Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Nilikuwa naangalia taarifa za habari kwenye luninga jana kuhusiana na michezo ya Jumuiya ya Madola, utani pembeni, jamaa wamechemsha vibaya sana. Yawezekana kabisa michezo safari hii isiendelee. Sasa ukijumuisha hii habari za uchafu na vivuko kubomoka, habari kwamba akina Husein Bolt na Assafa Powel hawatakuwepo zinafanya mvuto uliozoeleka na unaotegemewa kwa michezo kama hii upungue kwa kiwango kikubwa sana. Na hii leo nasikiliza BBC World wanasema kuna baadhi ya wanamichezo wa baadhi za nchi wamesha anza kuchomoa.
Mimi nilitegemea kikwazo kikubwa kitakuwa ughaidi, lakini jingine kabisaa ndiyo limejitokeza. Je, michezo itaendelea au itaairishwa?! One for the bookies!!