CRDB BANK si Bank ya kuiamini kabisa!

ebana na mimi nimepata tatizo hlo! mara ya mwisho account yangu ilikua na takriban laki 7,nimesafiri nimekuja mkoani nimetoa hela leo nashangaa kukuta laki 1 na elf 40. na mpaka kurudi dar es salaam ni mwezi wa 4! hv bank statement naweza kuomba popote? je inaonesha records za kila transcations
 
kwa hiyo madam kwa mtazamo wako wewe hapo benki haihusiki kabisaaaaaaaa! Usitake kuniambia eti tusimlaumu Kimei kwa wizi wa EPA kwa kuwa walioiba sio Kimei.

Anyway kila mtu ana uhuru wa kuwaza tofauti na mwingine, ila hii yako kwa kweli ni kali ya kufungia mwezi february 2012

Mi nimetoa tu mawazo yangu kutokana na upeo wangu ili kumpa wepesi ndugu yetu Manuu...na wala hakuna sehemu niliyosema kimei alaumiwe au asilaumiwe kuhusu hayo ya EPA.
Naomba unielewe,bank teller ni sehemu ya bank ila kama maelezo yake hayajitoshelezi then ni vema akaonana na meneja wa huduma kwa wateja..hapo kuna uwezekano wa kupata ufumbuzi.Inawezekana bank teller ndo mwenye mchezo mchafu..# nisamehe kwa maelezo yangu yaliyo kukera!
 
Ndo bank pekee niliyokuwa na imani nayo kama mambo yenyewe ndo haya basi tena.
 
hapa kuna side 2, bank na mteja.
Mteja- inawezekana pincode yako unashare na mtu, au inawezekana kuna mtu wako wa karibu sn anaijua pasi na ww kufaham na anaiba kadi na kutoa hela.
Uzuri wa hizi system za bank inaonesha each and ev.thing kinachofanyika kwenye acc ya mteja. Km hela imetoka kwenye ATM itakuonesha mpk ATM gani imetumika, tarehe, muda na mpk card no. Na ivo ndo vitu vya mwanzo kuangaliwa wkt mteja unapolalamika kuh upungufu wa hela yako. Na nnavojua mimi hayo hufanyika cust.service na ikishindikana unamuona accountant au operations manager na sio bank teller.
Manuu, wizi wa kuibiana wateja wenyewe kwa wenyewe upo zaidi kuliko banker kumuibia mteja.
Bank- inawezekana banker akafanya fraud, kwa system hii ya kisasa itaonekana tu hela imetokaje na user gani amefanya transaction kwenye hio acc yako. Cha msingi when u go back to the bank komalia mpk ihakikishe unapata ufumbuzi wa hela yako iwe km ni banker ndo aloiba au mtu wako mwenyewe. Yani closer person wko.
 
kwanini hukuomba kuonana na meneja siku hiyo? i mean head wa section yoyote tu ingesaidia wawe wanajua maana ezi wengi huwa ni wa chini chini.

I hope utafanikiwa, ila kama mimi wewe ningeripoti na polisi.
 
Jiunge na sim banking hela yeyote inayoingia au kutoka unapokea message na wanakuambia kama hutambui muamala uliofanyika upige simu kutoa taarifa immediately jombaa
 
exim weziiiiiii pambav

Nilpata kuingiza Exim Milioni 15.. Baada ya wiki nikawa nachukua not less,na not more than laki tatu... Nilifanya hivyo mara 6 ama 7 katika kipindi cha mwezi mmoja..

Cha ajabu nilikuja kugundua kwenye ACC yangu kuna pungufu ya laki tatu baada ya kupiga hesabu zangu..! Kwa kuwa nilikuwa napenda kutumia head office yao nikawafuata,wakanipa form nikajaza,kwenye masaa 24 wakawa wamerudisha amount yangu!

Benki bana.. Acha tu!

Na mateller wanatupenda sisi waswahili zaidi kwani si wafuatiliaji sana wa transaction za akaunti zetu ukilinganisha na watanzania wenye asili ya kiasia!
 
Amia kwetu NMB mkuu. Ila nao wezi vilevile wameshawahi kunikata 10,000 kwenye atm zao.
 
Jamani ebu tuambieni kama kuna wengine wenye tatizo kama hilo NBC.

Halafu nisaidieni hili swali,nipo nje ya nchi na huwa natuma hela kwenye account yangu ya Tz na sichukui hela,je usalama hapo unakwaje?
 
Manuu eeeh pole sana kwa yaliokupata lakini?-Ningependa kufahamu haya
Unajua Milioni moja pesa na nyingi sana hapo nyumbani hata kama ziko zaidi na hizo.Linapokuja swala la upungufu kwa kweli linaleta utata kama ulivyo lifikisha hapa na likajadiliwa na wadau,

Ni hivi ulipoona hakuna majibu ya kuridhisha toka kwa muhudumu kwa nini usinge muona meneje mda huo huo ukapata ukweli?
Unajua siku inayofuata unasafiri uone kuwa umetoa mwanya kwa muhusika kuliweka sawa tatizo kama (bank)wanahusika?

(Ushauri kumbuka jina na mda wa muhudumu uliemwambia tatizo lako kwa mala ya kwanza unapokwenda kwa meneja uwe na kuanzia kwa ngazi ya mwisho pia usisahau labda kuna mtu wako wa karibu alicheza hii inshu)

Mimi ni mteja wa CRDB mda mrefu sana sikatai hakuna tatizo.Yapo na wanayashughulikia vzr tuu.
POLE SANA
 
Jamani ebu tuambieni kama kuna wengine wenye tatizo kama hilo NBC.

