#COVID19 Corona Virus; New 9/11 (Kumekucha)Prt 1

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
566
511
TANBIHI: MADA HII SI KWA WATU WOTE. MAHUSUSI KWA WALE WENYE FIKRA PANA, WENYE UWEZO WA KUPOKEA MAWAZO KIZANI NA ELIMU NA IMANI YAO NA KUYACHANGANUA NA KUJENGA HOJA, DHANA SAWA AU TOFAUTI BILA KUKWAZIKA AU KUMKWAZA YOYOTE. KWA NAMNA YOYOTE IKIWA UNAFAHAMU UWEZO WAKO WA KUCHANGANUA NA KUTOFAUTISHA NA KUKWAZIKA NI MWEPESI NA MDOGO SANA, TAFADHALI ISHIA HAPA. VINGINEVYO MUANDISHI SI LENGO LAKE KUMKWAZA, KUMDHIHAKI, KUMDHARAU AU KUMDHALILISHA MTU YOYOTE AU TAASISI KWA NAMNA YOYOTE ILE, ILA KUTOA ELIMU.

“Those who are able to see beyond the shadows and lies of their culture will never be understood, let alone believed, by the masses.”

― Plato

Déjà vu- we had been on this road before, and not once, but many times.

Mara ya mwisho kupitishwa kwenye njia hii, kwa kasi hii ni 9/11.

images.jpg


Nakumbuka mara ya kwanza naiyona taarifa ya habari kuhusiana na 9/11, nilikuwa nimesimama karibu na luninga, nikaona majengo yale yanavyo poromoka, halafu nafasi yangu ikaniambia, hichi unacho kiona sicho, kuna zaidi ya hili nyuma ya taarifa hii. Sikuwa nimekubaliana na taarifa hii kutoka Day One, bila kuambiwa na yoyote. Miaka iliyo fuata nikawa mmoja wa vinara wanao kataa kwamba 9/11 haijafanywa na Bin laden, sikuwa peke yangu … na jina tunaloitwa ni conspiracy theorist ….’ Lakini mara zote, penye ukweli uwongo hujitenga na conspiracy theories zinageuka na kuwa conspiracy facts. Unaweza kuziona hapa baadhi ya kazi salim msangi hizo na wasomaji wa gazeti la mtanzania kwenye miaka ya 2006 mpaka 2012, najua wamekutana kazi hizi.

Janga la 9/11, au project ya 9/11 inaelekea mwishoni, viporo vichache vimebaki, kuna kiporo cha Syria na kiporo cha Iran, sababu zote hizi zilikuwa zishughulikiwe kwenye wimbi la 9/11. Wakati wa 9/11 wasemaji wetu wakubwa walikuwa ni CNN, VOA, ALJAZEERA, NK. Vyombo hivi hatuwezi kuviamini kwa asilimia kubwa. Zaidi kuhusiana na vyombo hivi vya habari na ajenda dhidi ya walimwengu pitia post hii ;

Leo ni vyombo vilevile tena, vipo mstari wa mbele kutuambia Dos na Don’t za Covid-19. Lakini bado upo huru, kwa nini kila unalo ambaiwa unalibeba kama lilivyo. Unaidhulumu akili yako, ... zakuambiwa changanya na zako.

Katika kipindi cha majanga ya namna hii, siku zote kunakuwa na taarifa za aina 3. Taarifa ya kwanza ni kutoka kwa mamlaka husika na wataalam wao, taarifa ya pili ni kutoka kwa viongozi wa kiserikali, kitaifa, kidini, kitaasisi, kimataifa n.k na taarifa za aina ya tatu ni kutoka kwa watafiti, wataalam na wachumbuzi huru. Kwenye mafuriko ya taarifa hizi kutoka kwenye sehemu zote tatu nilizo ainisha ni vyema kabisa msikilizaji ukautumia huu mesmo vyema … za kuambiwa changanya na zako.

Leo tena, watu wale wale, walio iburuza dunia nzima kupitia 9/11, wamerudi, na safari hii hakuna ndege kwenye majengo marefu, bali VIRUS / VIRUSI kwenye mwili wako, na jina linalo bamba ni COVID-19.

Sitazungumzia ni ipi asili ya Virusi hawa kama ni kutoka kwenye mazingira asilia au maabara, kwasababu hiyo siyo ishu. Tunakwenda ku-‘Pay attention to the man behind the curtain-‘, Tunajua kama ilivyo kuwa kwenye 9/11 kwamba kilicho kuwa kinatakiwa ni ‘kisingizio’ cha kufanya yale yaliyo fanyika kwa miongo miwili tangu 9/11 ilipo tokea, haikujalisha ni Osama amehusika au ni Bush na timu yake, kilicho jalisha ni kile ambacho ajenda ilihitaji, na kwa takribani miaka 20 tumeshuhudia ni nini ajenda ilihitaji …… wakati tunamalizia kutupilia mbali mafaili ya 9/11 na vikaragosi vyake (vikundi vya kigaidi), here we go again … na swali la kujiuliza ni ‘safari hii wanataka nini?’ Iwe ni maabara au natural haijalishi … nini wanataka ndiyo swali la msingi, stay put, sababu ndilo tunalo kwenda kulijadili.

Kulijibu swali hili, turudi nyuma kidogo … twende Hollywood, the place of magic and magicians of our times!

‘The Last man on Earth’
, hii ni filam ya mwaka 1964. Maudhui ya kwenye filamu hii ni ya mwaka 1968, kwamba matukio ya kwenye filamu hiyo yangetokea 1968. Mungu siyo Athuman, mwaka 1968, dunia ilipigwa na janga la mafua lililokuja kufahamika kama Hong Kong flu pandemic of 1968. Ugonjwa huo uliondoka na watu takribani milioni moja mpaka nne duniani kote.

index.jpg


Filam nyingine ni ‘The Omega Man’, hii ni ya mwaka 1971, maudhui yake ni kwenye mwaka 1977. Kwa mara nyingine Hollywood wakaiubuka vinara, mwaka huo 1977 dunia ilikumbwa na baa la mafua ya nguruwe.

LEGEND.jpg


Mwaka 2007, blockbuster filam, ya kinara wa Hollywood, Will Smith, iliyokwenda kwa jina la ‘I AM Legend’ ilitikisa soko la filam na maudhui yake ambayo yalilenga matukio ya baina ya mwaka 2009 na 2012. Again, wana mazingaumbwe wa Hollywood waliibuka kidedea, sababu safari hii walipatia tena, 2009 dunia ilipigwana HIN1.

Mwaka 2011, Hollywood walikuja na kitu kinaitwa ‘Contagion’, binafsi nilisha itazama hii filam siku za nyuma, lakini sikuitilia maanani kiasi hicho. Mara nikamsikia Bill Gate kaitaja hii movie kwenye Ted Show ambayo yeye alikuwa mzungumzaji, nikashtuka kidogo, nikaenda kupekua mafaili na kuitazama upya kwa utulivu. Yes, nadhani hata wewe msomaji utakuwa umeshiyona filam hiyo, imekuwa maarufu ghafla, kama hujaiyona kaitafute, sababu imetisha kwa jinsi ilivyo weza ‘kulitabiri’ janga hili la Covid-19.

CONTA.jpg


Setting yake ni ya mwezi Nov – December, kuelekea kwenye sikukuu ya Krimasi, sawia kabisa na janga la Covid-19. Sababu na lenyewe ni December 2019 ndiyo liliibuka. Popo, na nguruwe kwa mujibu ya filam hii ya Contagion ndiyo chanzo cha baa hili. Sawa na WHO wanavyo tuambia kuwa asili ya Covid-19 ni Popo … Mahali janga hili lilipo zukia ni China, Hongkong, sawia na Covid-19 China.

Nisikuchoshe kama hujaitazama kaitazame, ‘wametabiri’ mpaka kufungwa kwa mashule, athari ya uchumi tunayo anza kuiyona, makaburi ya halaiki kama Italy na kwengineko yanavyo onekana sasa; njia za kujikinga kama Social distance, don’t touch you face, wash your hands nk.

Ni kama Covid-19 script iliandikwa kwenye hiyo movie, miaka 8 kabla, kutoka A to Z.

Swali

‘Is it coincidence?’,

‘Is by chance Hollywood get it right again by 95%?

‘Can You Win a Million Dollar Lottery a Million Times?

Nini kinaendelea?

Hallo I am talking to You!


Novemba 2019 serikali ya Marekani kupitia National Center for Medical Intelligence, walipatiwa taarifa za kishushu juu ya uwezekano wa kuwepo kwa milipuko wa Covid-19. Ukweli wa taarifa hii ulirushwa na vyombo vikubwa vya habari nchini humo kama CBS na CNN. Baadae Serikali ya Trump iliikana taarifa hiyo kupitia kitengo chake cha intelejensia, Director of National Inteligence.

Mwaka 2017 ripoti kutoka Pentagon, ilitabiri vilivyo uwezekano wa kutokea janga la homa ya mapafu na kusambaa dunia nzima. Ripoti hiyo ikasema janga hilo litaathiri jamiaa na uchumi wake kwa kipindi cha mpaka miaka miwili.

Vipi tupo sambamba?

Taasisi za afya za kimataifa ikiwemo WHO kitu cha kwanza walicho sema kuhusu tiba ya janga hili ni kuwa itakwenda karibu miezi 18 kupata tiba. Bill Gate Tajiri wa kutoa chanjo duniani anazungumza habari hiyo hiyo, na ripoti ya Pentagoni miaka mitatu kabla ya janga kutokea ilisha litabiri, na athari zake na hata muda litakao dumu, miaka miwili. Athari ya uchumi si suala la kuuliza, athari ya kijamii, na mambo ya ‘Social Distance’ hilo ni jibu pigia mstari, imebaki ishu ya miaka miwili, vipi unadhani Corana inaisha kesho? Fikiria tena!



Lakini ripoti ya Pentagon haijaishia kusema tu kwamba athari zitakuwa za kiuchumi pekee, lakini pia imetaja kuhusu ugaidi, muuzaji wa chanjo duniani, Bill Gate naye kataja uwezekano wa ugaidi kupitia janga hili. Zaidi kuhusu hizi nukta mbili tutakutana mbele huku, kuna mahali pake tutazitaja upate picha maridhawa. Ingawa haitakuwa maridhawa hivyo sababu ugaidi utakuwa sambamba na hilo.

Wakati unalizungusha hilo kwenye akili yako, njoo mpaka mwaka 2015, Bill Gates, ndani ya Tedx Show, akiwa na mada ya, ‘The next outbreak? We're not ready.’ Bill Gates alikuwa akiitahadharisha dunia na walimwengu kuwa, tishio tulilo nalo kama dunia, siyo Bomu la nyuklia, bali Kirusi. Bill akasema kama kuna kitu kitakacho weza kuuwa watu takribani milioni 10 kwenye miongo michache ijayo, basi kitu hicho kitakuwa ni kirusi/ Virusi hatari.



Tunaweza kusema Bill ni mtu anaye kesha akisoma hiki na kile ali ajue shida ya dunia iko wapi, na kwa kutumia pesa na ‘moyo’ wake wa kipekee aisaidie dunia, sababu yeye ni mtu special sana na anafanya kazi za kipekee sana kuzisaidia nchi masikini, hasa kwenye ‘chanjo’ na kwengineko.

Dr Michael Ryan, Executive Director, WHO, ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki kwenye ‘Event 201’ ambayo iliendeshwa na World Economic Forum na Bill and Melinda Gates Foundation, Zaidi kuhusu tukio hili tutakutana nalo mbele.

