nyandaojiloleli
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 205
- 18
sioni shida kwa watu wa bank kwenda kanisani kumshukuru Mungu. Pale hawajafanya biashara yoyote wameenda kumshukuru Mungu. Mbona NBC ishakuwa bank ya kiislam.
Islamic bank ni matokeo ya udini wa JK. Zitafutwa 2015 haraka.
GT ndo nani?GT amehamishia uislam wake kwenye benki anayoingoza ya NBC, huko wameanzisha kitengo cha ISLAMIC BANKING!!
Jumapili ya tarehe 18 Desemba, 2011nilibahatika kusali misa ya kwanza katika Kanisa Katoliki la Mt. Patrice, Morogoro. Niliona maajabu ua kituko hali iliyonilazimu kuandika katika Jamii Forum ili niweze kuwashirikisha na kupata ushauri ma maoni ya wadau. Issue yenyewe ni kwamba benki ya CRDB Mkoani Morogoro waliomba misa ya shukrani kwa ajili ya wateja wao! Ulikuwa ni mjumuiko wa matawi yote yaliyoko Morogoro. Misa iliongozwa na Askofu Mkude.
Katika mahubiri, Askofu Mkude alionyesha kushangazwa kwake na benki kuomba misa! Inakuwaje benki waombe misa. Pia aliwashukuru kwa kumtanguliza Mungu katika shughuli zao za kibenki na kuwaasa wafanye kazi kazi zao kwa uadilifu. Na hatimae CRDB bank wakatoa vipaji wakiwa ndani ya T-Shirts zao za CRDB Family Day.
Wakati wa kutoa Vote of Thanks, mwakilishi wa benki alieleza kuwa wameomba misa kumshukuru Mungu kwa kuwa benki bora kwa mwaka huu na kwashukuru wateja wao kwa kuwasupport. Na kwamba walikuja kanisani kwa "umoja wao" bila kujali itikadi ya dini zao!
Wasiwasi wangu: Kwa mwenendo huu tutatarajie nini kwenye nyumba zetu za ibada? Je, Yesu hakupindua pindua meza za watu waliokuwa wakifanya biashara katika sinagogi? Ninavyoona (kwa mtazamo wangu) si ajabu siku zijazo tutakuwa tukisikia kuwa Misa ya Kwanza imedhaminiwa na ya Tigo, Misa ya pili NMB na misa ya watoto NBC Ltd!
Waumini tunayapeleka wapi makanisa haya? Je, CRDB watadhubutu kwenda msikitini pia kuwashukuru Waislamu kwa kuwa wateja wao kwa "umoja" wao bila kujali itikadi zao kama walivyofanya Morogoro katika kanisa Katoliki?
Nawasilisha.
Islamic bank ni matokeo ya udini wa JK. Zitafutwa 2015 haraka.
Hakuna tatizo katika hilo, tena linaimarisha zaidi Umoja wa Watanzania bila kuhangaika na imani zao! Kwa miaka yote Kanisa Katoliki limekuwa likifanya maombi maalum kwa viongozi wa Nchi yetu bila kujali dini zao, wamekuwa wakiombea wagonjwa kwa ujumla wao...kuna ajabu gani kumshukuru Mungu kwa mafanikio ya Asasi ambayo inahudumia binadamu bila kuwabagua kwa imani zao?
Waliamini kwamba Kristo ndio kweli,ndio mwanga,ndio mafanikio na kila kitu!