi, Mjumbe Kitengo cha Wanawake na Katibu Msaidizi.

Hata hivyo, nafasi ya Katibu Mkuu haikuwa imetangazwa tangu mwanzo baada ya aliyekuwa Katibu Msaidizi Japhet Maganga kuchukua nafasi hiyo kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili awali Seif.

Akizungumza kuhusu pingamizi hilo, Wakili wa wapeleka maombi Nashon Nkungu amesema tayari Jaji wa Mahakama Kuu Gerson Mdemu ameshapokea ombi hilo.

“Kimsingi sisi hatupingi mkutano na wala nafasi zingine zote zitakazokuwa na uchaguzi, tunachokifanya hapa ni kupinga uchaguzi wa nafasi hizo mbili kwani bado kuna shauri ambalo linaendelea mahakamani kwa hiyo tusingeweza kuruhusu,” amesema Wakili Nkungu.

Hivi karibuni Mahakama Kuu iliwafutia kesi Allawi na Seif ambao walishahukumiwa na kutumia kifungo baada ya kueleza kuwa walitiwa hatiani kimakosa.

Mbali na hilo, wawili hao walifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma wakiomba tafsiri ya kisheria kuhusu kitendo cha Mkutano Mkuu wa CWT wa 15 na 16, 2022 kujadili majina yao wakati kulikuwa na zuio la kimahakama kesi ambayo bado inaendelea hata sasa.

Mkutano wa kesho Tanga utaongozwa na Rais wa CWT, Leah Ulaya na Katibu Mkuu Japhet Maganga ambao waligomea uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi za Ukuu wa wilaya wakitaja kuwa na majukumu makubwa ndani ya chama hicho.
 
Hao Cwt kwa miaka mingi wamekuwa engineers wa kuchochea migogoro kwenye vya vingine vya kutetea walimu lengo likiwa ni kuendelea kumonopoly walimu wakose nafasi ya kujiunga na vyama vingine .Halafu leo wao kwa wao wameanza kuzinguana kwa sababu ya kulinda maslahi binafsi na si walimu walio na matatizo lukuki
 
Hawa wapuuzi wanataka mpaka kutoana roho, kisa tu hela za walimu wenzao!
 
Back
Top Bottom