CUF: Taarifa kwa waandishi wa Habari juu ya Kujiuzulu Mwenyekiti Prof. Lipumba

Ninaweza kumuelewa Slaa japo kidogo lakini siyo prof. Lipumba, alikuwa hana sababu ya msingi hadi kusababisha kujiuzulu.

Haiingii akikini mtu mzima kama prof. kujiuzulu kisa eti Chadema imemkaribisha mwanachama asiyemtaka yeye m/kiti wa chama kingine lazima kuna nguvu nyuma, ila atambue pamoja na vyote alivyoahidiwa amejishushia heshima kitaifa na kimataifa.

unamuelewa slaa kvp na usimwelewe lipumba kvp, kama nawe si unafiki na ubaguzi, lipumba kavumilia mangapi, we unajua kiwango alicho kwazika,?penda kuheshimu maamuzi ya mtu yeyote,iweje maamuzi ya slaa umeona sahihi na isiwe kwa lipumba ili hali wote walishiriki mchakato huu unaondelea. Acha kujifanya hamnazo kuwa bright person with right opinion
 
Safari njema Lipumba, maamuzi yako yanatoa nafasi kwa chama kupata kiongozi mpya mwenye mawazo mapya ya kukikuza!! Tunakushukuru kwa kutufikisha hapa!
 
Siyo bure Lipumba the prof. Ameamua kusaliti UKAWA kwa ajiri ya kutunisha mfuko...dhamira yako inakusuta Lipumba.Haiingii akilini kumkalibisha EL na kutoa nasaa juu kwa huo ujio ghafla tu utashi umekurudia unawakandya wapambanaji wenzako...umekula maharage ya wapi Lipumba?

Dr.Slaa najua upo kwenye wakati mgumu, pengine kutishiwa maisha kwa kukataa kuhongwa Kama prof. Endelea kusimamia unachokiamini maana rushwa inakufanya kuwa mtumwa.

Pole tupo pamoja, Dkt. UKAWA mbele!!!!
 
Lipumba ni mnafiki sana angekuwa baba yangu ningeona aibu sana kuwa na mzazi wa aina yake
 
Namheshimu prof. kwa taaluma yake lakini sio kwenye siasa.

Lipumba alikuwa hana watu kaondoka yeye kama yeye, pale Lipumba alikuwa kama boya nakuhakikishia hatakuwa na impact yeyote CUF, angekuwa Seif ndiye kajiuzulu muda huu tungekuwa tunasema mengine.

Mngalisema mengine Kwa kuwa mnajua katika nchi hii Maalim Seif ndie mpinzani wa kweli na ambae CCM wanajua hawana mbinu yeyote ya kumshawishi akashawishika!

Si unaona ya kuwa tokea CCM wamfukuze kwenye chama basi nyote yake inazidi kung'ara badala ya kufifia
 
Jussa sasa awe mwenyekiti yeye tu tujue moja maana ndio wanakipeleka peleka chama kama shamba lao yeye na maalim seif
 
HABARI ambazo siyo rasmi ni kwamba LIPUMBA baada ya kuongea na waandishi wa habar kaenda moja kwa moja Airport na kuelekea kusikojulikana..

hapa buguruni hali si shwari katika makao makuu ya CUF watu ni wengi hawaamini kilichotokea kujiuzuru kwa MH. LIPUMBA.
 
Jussa sasa awe mwenyekiti yeye tu tujue moja maana ndio wanakipeleka peleka chama kama shamba lao yeye na maalim seif

Kwani wewe ulitoa shilingi yako wakati CUF inaanzishwa!?

Kama unaona Jussa na Maalim wanakipeleka chama kama shamba lao, kwanini huanzishi chama chako na wewe ukapata shamba lako?

Muige Hamad Rashid yeye kaanzisha shamba lake ADC.
 
Kuna vitu vingine havifai kujadili mbele ya watu wenye akili timamu, likitokea jambo watu wamenunuliwa, hivi dr. slaa naye kapewa kiasi gani na kwa lipi umpe Lipumba hela, kama watu wananunuliwa na wanakubali kirahis hivyo basi ccm wameshashinda tayar kwan wanaweza kuwapa hela watanzania wote, tusijishushe kiasi hiki kwa hoja za kununuliwa hata hao ccm wanajua ni kazi bure kwan kura ni siri ya mtu, so hata ukiwapa hela ni bure tu. Prof Lipumba hawez kununuliwa kirahis hivyo yeye ameamua kusimamia yale anayoamini hili la Kikwete sijui kununua watu ni hoja muflisi kabisa.

we jamaa mbona una akili sana una hakika hatuna undugu kweli???
 
CUF ni maalim bwana

CUF ni chama cha siasa ambacho wenyewe ni wanachama walioamua kukifuata miongoni mwa watanzania maalim Seif akiwa ni mmoja wapo.

Sasa unaposema CUF ni maalim unakosea Sana maana yeye peke yake katu hana uwezo wa kukifikisha chama hapa kilipofika.
 
Kwani wewe ulitoa shilingi yako wakati CUF inaanzishwa!?

Kama unaona Jussa na Maalim wanakipeleka chama kama shamba lao, kwanini huanzishi chama chako na wewe ukapata shamba lako?

Muige Hamad Rashid yeye kaanzisha shamba lake ADC.

Loud and clear, ubarikiwe sana mkuu
 
Back
Top Bottom