CPA: Review classes

Musasira ni kiboko ila kama amegawa kazi inabidi ufikirie mara mbili mbili kabla ya kujiunga nao. Kila la heri Husninyo.
 
Last edited by a moderator:
Wako Organized kweli, lakin unaweza pia ukajaribu kwa Rashid Ilala Primary School.

Ubaya wa APT Mzee Musasira amegawa sana kazi kwa walimu wengine hivyo ufanisi umepungua.

ahsante Shark. vipi edson wa mnazi mmoja nae yupo vizuri?
 
Last edited by a moderator:
Musasira ni kiboko ila kama amegawa kazi inabidi ufikirie mara mbili mbili kabla ya kujiunga nao. Kila la heri Husninyo.

ila kama amegawa kazi si ndio ufanisi ungekuwa mzuri kuliko yeye kufundisha masomo yote!! au inawezekana aliowapa hawapo vizuri. ahsante BAK
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo maana yake Mkuu Husninyo. Uwezo wa mtu na mtu katika masuala mbali mbali ikiwemo kufundisha unatofautiana sana, mwingine akikufundisha somo ambalo linadaiwa gumu sana unaweza kuliona ni rahisi kama kunywa maji na mwingine somo lile lile ukaliona gumu kupita kiasi, lakini ukijipinda mgongo (kwa masaa chungu nzima kwa siku ikiwemo weekends) unaweza kabisa kufanikiwa.

ila kama amegawa kazi si ndio ufanisi ungekuwa mzuri kuliko yeye kufundisha masomo yote!! au inawezekana aliowapa hawapo vizuri. ahsante BAK
 
Last edited by a moderator:
Wako Organized kweli, lakin unaweza pia ukajaribu kwa Rashid Ilala Primary School.

Ubaya wa APT Mzee Musasira amegawa sana kazi kwa walimu wengine hivyo ufanisi umepungua.

Hakika Mzee Musasira kagawa kazi kwa wengine lakini ujue kwamba somo moja kama, International Finance, linafundishwa na walimu karibia watano, hii itaondoa mwalimu asiye na uzoefu kufundisha hilo somo lote, kumbe kwa wazo la huyu mbunifu, creative and innovative, Musasira linaondoa hiyo kitu, plz nenda APT centre, kwa masomo yote matatu ya module moja wawezafundishwa na walimu karibia 15 na ni wazoefu wanaofundisha vyuo mbalimbali iwe arusha au hapa dar wanapiga part times zao hapo pia utashangaa maana mwalimu wa APT anafundisha ktk centre nyinginezo, nakusihi nenda APT!
 
mh isuto hao walimu unawafahamu? nway, ahsante kwa taarifa. kuna mdau aliniambia hapo anaweza mwalimu akafundisha topic hata haijaisha anakuja mwalim mwingine anaanza topic mpya ya somo hilo hilo. sijui ya kweli hayo!!! ngoja tuone itavokuwa.
 
Kuna mhadhiri wa ifm anaitwa dr.Nkoba ni mzuri sana kwenye international finance wakati nipo dar alikuwa anafundishia biafra,hakuna kama yeye kwenye hilo somo.Kuhusu somo kama Financial Reporting ulizia Issa Siasa anafundishia wapi,ukimpata na huyo CPA tayari unayo mkononi.APT(Kwa Musasira) miyeyusho mingi.Kingine nunua vitabu vya ACCA huwa wanatoa text book na exam kit kwa kila somo vitakusaidia mno,unaweza kuvipata NBAA Bookshop au Osman Tower(mkabala na Elia Complex) mtaa wa zanaki kwenye review centre inayoitwa ftc(Financial Training Centre).
 
ahsante Shark. vipi edson wa mnazi mmoja nae yupo vizuri?

Yeah, watu wanamsifia nae.
Wajua nikupe siri, hawa walimu ndio pia watungaji wa mitihani so wapo ambao wakipigisha pepa zao ile mwishoni mwishoni, basi maswali mawili matatu hukosi, Rashid ni mmoja wao!!

Edson sina uzoefu nae sana, buta kuna jamaa zangu kadhaa wamedunda pale kwenye haya matokeo ya juzi, you can try there as well!!
 
Mimi nakushauri uende kwa Edson,yupo fresh kwenye international na fiancial report.tax nenda kwa rashid boma ilala.

Kama mkuu alivyosema,module e kasome kwa rashid na nkoba pale ilala boma cuz jamaa wapo vizuri halafu module f kapige kwa edson pale mnazi mmoja,personally nimefanya hivyo and now am a cpa holder....musasira wa apt is gud but amelost touch kwani amedelegate masomo kwa watu ambao wengine c wazuri sana kwenye teaching...all da best
 
acheni tabia na kasumba zenu za kizamani! mnanikumbusha enzi za tuition secondary school
CPA inahitaji intensive preparation sio umefundishwa na nani au upo centre gani?
sasa we leta ulimbukeni wako kwenye taaluma mara kwa musasira,nkoba,zawadi,kakozi,edson utashangaa unazeeka tu ukiwa unatafuta CPA.alafu kuna ndugu wengine naona kama wanafuata mkumbo tu,eti kwa sababu fulani kawa certified au charted maisha yakawa mazuri nae anajaribu kusafiria nyota ya mwenzie!
ndio maana leo utakuta mtu ana CPA anashindwa kufanya bank reconciliation,budgeting ,sasa preparation ya fs ataweza kweli?
 
nenda kwa Edson
Nenda kwa Rashid.
Nenda kwa Musasila,
Nenda Inspire.
Nenda kwa Paul.
Nenda Beta consultants,
Mwisho wa siku sehemu kubwa ya kufaulu itatengenezwa na wewe mwenyewe kwa sababu vituo vyote hivyo vinatoa watu wanaofaulu na wanaofeli pia ila cha muhimu ni kufanya discussion hasa na watu wanaotoka centers tofauti ili ku-share elimu toka vituo tofauti.....
 
Naomba kujuzwa kama kuna kituo chochote maeneo ya kati ya Kibaha na Ubungo, anything hapo katikati kwa ajiri ya unafuu wa logistic
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom