Confessions of an Economic Hitman & Tanzania

Lakini unakubaliana nami kuwa Mkapa ndiye aliyeuza nchi kulingana na kitabu chenyewe!
Maanake nisha jua unakotaka kwenda baada ya kuona unakotoka..
 
Bandugu,

Ukiangalia kwa undani hawa jamaa ni very strategic.......kama alivyoonyesha Mkuu Susuviri.......tuangalie sana mfano wa huu mkutano ujao huko Arusha.

Nakubaliana na Mkandara............kwa nchi yetu hatuwezi kumuacha Mkapa na hata JK pia.......na brain ya Mkapa zilikuwa Mramba + Kigoda + Chenge + Yona + Mzindakaya.....na sasa akina Karamagi siwezi kuwaacha katika kundi hilo
 
Ogah,
Binafsi nilijua toka zamani kuwepo kwa hawa hit men kama nilivyozungumza hapo awali na kama unakumbuka niliwahi kuvutana sana na mwalimu wetu AugustineMushi ktk issue ya Mkapa na pia kijana mmoja Mwiula zama za Bsctimes ktk maswala ya hawa wawekeshaji lakini sikuaminika na hata mmoja wao kwa sababu sikuwa na ushahidi mkononi kama huu. Na laukama tusingeweza kupata ushahidi kama huu, jamaa asingejitokeza ingebakia watu kusema mambo kama haya ni uzushi mtupu...
Sasa tukirudi ktk swala la Arusha na kama mnaniamini ktk hili basi naomba muweke record ya maandishi yangu, kesho nitayatumia vilevile kwa sababu nafahamu kinachoajiri.
Mkutano wa Sullivan una madhara yake ni sawa na kumleta Mchina enzi za Ujamaa badala ya mkoloni bepari wakati lengo la Mchina pia ilikuwa kuweka koloni la Kiuchumi kwa kupitia siasa zake ingawaje wao walikuwa hawachukui faida kubwa kuliko nchi za Magharibi. Hapo somo lilikuwa unafuu na sio kwamba hatukutawaliwa kiuchumi na nchi hizi zenye siasa mbaya kiuchumi..
Hivyo hivyo Sullivan ni kundi ambalo linapingana na umilikaji wa rasilimali za nchi zetu kupitia serikali za mataifa makubwa hivyo wametafuta njia bora nazenye unafuu kuzisaidia nchi zetu. Pamoja na yote haya hakuna kitu cha Bure wala Maria teressa ktk maswala ya biashara. Kuna mategemeo mengi toka kwao kuwa nao watafaidika ktk biashara hii tofauti na kifungo tunachokipata sasa hivi ktk mali zetu..
Tatizo letu sisi Wabongo tunaogopa kila kitu tukifikiria tu kusaidiwa kama vile mila yetu inavyojieleza kwamba unapomsaidia mtu hakuna malipo yaani umepewa BURE!... in Western world unaelewa kabisa hakuna msaada wa bure hata hizo zinazoitwa Aids zina gharama zake. Huku mzee akimpa mtoto mkopo wa elimu atasema nilisaidia mwanangu kusoma wakati Bongo kama mtoto atatakiwa kurudisha mkopo huo basi huo hauhesabiki kama msaada. Ukimkaribisha mgeni nyumbani akinunua chakula basi hukumpa msaada, hizi ni mila zetu ambazo msaada siku zote una maana moja tu BURE.
Hii ndio maana hata mkutano wa Suilivan wanauwekea mashaka kwa sababu unajieleza wazi kuwa hapa ni biashara...Kwa Wabongo bora ingesemwa msaada kama wasemavyo IMF ama Bush kungekuwa na mapokezi tofauti.
Nadhani nimebishana vya kutosha na Yournameis Mine ktk hili na watu wengi hasa waishio Marekani wanapingana na Sullivan kutokana na media kubwa ambao zinasimamia maslahi ya big corporates ambazo hata siku moja huwezi kusikia wakizitaja kwa ujangili wake.
Na hawa ndio wenye nguvu ya kumpeleka hitman kupitia vitengo vya IMF ama mashirika makubwa ya kifedha ya Umoja wa kimataifa.
Juzi tu niliona ktk BBC wakisema Mchina ameingia ku colonize Africa baada ya kupata deal la madini huko Congo wakati hawahawa wazungu wana mashirika yasiyo na hesabu Africa wakifanya kazi hiyo hiyo lakini hujasikia wakisema wamekuja Ku colonize Africa...
Yes, tuwe macho na wawekeshaji toka nje lakini kama kutakuwepo na UWAZI ktk deal lolote na hasa mikutano kama hii ambayo inamkaribisha Mtanzania yeyote kushiriki sidhani kama tungekuwa na matatizo ya Richmond na kadhalika...
Tofauti kubwa ya mkutano huu wa Sullivan na hawa EHM ni kwamba wao hu target nchi yenye kitu fulani wanachokitaka na kumfuata rais moja kwa moja kwa hadi nyingi huku wakiweka sheria za umilikaji kile walichokifuata ama sivyo basi deni lenyewe haliwezi kulipika. Zamani ilikuwa miundo mbinu ya nchi kama vile umeme, maji, mawasiliano na kadhalika siku hizi wameingia hadi ktk madini, oil,gas na vitu vingine muhimu sana ktk uchumi wa nchi zao. Kumbuka sokom bado lipo Ulaya hapa ni sehemu ya shamba wanapokuja lima na kuvuna.
Kifupi mtego wao ni kama mtu aliyeingia Morgage ya nyumba akiambiwa downpayment ni zero na pengine interest rate ni asilimia 5, kumbe ukijikanyaga tu na kuweka sahihi, mkuu umekwisha baada ya mwaka mmoja interest rate inapanda na unaweza lipia nyumba kwa miaka 20 ukawa hujapunguza deni isipokuwa umelipa interest kwa miaka yote hiyo.
Hawa Sullivan ni maelewano yetu sisi na wao na kwa mara ya kwanza Tanzania inaweza kufanya biashara na mashirika na nchi za nje badala ya sisi kutegemea G8 ambao siku zote wamekataa hata kutupa nafasi ndani ya kamati zao za uchumi acha mbali kukaa nao kitako kujadili biashara, hadi leo tutaendelea kupangiwa bei ya mali zetu..
Je, JK anaweza kuwa kashikwa na jamaa?.. hilo sina uhakika hadi sasa lakini Sullivan haihusiani kabisa na jamaa hawa wa EHM.
 
Lakini unakubaliana nami kuwa Mkapa ndiye aliyeuza nchi kulingana na kitabu chenyewe!
Maanake nisha jua unakotaka kwenda baada ya kuona unakotoka..

..hujajua!

..inaonekana hujakisoma kitabu vizuri!kama ameuza then yeye sio ehm!

..ehm ni mtu aliyesoma,mwenye kazi nzuri halafu anakuwa trained kwenye somo la kutengeneza miradi mizuri ya maendeleo [japo karatasini] na kunolewa skills za ushawishi. deal la miradi hii ni kuwaingiza vipofu kwenye lindi la madeni na hivyo utegemezi usioisha!

..huyu anachomekwa kwenye orgs. kama wb,imf,usaid na dfid. unaambiwa ni mtaalamu wa mradi huu au ule. yeye akiandika mradi au kuwasaidia kuandika haukosi fedha. infact,huwa anakuja na miradi kabisa!

..mfano wa mradi kama huu ni songas!

..sasa nadhani umenielewa!
 
Back
Top Bottom