CRDB BANK si Bank ya kuiamini kabisa!

Hiyo michezo kwenye mabank yetu nilishaishtukia siku nyingi mno! Siku hizi mimi kwenye account zangu nawacha kama 150'000 hela nyingine huwa nazizungusha kwenye biashara! Au kwaushauri mzuri badilisha hizo hela kwenye mfumo wa dola halafu fungua USD$ Account kwakua uwezi toa dola kwenye ATM mpaka uingie kwa Cashier dirishani hii ni kwausalama zaidi.
 
Inawezekana huyo bank teller ndiye aliyecheza huo mchezo. Pia inawezekana ameshastuka kwa hiyo amerudisha pesa zako. Nakushauri nenda tena kwenye ATM uangalie kama zimerudishwa. Ikiwa bado onana na Manager, haki ya mtu haipotei, itacheleweshwa tu
 
Kama washauri wengi hapo juu walivyoandika...chukua usukani wa fedha zako... hata kama ni senti moja,, weka record lini umeweka ngapi na lini umetoa ngapi.. halafu ukipata statement ihakiki ili ujue transactions gani zina utata,...chukua hatua hapo ni kumwona meneja moja kwa moja..Je Teller huyo anakujua?? au mnafahamiana??? maana isijeikawa unampa achukue hakupi kumbukumbu halafu kumbe amefanya madudu behind your back...
Ushauri mwingine ni kutumia ATMs zaidi kuliko teller.... Tujulishe maendeleo yake..
 
Somo lingine wakuu, kama una hela nyingi usiwe unatoa kwa ATM. Wafanyakazi wa benki wameanzaisha kamtindo ka kuiba hela kutoka kwenye akaunti zilizonona za wateja wakijua kuwa mhusika huwezi gundua wizi huo hasa kama una mazoea ya kwenda kutoatoa hela kwa ATM. Wajanja wanaenda kaunta unatoa hela ya kutosha kwa matumizi ya wiki 2 au 4 na unahakikisha una-note somewhere amount na siku uliyotoa hela.

Wakigundua hutumii ATM kudroo hela huwa wanaogopa wanajua lazima utakuwa unatunza kumbukumbu tu!
Anyway sijui,lakini mimi huwa ninahifadhi mpunga mrefu tu CRDB account,but sijawahi punguziwa hata sh.100.Kuhusu utunzaji kumbu kumbu,mimi kila ninapodraw pesa ATM,lazima nihifadhi ile karatasi inayoonyesha salio mara ya mwisho nilipochukua pesa.
 
wezi wakubwa kwenye kampuni zinazotumia technolojia ya kompyuta kwa sana ni watu wa IT(hata mkinuna)vijana tuna tamaa sana ya utajiri wa haraka siku hizi
 
Unaweza ukailaumu bank wakati kosa ni la bank teller..mara nyingi hawa ma bank teller ndo wanaopiga deal zote...

kwa hiyo madam kwa mtazamo wako wewe hapo benki haihusiki kabisaaaaaaaa! Usitake kuniambia eti tusimlaumu Kimei kwa wizi wa EPA kwa kuwa walioiba sio Kimei.

Anyway kila mtu ana uhuru wa kuwaza tofauti na mwingine, ila hii yako kwa kweli ni kali ya kufungia mwezi february 2012
 
Nashangaa CRDB Bank ni Bank pekee inayotoa world class Call Center ambayo inafanya kazi saa ishirini na nne kushugulikia malalamiko ya wateja. Mimi nilikuwa nje ya nchi nilipata tatizo nilisaidiwa ndani ya masaa matatu. Mbona wewe hukusaidiwa.
 
