CT scan MRI Muhimbili Buree

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
Muhimbili yapunguza gharama za vipimo

Na Otilia Paulinus
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepunguza gharama za vipimo vya matibabu kwa wagonjwa wa rufaa.

Vipimo vilivyopunguzwa gharama hospitalini hapo ni vipimo vya aina mbili; ambavyo ni MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, vipimo vilivyopunguzwa gharama ni kiitwacho MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.

Lengo la kupunguza gharama hizo, Aligaesha alisema ni kuwafanya wagonjwa waweze kumudu gharama za vipimo hivyo na kuanza matibabu mapema.

“Awali kipimo cha MRI kilikuwa kinagharimu Sh 350, 000, lakini sasa kimeshuka hadi 100,000 na kile cha CT Scan kilikuwa kinagharimu Sh 170,000 na sasa kitakuwa kikigharimu Sh 50,000 kwa wagonjwa watakaokuwa wamepata rufaa ya kutibiwa hapa Muhimbili wakitokea Hospitali za Wilaya na Mkoa.

“Kimsingi punguzo hili limeanza tangu mwezi uliopita na hili limekuja baada ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutaka kuifanya Muhimbili kuwa Hospitali Maalum ya kutoa vipimo vikubwa ambavyo hapo awali havikuwapo.
“. .

Hili punguzo limeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Muhimbili na MOI
 
CT scan inagharimu sh 300,000/- katika hospitali za Private kama Regency, Aghakan. na kwa sasa Muhimbili ni sh 50,000/-
MRI inapatikana Muhimbili na Aga Khan tu kwa Tanzania.
Aga Khan sh. 500,000/- Muhimbili Sh. 100,000/-
 
CCM OYEEEE....!
Natoa pongezi zangu za dhati kwa serikali ya CCM chini ya makamanda KIKWETE,MUKAMA,NAPE et al kwa kuwezesha yote hayo
 
CT scan inagharimu sh 300,000/- katika hospitali za Private kama Regency, Aghakan. na kwa sasa Muhimbili ni sh 50,000/-
MRI inapatikana Muhimbili na Aga Khan tu kwa Tanzania.
Aga Khan sh. 500,000/- Muhimbili Sh. 100,000/-
this is a good news kwetu... what we need to struggle now ni kuboresha customer service and equipment maintenance and repair... BTW, huu ni ule msaada wa ABBOTT au ni pesa za wananchi ndizo zilinunua mashine?
 
Nimewahi kusikia kuwa CT scan ina madhara kwa binadamu,yaweza kusababisha matatizo ya figo na saratani na tatizo ni ile midawa wanayokutia kwenye mishipa.Kuna yoyote mtaalam wa hiyo kitu atujuze?
 
SERIKALI YA CCM ISIPOSEMA......wapo watakaodaka hoja na kusema uwongo....NA UWONGO UKISEMWA MARA NYINGI HUGEUKA UKWELI
 
Muhimbili yapunguza gharama za vipimo

Hili punguzo limeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Muhimbili na MOI
Punguzo sawa, je huduma itapatikana? Au ndo yaleyale ukifika unaambiwa machine ina matatizo inabidi usubiri wiki mbili au nenda Regency! Na tatizo la mgonjwa ambaye nature ya tatizo lake tu haihitaji CT wala MRI, na akiambiwa anaona kakataliwa.

Tusubiri kuona foleni itakavyokuwa ndefu!
 
SERIKALI YA CCM ISIPOSEMA......wapo watakaodaka hoja na kusema uwongo....NA UWONGO UKISEMWA MARA NYINGI HUGEUKA UKWELI
umeanza kuniudhi kwa kuleta siasa hapa... hii effort imekuja baada ya kuona mamashine yanakua white elephant mkuu

na ni lazima patakua na watu wa maana (tunawaita development partners) waliokomalia haya

bima ya NHIF au za maofisini hazilipi hivi vipimo na wazazi na wazazi wa wazazi wetu wanatumia hivi vipimo and they can not affort
 
duh bonge la nafuu ila kwa wengine ni mzigo bado inatakiwa ifanyike buree kwa wasio na uwezo!Kingine nacho hofia hapo isije kufanyika hujuma ya kuharibu hizo mashine ili kule private wapate nao kazi duh wewe unatoa huduma laki 5!sio mchezo
 
hakuna nafuu yoyote kuna watu ambao hawana uwezo na wanahitaji tiba
niliwahi kwenda KCMC kwa kipimo cha CT scan gharama ilikuwa 120,000 pembeni kulikwana
na mgonjwa anatakiwa kufanyiwa kipimo hicho lakini hakupewa huduma kwa vile hakuwa na pesa
ungeniambia kinatolewa bure ningesifia serikali lakini kwa gharama ya 100,000 mmmmmmmmmmmh
 
Punguzo sawa, je huduma itapatikana? Au ndo yaleyale ukifika unaambiwa machine ina matatizo inabidi usubiri wiki mbili au nenda Regency! Na tatizo la mgonjwa ambaye nature ya tatizo lake tu haihitaji CT wala MRI, na akiambiwa anaona kakataliwa.

Tusubiri kuona foleni itakavyokuwa ndefu!
Foleni haikwepeki mkubwa, mashine ni moja ya serikali, ipo muhimbili, Dsm population about 5million, Tanzania population about 40million.
Mashine ni moja.
Ukiambiwa njoo wiki ijayo, ulipe 100,000/- ufanyiwe au uende aga khan ulipe 500,000/- you will weigh the two option kulingana na afya yako itavyoruhusu.
 
hakuna nafuu yoyote kuna watu ambao hawana uwezo na wanahitaji tiba
Think straight, MRI toka 350, 000 na 100,000? hamna nafuu yoyote?
CT scan 170,000/- na sasa 50,000/-
Haihitaji kujua aljebra kung'amua.
 
duh bonge la nafuu ila kwa wengine ni mzigo bado inatakiwa ifanyike buree kwa wasio na uwezo!Kingine nacho hofia hapo isije kufanyika hujuma ya kuharibu hizo mashine ili kule private wapate nao kazi duh wewe unatoa huduma laki 5!sio mchezo
Kwa pressha ya wagonjwa Mashine tangu iwe installed inapiga kazi 24/7! No breather!
Weka logic hapo.
 
bima ya NHIF au za maofisini hazilipi hivi vipimo na wazazi na wazazi wa wazazi wetu wanatumia hivi vipimo and they can not affort
With the current punguzo all NHIF clients irrespective of their insuarance category (green/brown/etc) have CT and MRI services at their disposal
 
jee ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kutoa sh 100 000?

Wewe na mimi tunaweza kulipa 100,000 for MRI lakini hatuna uwezo wa kulipa 350,000/- ya awali.
Kwa watakaoshindwa kulipa hata hicho kiwango kuna idara maalum ya msamaha inayoshughulikia matibabu yao ikijumuisha vipimo, dawa, consultations hata chakula na ikibidi nauli na escort ya kurudi Urambo nyumbani alikotoka.
 
apo...
sio rahisi kwa wote wanaopata huo msamaha ukilinganisha na idadi ya hao "wasio na uwezo" wa kulipa ngaa elfu 20
nipo katika icho kitengo cha msamaha na wanarudi wengi tu kufia home,
ni wagonjwa wa HIV tu napo unafuu upo kwa kutolipia costs ingawa kwa mbinde kweli.

ingawa km usemavo walio na uwezo huo ambao ni wachache vs wengi maskini
bado tuna mwendo mrefu sana ktk huduma za afya Tanzania
 
Back
Top Bottom