Commision and ommision mistakes

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Miongoni mwa mambo wanasiasa wanasahau ni aina ya makosa mtu aweza kufanya akiwa madarakani. Kuna commission mistakes- makosa ya kufanya visivyo sahihi na Ommision mistakes- makosa ya kushindwa kufanya mambo sahihi.
Kama wewe siyo fisadi/mwizi lakini watu waliochini yako, wanaowajibika kwako wakahujumu mali na kuiba, unawajibika kuwachukulia hatua vinginevye utakuwa na dhambi ya ommision- umeshindwa kufanya yaliyo sahihi, nawe unageuka kuwa fisadi!
Kama viongozi wetu siyo wezi/mafisadi lakini watu waliochini yao ni mafisadi, kwa kuwa hakuna hatua walioichukua dhidi yao basi inayoonekana na kuwaridhisha wananchi basi na wao ni Mafisadi.
Waziri mkuu kukataa shangingi wakati mawaziri wake wote wanaziendesha, asichukue hatua ya kuwazuia nao kuwa nazo haina maana, ana dhambi ya ommision- kushindwa kufanya mambo ambayo anafahamu fika kuwa ndiyo mambo sahihi ya kufanya kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Raisi kushindwa kuwachukulia hatua wezi na kusema kuwa mimi simo haiwezi kumsaidia, hiyo ni Ommision- anatuhumiwa kushindwa kufanya mambo tuliyomkabidhi kusimamia.
Siasa ni ngumu, siyo kitu cha kukimbilia, inabidi uwe msafi ili uweze kuwaadabisha walio wachafu chini yako!
 
umesomeka vilivyo, lakini kwani wanasikia?


Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Omission or failure to act while a person is legally bound to act constitutes a criminal offence provided that omission is done intentionally.
Acting in favour of crooks whether being friends and relatives is equally the same!
 
Back
Top Bottom