LAKINI…

Bill kwenye hii talk show, alitabiri vitu kama Hollywood wanavyo fanya kwenye filamu zao.

Kwanza Bill alizungumzia udhaifu wa maradhi mengine ya kuumbakiza kama Ebola, Zikha na mengineyo, kwamba maradhi hayo yakisha kupata mtu unakuwa mahututi kitandani huwezi kutembea hivyo huwezi kuwaathiri watu wengi na hiyo ndiyo ilikuwa salama yetu.

Lakini akatabiri kuwa, next time hatutapata bahati hiyo, akaendelea na utabiri wake kwa maana hii, Je itakuwaje ikiwa mtu utapata na maradhi ya kuambukizwa na bado ukawa huna dalili yoyote, unaweza kuendelea na shughuli zako kama kawaida, lakini wakati huo huo unaendelea kusambaza maambukizi kwa wengine? It sounds like Covid-19 to me …!

Bill akazidi kutujaza hofu, akatukumbusha baa la Spanish Fluu la mwaka 1958, ambalo lilikula uhai watakribani watu million 25 duniani kote. Bill akasema aina hili la baa likija linaweza kusambaa haraka sana kote duniani, na kuuwa watu milioni 30. Mpaka Contagion filam inamalizika watu milioni 26 wamekufa, lakini kwa maneno ya Bill mwenye alisema, ‘that's just pure Hollywood.’ Lakini namba ya Spanish Fluu, na Contagion na hii ya Bill hazija achana sana. Hii ni variable nyingine na kuongezea kwenye hesabu yako ya probability. Endelea kutatua hesabu hizo na mimi naendelea kuonganisha doti.

... To be continued Inshallah ....
 
Asante sana mkuu kwa mada murua japo innahitaji kutulia kuisoma kutokana na urefu.

Hii issue ya NWO iliwahi kuonekana kama fiction au imagination miongoni mwa watu na leo nafurahi ninapoona baadhi ya watu mkiipa nafasi kupitia elimu kama hii.

Bill anatumika na ameamua kupitia taasisi zake kuendana na hizi secret agenda, mtu unapaswa ujiulize kwa akili ya kula ugali na matembele, iweje huyu jamaa ananipa nyama nilie ugali huku hali yangu hairuhusu kula ugali nyama!!

Kupitia taasisi zake anaenda kupindua dunia kupitia magonjwa 'tunayoyaona hatari kwa dunia' ili afikie hadhima yao.

Iwe ni kupitia covid-19 au ugonjwa mwingine ila hii case ni kubwa na ndiyo maana ile mipango yao ya chanjo kwa binadamu kupitia cheap inaenda kutimia soon.

➡This is a trailer, real movie is in progress.
 
We endelea kujidanganya tu eti Bill Gates ana moyo wa kipekee na anaisaidia dunia, soma kitu inaitwa "Global 2000 Plan" kisha tafakari upya. Moyo wa kipekee my foot
 
Again Buddy - Let's pay our attention to the man behind the curtain

Ni Secret Society inayooperate katika nyanja zote maradufu kiuchumi, kisiasa, kijamii na nk. na kupenyeza mizizi yake huko.
That's why hata chaguzi nyingi za Nchi zetu hizi za Dunia ya Tatu matokeo tayari yapo kiganjani mwao. Huku kinachofanyika ni kiini macho tu ya kile walichokipanga.

Ni kweli Dunia inajizungusha kwenye muhimili wake or We can say "Planet Earth rotate on it's own Axis".
Lakini (Secret Society) Wameshika Usukani wa Dunia hii wanaiendesha Dunia kwa Speed wanayoitaka wao either 50km/h or 80km/h even Direction wanachagua twende kushoto au kulia, twende mbele au turudi nyuma.

I'm not good on typing but i just made only some addition in order for everyone Else to think in and outside the box.

Thanks for the nice thread and i will take another time to digest it.
Best of Luck.
 
Back
Top Bottom