CUF, CHADEMA wamshangaa Nape

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Dunstan Bahai

VYAMA vya Wananchi (CUF) na Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) vimesema vina historia ya kuuchukia ufisadi na kwamba havina sababu ya kutumiwa na mtu au kiongozi yoyote katika kufichua mafisadi wote.

Kauli hiyo ilikuwa ikijibu kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM Bw. Nape Nnauye jana kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Bw. Nnaye alinukuliwa akisema kwamba vyama hivyo vinatumiwa na pia ni mawakala wamafisadi waliomo ndani ya CCM katika kumchafua na kumpaka matope Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na Majira jana, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa amestaajabishwa na kauli hiyo ya Bw. Nnauye kwani wao wamekuwa mstari wa mbele na wanayo historia ya kutangaza na kuwafichua mafisadi nchini.

Chama chetu kina historia ya kuchukia ufisadi, na tumekuwa mstari wa mbele katika kutangaza sera zetu zikiwemo za kuuchukia ufisadi kama ule wa manunuzi ya rada, ndege ya Rais, mikataba mibovu ya madini, EPA, IPTL na ufisadi wa ina yoyote hiyo na mstaajabu huyu kijana kama kweli ametoa hiyo kauli, alisema Profesa Lipumba.

Alisema kuwa hakuna kiongozi au mtu yoyote atakayewatumia wao kama chama, kama wa kuchafua watu wengine kwani chama chake kinajinadi kwa sera zake na hata masuala ya ufisadi nayo yamo kwenye sera za chama chao.

Akizungumza kwa niaba ya CHADEMA, Katibu Mtendaji wa chama hicho, Bw. Victor Kimesele alisema kwanza Bw. Nnauye siyo saizi yake na kwamba hiyo kauli ni ya mfa maji.

Huyu kwanza siyo saizi yangu, hizo kauli ni za kutapatapa tu kwani Chadema ilipowataja mafisadi haikutumwa wala kutumiwa na mtu na hata huyo Rais Kikwete alikuwemo kwenye orodha ya mafisadi tuliowataja," alisema Bw. Kimesera.

Huku akiangua kicheko cha kuashiria kuidharau kauli hiyo ya Bw. Nnauye, Bw. Kimesele alisema kuwa Nnauye anaona hodari kuzungumza sana kwenye vyombo vya habari lakini spidi aliyoanza nayo itakwisha.

Kwa mujibu wa Bw. Kimesele, CHADEMA itaendelea kuwataja mafisadi na itaendelea kuwaeleza wananchi jinsi wanavyoharibu uchumi wa nchi.

Alisema kwamba wao wenyewe kwa wenyewe wanajuana mafisadi ni wa kina nani na ndiyo hata kwenye vikao vyao wananyoosheana vidole.

Katibu Mtendaji huyo wa CHADEMA alisisitiza kwamba chama chake ndicho chenye historia ya kutamka hadharani mafisadi na kwamba hata kwenye orodha ya waliyo nayo wamo viongozi wa juu CCM.

Alisema pamoja na kauli ya Nnauye, lakini wataendelea kuwafichua mafisadi na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwajua walipo na wanachokifanya katika kuuhujumu uchumi wa Tanzania.
 
Mwacheni dogo atange na njia akikua ataacha!!!!!!!!!! Mtoto siku zote akinunuliwa mdoli siku za mwanzo mwanzo si mnajua tena, hakuna hata watu kunywa maji tena mitaa yote!!!
 
Napy Mwandozya unacheza ngoma ya kitoto na siku zote ngoma yaya kitoto haikeshi.Hakuna chama cha upizani kinachoweza kupokea hiyo mizoga,hao saizi yao huko huko CCM, tunajua mchezo mnao cheza. Kama kweli nyie ni wanaume wa shoka wapelekeni mahakamani na warudishe vijisenti walivyofisadi.Na kama kweli sheria itafuata mkondo, basi na JK lazima awemo kwenye mkumbo wa kwenda jela
 
Huyu Nape anakera sasa wapinzani wanatetea mafisadi ilihali ccm bado inawahifadhi,amwulize mwenyekiti wake kwanini wasubiri siku 90 hayo ni madhaifu ya mwenyekiti wao.Mwenyekiti wa kweli alikuwa Nyerere na aliondoka na ccm yake safi si hii ya watu walafi wa mali za umma macho yamewatoka na wamejaa fitina
 
Kabla ya kumshambulia nape mwambie Mbowe arudishe 200 mil. ya Lowassa, na gazeti lake la tanzania daima liache kumsafisha lowassa...

Ni vizuri chadema wakamchukua kabisa lowassa wakiona anafaa!
 
Back
Top Bottom