Counter attack......Yasikukute

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,156
Jamaa kampenda binti....Bila shaka kwenye macho ya wengi ilionekana wanapendana. Siku zikaenda na miezi kadhaa.

Sijui nini kilimpata binti, akaanza kupungunza mapenzi kwa Boyfriend wake. Boyfriend akawa anamlaumu kulikoni umekuwa hivyo siku hizi, binti akatia pamba.

Uhakika kama binti anamsaliti hana. Hatimaye binti akasema "yatosha" sitaki haya mahusiano tena kwa lugha ya kukera. Jamaa akalalamika lakini akakubali shingo upande hasira moyoni. Baada ya mwezi akamfuata mpenzi wake akiwa mpole na lake moyoni....Kweli baada ya kuzungushwa kama wiki 3 binti akakubali kurudiana naye.

Mapenzi yakaanza kunoga..Jamaa alipoona binti sasa kafika na ka-relax akamfanyia kitimbi fulani siku moja..binti akamsihi abadilike na kulalamika................Jamaa akamwasha kibao na kumwambia "Kuanzia leo mimi na wewe mwisho ondoka'.

Binti mpaka sasa mawazo tele na machozi kibao, lakini jamaa ana furaha kupita kiasi.........Kumbe kumbembeleza kote ilikuwa ni njama ya kulipa kisasi.

My take: Huu mchezo alioufanya jamaa si mzuri.
 
platozoom kisasi kibaya
ila kwa alilolifanya binti kwa jamaa nalo ni baya
Ungempa mwenzio sababu z akusitisha uhusiano na sio bila sababu unakatisha mahusiano ghafla bila maelezo
Ila jamaa nae duh
 
Last edited by a moderator:
Safi sana .....kwani alivyokuwa amefanya binti kwa jamaa ndio ilikuwa vizuri?.....kwanza huyo binti hana msimamo ndio mana yamemkuta ya kumkuta ataachanaje afu arudiane?......wacha alie na kusaga meno manake amayataka mwenyewe!
 
Mtenda akitendewa hujihisi kaonewa.....wacha apate maumivu kama aliyoyapata mwenzie wakati kamuacha bila sababu!
 
sweetlady nakubaliana na wewe
Wacha alie kwanza na ajue machungu ya kuachwa bila sababu
yeye alitikisa kiberiti sasa yeye mwenzake kakitikisa na kakitumia ipasavyo wacha kimwakie
 
Last edited by a moderator:
platozoom kisasi kibaya ila kwa alilolifanya binti kwa jamaa nalo ni baya Ungempa mwenzio sababu z akusitisha uhusiano na sio bila sababu unakatisha mahusiano ghafla bila maelezo Ila jamaa nae duh

Mr Rocky Nilipoona wameachana mwanzo nikajua ni mambo ya kawaida wanapendana na watarudiana. Na kweli wakarudiana lakini baadaye jamaa alipomuacha ndio nikajua ni kisasi. Nifanye nini tena
 
Last edited by a moderator:
Jamaa alikuwa kwenye nafasi nzuri kuacha maumbile yalipize kisasi, lakini kitendo cha yeye kulipiza kisasi, ni sawa na kutega mwimba ambao matokeo yake utamchoma mwenyewe.................
 
Safi sana .....kwani alivyokuwa amefanya binti kwa jamaa ndio ilikuwa vizuri?.....kwanza huyo binti hana msimamo ndio mana yamemkuta ya kumkuta ataachanaje afu arudiane?......wacha alie na kusaga meno manake amayataka mwenyewe!

Nitaanza kukuogopa@sweetlady ..kwani tunakosea wangapi? wakilipiza je?
 
Jamaa alikuwa kwenye nafasi nzuri kuacha maumbile yalipize kisasi, lakini kitendo cha yeye kulipiza kisasi, ni sawa na kutega mwimba ambao matokeo yake utamchoma mwenyewe.................
Mtambuzi nimezaliwa mrima Kiswahili na kunga zake lzinanipa tabu..ufafanuzi tafadhali
 
Last edited by a moderator:
sweetlady nakubaliana na wewe
Wacha alie kwanza na ajue machungu ya kuachwa bila sababu
yeye alitikisa kiberiti sasa yeye mwenzake kakitikisa na kakitumia ipasavyo wacha kimwakie

Na inaonyesha kinamuwakia haswa lol.....mie nimependa sana maamuzi ya huyo mkaka! Na inaonyesha wala mdada hakuwa na sababu maalumu ya kumwacha mkaka ndio mana hata aliweza kumrudia..... platozoom mwache mkaka ajipe raha kwa raha zake amelipa kisasi alaah!
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky Nilipoona wameachana mwanzo nikajua ni mambo ya kawaida wanapendana na watarudiana. Na kweli wakarudiana lakini baadaye jamaa alipomuacha ndio nikajua ni kisasi. Nifanye nini tena
platozoom hapo kwa sasa ni pagumu maana huyu jamaa nia yake ya kumbembeleza arudiane naye ilikuwa sio kwa mapenzi tena ila kwa ajili ya kulipiza kisasi

Na ameshalipiza kisasi chake kurudiana tena hapo kwa kweli ni pagumu
 
Last edited by a moderator:
Na inaonyesha kinamuwakia haswa lol.....mie nimependa sana maamuzi ya huyo mkaka! Na inaonyesha wala mdada hakuwa na sababu maalumu ya kumwacha mkaka ndio mana hata aliweza kumrudia..... platozoom mwache mkaka ajipe raha kwa raha zake amelipa kisasi alaah!
sweetlady kabisa inaonekana dada hakuwa na sababu yoyote ya kumwacha jamaa
Alienda huko akamiss jamaa akaamua kurudi japo alibembelezwa
 
Last edited by a moderator:
platozoom hapo kwa sasa ni pagumu maana huyu jamaa nia yake ya kumbembeleza arudiane naye ilikuwa sio kwa mapenzi tena ila kwa ajili ya kulipiza kisasi

Na ameshalipiza kisasi chake kurudiana tena hapo kwa kweli ni pagumu

Sifikiri kurudiana naye itakuwa rahisi...Kimsingi kitendo cha binti kumwacha mara ya kwanza kilimuuma sana na alipandwa na hasira kila uchwao. Na kama si kufanya hili angefanya jingine.

Ila nakubaliana na wewe si kitendo cha kiungwana
 
sweetlady kabisa inaonekana dada hakuwa na sababu yoyote ya kumwacha jamaa
Alienda huko akamiss jamaa akaamua kurudi japo alibembelezwa

Ni kweli Mr Rocky .....aliona raha kumfanya mwenzie aishi kwenye maumivu kwa kipindi chote alichomwacha....sasa na yeye aende akambembeleze jamaa ili aupate utamu wake!.....afu ningemjua huyo jamaa ningemshauri asimsamehe kwa haraka lol.... platozoom nipe namba za mkaka tafadhali teh teh!
 
Last edited by a moderator:
Jamaa alikuwa kwenye nafasi nzuri kuacha maumbile yalipize kisasi, lakini kitendo cha yeye kulipiza kisasi, ni sawa na kutega mwimba ambao matokeo yake utamchoma mwenyewe.................
Mtambuzi kwa nini usione kuwa maumbile yamelipa kisasi kwa binti pia?.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye red nimekununia mpaka unambie utaanza kuniogopa kwa lipi?........ platozoom kwanini huyo binti alimwacha mkaka wa watu?

Binti alishiba mapenzi.Alipendwa sana na kwa sababu alijua hivyo ukichanganya na kiburi cha kila akipita mahali anatongozwa (sura nzuri pia)..nani atamuuliza..na hata akimuuliza atamfanya nini?

Kuhusu kukuogopa mbona liko wazi............Kwa hiyo nitonye akikukosea vibaya unalipiza kisasi?
 
Last edited by a moderator:

Binti mpaka sasa mawazo tele na machozi kibao, lakini jamaa ana furaha kupita kiasi.........Kumbe kumbembeleza kote ilikuwa ni njama ya kulipa kisasi.

Kumbe ulikuwa hujui

My take: Huu mchezo alioufanya jamaa si mzuri.[/QUOTE]
 
Binti alishiba mapenzi.Alipendwa sana na kwa sababu alijua hivyo ukichanganya na kiburi cha kila akipita mahali anatongozwa (sura nzuri pia)..nani atamuuliza..na hata akimuuliza atamfanya nini?

Kuhusu kukuogopa mbona liko wazi............Kwa hiyo nitonye akikukosea vibaya unalipiza kisasi?

Aisee mimi nna roho ya kulipa kisasi sana .....ukinifanya nkapata maumivu kwa namna yoyote ile lazima nihakikishe na wewe nakutia maumivu siku moja.......sasa huyo mdada si anasura nzuri?.....aende sokoni akaiuze sasa!
 
Back
Top Bottom