CRDB Bmna bank ni Benk inayotusaidia kwa nanmna nyingi ina misingi ya uzawa kuinua maisha ya watanzania na uchumi wa tanzania kwa ujumla ni Benk iliyosikiliza mteja kwa hiyo siyo vizuri kunyeea kambi. Acha uzushi tujenge nchi yetu. tusivuruge miundombinu ya kujenga nchi yetu
 
This an isolated case. I deal with most of banks through my day to day activities you can not compare CRDB with any other banks except NMB and NBC in terms of accuracy
 
Nawashangaa sana watanzania wenzangu mnavyoiponda CRDB Bank wakati hii ni benki yetu watanzania, mnataka Tanzania iendelee wakati mnashabikia benki za kigeni badala ya kushabikia benki zetu za ndani. Huu sio uzalendo kabisa na ni ujinga mkubwa sana, watanzania amkeni acheni ushabiki usiokua na maana, hamjui kama hizi benki za kizungu ni kwa manufaa ya wazungu?mnafikiri wanakuja ku-invest huku kwa manufaa ya watanzania? TUACHE USHABIKI WA KIJINGA TUFANYE KAZI NA KUSHABIKIA VITU VYENYE MANUFAA KWA TAIFA LETU.
 
cha muhimu ukitoa hela kwa ATM usiache kuchukua risiti..ni kumbukumbu nzuri sana!
siku wakizingua unawaomba statement unalinganisha na risiti! utagundua tu wapi walikuchezea shere!
 
Miezi kama sita iliyopita nili deposit shiling milion moja kwenye account yangu ya hapo CRDB jana nikaenda pale kutaka kuchukua kiasi fulani cha fedha nikaomba bank statement yangu,nikapewa balance inaoonyesha nina shilingi elfu kumi na mbili tu.

Sikuamini nikamuuliza yule bwana mbona niliweka shilingi milion moja mwezi wa tisa na kwenye account nilikuwa na elfu ttemanini kabla sija deposit hiyo pesa? Jamaa akacheck akaniambia inaonekana hiyo pesa ilichukuliwa kwa njia ya ATM machine kataika awamu mbili tofauti.

Nikamwabia aliechukua ni nani sababu mi sijawai kuja chukua hiyo pesa, nikamwambia si kwenye ATM machine kuna camera yenye uwezo wa ku track matukio yote ya hapo check ili tuone aliechukua hiyo pesa jamaa akachek baada ya mda akaja na kuniambia aliechukua inaonekana alikuwa amejitanda kitu kichwani na picha haipo clear.

Nikamsisitiza anionyeshe hiyo picha kama ni mtu wa kwenye familia yangu nitmjua hata kwa umbo jamaa mara aingie ndani atoke bila majibu ya maana.Nikamwambia aniruhusu kama yeye ishu ameishindwa niende kwa meneja jamaa(bank teller) akaniambia nisubiri ila mpaka ikafika saa kumu na moja walikuwa hawajanipa jibu la nani kachukua pesa yangu.

Akawa ameniambia leo nirudi pale bank tuweze kucheck tena. Kwa bahati mbaya leo nilikuwa nasafari ya siku kama saba ndio nitarejea hivyo sikuweza kwenda pale.

Maswali mengi nilijiuliza sana je kuna mtu mwingine alishapatwa na shida kama hii? Na ni hatua gani ntaweza kuzichukua pindi nitakapo rudi kama hawatanipa majibu ya kutosha?

Kwanza nikupe pole mkuu, Jamani, ninavyofahamu mimi, Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele kuwahudumia wateja wake na wanauwezo mkubwa kuhandle suala kama lako kulikoni kuchafuliwa image yao.

Hakuna asiyetambua umahili wao katika kutatua kero za wateja, Hivi sasa ni kitu cha kawaida gadgets kumisbehave kwa muda iwe ni kwenye mabenki, makampuni ya simu n.k.then wanaweza kufanya reconcilliation kisha pesa ikarudishwa japo kwa kuchukua muda kidogo. Kwa maana hiyo, hakuna sababu ya kupanick, nijuavyo mimi suala lolote likishindikana kwa afisa wa ngazi ya chini, basi meneja na hata Kimei wako accessible wakati wowote ingawa inaweza kuwa kwa bureaucracy kidogo.

