Course ya Uchawa kwa ngazi zote

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Tayari tunaanza kutoa course ya Uchawa ngazi ya Certificate, Diploma na Degree. Bado mchakato wa kuto Masters unaendelea.

Kutokana na kuwepo fursa mbalimbali katika Dunia yetu hasa nchini TZ na kuangalia namna ya kusaidia wananchi tayari course hii imeanza kutolewa kwa aliye tayari tuwasiliane.

Ni mafunzo ambayo yanakusaidia uweze kuishi kwa maneno tu ukimpigania mtu ambaye una uhakika anaweza badilisha maisha yako kiuchumi. Ukiwa tayari tuwasiliane usijali kwa sasa una Elimu gani. Hiyo haitahesabika unapokuja jiunga kwenye hii course.

Usiache wenzako wale maisha nawe ukabaki kusononeka tu kuwa wanaishi kiuchawa. Chukua hatua. Faida ni nyingi. Kuna kupata vyeo, kupanda vyeo, kupata teuzi, kufadhiliwa, kupata upendeleo, umaarufu n.k

Wenzako wanasonga mbele wewe utabaki hapo ulipo.
 
Back
Top Bottom