Halafu nisaidieni hili swali,nipo nje ya nchi na huwa natuma hela kwenye account yangu ya Tz na sichukui hela,je usalama hapo unakwaje?
Hi Ex, mambo?
Matatizo yaweza kuwepo, kuna system misbehaviour, kuna wizi wa kuibiana wanandugu wenyewe kwa wenyewe na kuna fraud zinazofanywa na bankers.
Cha muhimu ni kuwa makini na kufuatilia mara kwa mara, mambo ya hela c ya kupuuza tuu.
Kuh transfer nje ya nchi haina shida hela yako inaingia ukituma, ila pia inabidi kufuatilia.
Na km una acc NBC fungua internet banking itakkuwezesha kuangalia transaction zako thru internet, na km una prob yyt u better call help line no zipo kwenye bankteller yako
 
Nawashangaa sana watanzania wenzangu mnavyoiponda CRDB Bank wakati hii ni benki yetu watanzania, mnataka Tanzania iendelee wakati mnashabikia benki za kigeni badala ya kushabikia benki zetu za ndani. Huu sio uzalendo kabisa na ni ujinga mkubwa sana, watanzania amkeni acheni ushabiki usiokua na maana, hamjui kama hizi benki za kizungu ni kwa manufaa ya wazungu?mnafikiri wanakuja ku-invest huku kwa manufaa ya watanzania? TUACHE USHABIKI WA KIJINGA TUFANYE KAZI NA KUSHABIKIA VITU VYENYE MANUFAA KWA TAIFA LETU.

nahisi we utakuwa na matatizo ya akili,kisa CRDB ni bank ya wazawa hata kama wanatuibia vijisenti vyetu,tuwapambe tu eti,kwenye ukweli lazima tutaongea ili wabadilike!!au we ndo huyo teller msanii?
 
Pole sana, ila ukirudi ufatilie mpaka kwa meneja upate uhakika wa pesa zako kachukuwa nani? Kuna mambo mawili. Kama Kadi yako haikutumika kutolea hizo pesa kwenye ATM au kwa Teller, utakuwa umepona, kwa kuwa Bank itawajibika kukurudishia pesa zote zilizoibwa. Lakini ikithibitika kuwa kadi yako ndio iliyotumika kuchotea huo mshiko basi ujue imekula kwako.

Kadi na password ni vitu vya kutunzwa sana, usiviache hovyo au kumpa mtu.
 
Hi Ex, mambo?
Matatizo yaweza kuwepo, kuna system misbehaviour, kuna wizi wa kuibiana wanandugu wenyewe kwa wenyewe na kuna fraud zinazofanywa na bankers.
Cha muhimu ni kuwa makini na kufuatilia mara kwa mara, mambo ya hela c ya kupuuza tuu.
Kuh transfer nje ya nchi haina shida hela yako inaingia ukituma, ila pia inabidi kufuatilia.
Na km una acc NBC fungua internet banking itakkuwezesha kuangalia transaction zako thru internet, na km una prob yyt u better call help line no zipo kwenye bankteller yako
Mi niko poa Angel,sijui wewe.
Thanks much sikuwa nafahamu hilo,isiwe naweka tu hela zangu bank baadaye narudi naambiwa sina hela.
 
Ina maana huyo Bank Teller siyo mfanyakazi wa CRDB? kiasi cha kumtenganisha na bank kama ulivyosema? Mi naona kama bank teller ni wa CRDB basi CRDB inahusika kwani ndiyo mwajiri wake na huwe separate hivi vitu. kama ni kuwajibika ni CRDB kama bank na siyo teller.
mkuu hata mimi nilimshangaa uyu mdau kutenganisha bank teller na bank. okh ngoja niwe upande wake, niambie ingekuwa
ni bank ndo inaiba basi ingekuwa inaibaje?
 
Hoja yako haina mashiko.Inatoa picha ya jinsi ulivyo mpumbavu. Mimi nimteja wa benki ya CRDB kwa muda mrefu sasa. Na mara zote ninapokuwa nimetatizwa na issue ya kihuduma, ninapata ushiriakiano mzuri, maelekezo na ushauri kutoka kwa timu mahiri ya CRDB Bank. Siyo VIZURI, kuibuka na kubwabwajaaaaaaaaa kama kasuku, kwa ishu ambayo inaweza kusovika kiungwana kabisa. Usituambukizi uchuro wako sisi wateja wa benki yetu CRDB. Kamata hiko kipande, utulie

we mteja au mfanyakazi!!
 
Nafikiri ungepima ubora wa bank kwa jinsi walivyolishighulikia tatizo lako mpaka mwisho. Usilaumu katikati. Matatizo yapo kila mahali, ila jinsi ya kuyatatua ndio kunaipa au kuinyima kredeti taasisi husika.
Navyojua mimi crdb wana afadhali kuliko banks nyingi tu. Kama unabisha kaweke hela zako barclays
 
nafahamu CRDB kuna baadhi ya staff VIBAKA wana mtindo wa kucheza na akaunti za watu. Hasa hubamiza akaunti ambazo hazina frequent transactions. Kusingizia hela imechukuliwa ATM ni janja yao tu, ukiwa mkali hela inarudi fasta.
 
Back
Top Bottom