Kwa maana hiyo, hakuna sababu ya kukosa imani na benki ya kizalendo ambayo ni tegemeo la kusukuma gurudumu la uchumi nchini. Benki hii ndio inayoongoza kwa kuwakopesha wakulima na hivyo kuleta ajira nyingi kwa watanzania. Kitengo chao kipya cha Call Centre kilichopo pale Kijitonyama kimekuwa kikishughulikia kero kama hizo kwa umakini kabisa. Sisi tuliozoea kutoa fedha katika ATM mida ya jioni tukiona ATM zimefungwa au kadi kunaswa, tunawasiliana na Call Centre na kupata msaada wa haraka.

Nadhani wanachotakiwa kufanya CRDB ni kuwapa elimu zaidi wateja wake kuhusu kitengo chao cha kutatua kero za wateja wanachokiita Call Cantre ambacho mimi na wengine wengi tunakitumia
 
Jamani watanzania muige utamaduni wa kupongeza maendeleo yanaofanywa na watanzania wenzenu. Tabia ya kupenda kuona watu wa nje ndo wanaweza haina msingi n Kama Tija katika maendeleo ya Taifa letu. CRDB Bank benki ya kizalendo inatuhudumia kwa ubora wa hali ya juu na umakini leo mtu anatoka huko na uzushi na uongo amboa hauna tija kwa maendeleo yetu. Kama unatazi banki iko wazi nenda beleka malalamiko yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hiyo michezo kwenye mabank yetu nilishaishtukia siku nyingi mno! Siku hizi mimi kwenye account zangu nawacha kama 150'000 hela nyingine huwa nazizungusha kwenye biashara! Au kwaushauri mzuri badilisha hizo hela kwenye mfumo wa dola halafu fungua USD$ Account kwakua uwezi toa dola kwenye ATM mpaka uingie kwa Cashier dirishani hii ni kwausalama zaidi.

Savings TShs. 150,000????????unasomesha?????Ukiugua ghafla???????????Mke akijifungua unafanyaje????ukipata msiba utaugharamiaji?????.

You should at least have equivalent of six months intact in your bank account

 
Hoja yako haina mashiko.Inatoa picha ya jinsi ulivyo mpumbavu. Mimi nimteja wa benki ya CRDB kwa muda mrefu sasa. Na mara zote ninapokuwa nimetatizwa na issue ya kihuduma, ninapata ushiriakiano mzuri, maelekezo na ushauri kutoka kwa timu mahiri ya CRDB Bank. Siyo VIZURI, kuibuka na kubwabwajaaaaaaaaa kama kasuku, kwa ishu ambayo inaweza kusovika kiungwana kabisa. Usituambukizi uchuro wako sisi wateja wa benki yetu CRDB. Kamata hiko kipande, utulie
 
Pole sana jamani, maisha yenyewe ni balaa tupu, mtu unajitafutia ili angalau kesho usilale na njaa kumbe wengine wanasema afadhali umeleta, watashughulikiwa na Mungu ipo siku za mwizi arobaini.

Risiti ya kuweka hela ndiyo itakusaidia, lakini hiyo issue wewe nenda moja kwa moja kwa manager, wala usihangaike na hao mateller wengi ni wezi sana, wanatuvuna tuu yaani imeniuma saana na Mungu atakusaidia haki yako lazima utaipata na lazima mtu awajibishwe hapo.

Utupe taarifa yatakayojiri huko
 
Watanzania tufanye kazi tusongembele tuache uzushi usio na tija na kupoteza muda. Tujadili tufanye nini kuinua sekta ya kibenki nchini badalala ya kuharibu mambo mazuri yanayofanywa na Beki ya CRDB. Hatuwezi kujiuliza mashirika mangapi yalibinafisishwa. mangapi yanafanya vizuri naipongeza sana Benki ya CRDB kwa kufanya Vizuri Wasonge mbele. Popote kwenye mafanikio wambea wengi
 
Back
Top Bottom