Bila kujali kelele na yaliyosemwa juu ya Hayati Magufuli, kuna ulazima wa haraka sana kumpata mwingine wa aina yake

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,956
4,144
Hata kama staandika matarajio yenu, kifupi ni kwamba, Tanzania inahitaji tena na kwa haraka mno mtu mwenye mfanano na hayati JPM,

Tuambizane ukweli, ni nani miongoni mwenu ambaye anaweza kuwa Rais wa nchi, wananchi wake wakalemewa na ukali wa maisha namna hii akaendelea kuwaonea huruma mafisadi,? Kusafiri tu kumekuwa ni anasa? Achilia mbali kusafiri, unapaswa pia uendelee kumwomba Mungu ili isitokee umeuguliwa na ama kuugua! Ndo utajua hujui! Hapa tunaongelea miaka miwili tu, Je mitano itakuwaje? Kuna wengine wanasema eti iende hadi 2030???? Wale watafiti wa ndoa mtatuletea jibu la wanandoa wangapi walikimbiana na ndoa ngapi zilifungwa ukilinganisha na miaka mingine kumi iliyopita...!

...............................................................................

Watanzania acheni kuendekeza ujinga, uzembe na ulalamishi

Wengi wenu ni walalamishi na msiopenda kabisa kufanya kazi, (wavivu wa kupindukia) mnapenda starehe bila kujali mnachoingiza

Familia zote masikini chanzo ni baba legelege, baba asiyeweka mfumo na mwongozo thabiti juu ya watoto wake, ni kuandaa mababa wengine walioferi maisha tokea kwa makuzi yao

Nikikumbuka kipindi cha huyo mwamba, kila mtu alipenda kufanya kazi, maofisini nako vile vile kwa sababu baba alikuwa ni mchapa kazi, mkemea uzembe, mkemea wezi na kila maovu, JPM aliwakemea mpaka viongozi wastasfu kwa sababu alijua nini anafanya juu ya nchi hii yenye watu masikini na sio tu masini, bali pia ni nchi yenye wajinga wenge!

Hayati Magufuli alikuwa ni mwalimu mzuri wa mapato na matumizi pia, kila kilichokuwa kikipatikana, kilielekezwa sehemu hisika tu na kufuatiliwa kwa ukaribu

Na ndiyo maana karibu kila mradi ulikuwa ukienda vema kwa sababu shilingi ilikuwa haipotei ovyovyo,

Nikiangalia sasa tulipo na tunavyokwenda, tumekopa matrilioni ya shilingi, na bado miradi ya kimkakati inasuasua, nani aseme tupo kwenye njia sahihi? Hivi ni nani mpaka muda huu kawajibishwa kwenye ripot ya CAG iliyovunja records ya upotevu wa mabilion ya shilingi, nani kajihudhuru walau tuweke imani kwa wanaotuongoza? Nani kafikishwa mahakamani ili tuseme tunatendea haki wananchi??

Mgogoro wa Wizara ya Nishati na wananchi, ni kama kumekosekana mtu wa kuutibu huu mgogoro, visingizio viingi na havijawahi kuisha, kwa nini tuwe na mgao wa umeme?? Tunakosa nini yaani, mwenye jibu wa swali hili nitamlipia ya bando la mwezi mzima, kwa nini kuwe na mgao wa umeme Tanzania kama siyo ulegelege na uzembe tu uliokubuhu?

Kama tunataka kuwa nchi inayopiga hatua kiuchumi na kuwa nchi inayoheshimika nje ndani, basi tunamhitaji mfano wa mtu aliyepita, yaani JPM asiyeogopa kufa kwa ajili ya maisha ya wengi ili akabiliane na wezi, mafisadi, wazembe na makuwadi wa kisiasa na machawa yaliyokosa kazi za kufanya, yanaabudu watu ili yalipwe badala ya kufanya kazi halali!

Wale kufokafoka karibuni mfoke, na sababu ni moja tu, maslahi yenu yaliyojengwa kwenye wizi na ujanjaunja, ndiyo huwa hamtakaki viongozi kama hao!

Mwisho, Ipo siku itajulikana iwapo Rasilimali Mungu alizotupa zilipaswa kulindwa kwa nguvu na kwa jicho la husuda kama alivyokuwa akifanya JPM na au tuendelee kuziona ni kama Mungu alituwekea kwa bahati mbaya na hatuzitaki!
 
Hata kama staandika matarajio yako, kifupi ni kwamba, Tanzania inahitaji tena na kwa haraka mno mtu mwenye mfanano na hayati JPM,

Watanzania acheni kuendekeza ujinga, uzembe na ulalamishi

Wengi wenu ni walalamishi na msiopenda kabisa kufanya kazi, (wavivu wa kupindukia) mnapenda starehe bila kujali mnachoingiza

Familia zote masikini chanzo ni baba legelege, baba asiyeweka mfumo na mwongozo thabiti juu ya watoto wake, ni kuandaa mababa wengine walioferi maisha tokea kwa makuzi yao

Nikikumbuka kipindi cha huyo mwamba, kila mtu alipenda kufanya kazi, maofisini nako vile vile kwa sababu baba alikuwa ni mchapa kazi, mkemea uzembe, mkemea wezi na kila maovu,

JPM alikuwa ni mwalimu mzuri wa mapato na matumizi pia

Na ndiyo maana karibu kila mradi ulikuwa ukienda vema kwa sababu shilingi ilikuwa haipotei ovyovyo,

Nikiangalia sasa tulipo na tunavyokwenda, tulivyokopa matrilioni na bado miradi ya kimkakati inasuasua

Mgogoro wa Wizara ya Nishati na wananchi, ni kama kumekosekana mtu wa kuutibu huu mgogoro, visingizio viingi na havijawahi kuisha

Kama tunataka kuwa nchi inayopiga hatua kiuchumi na kuwa nchi inayoheshimika nje ndani, basi tunamhitaji mfano wa mtu aliyepita, yaani JPM wa pili ili akabiliane na wezi, waongo, wazembe, chawa n.k

wa kufokafoka karibuni mfoke, na sababu ni moja tu, maslahi yenu yaliyojengwa kwenye wizi na ujanjaunja, ndiyo huwa hamtakaki viongozi kama hao!
Itachukua miaka 100 kumpata anayefanana atabaki hana mfano!
 
Binafsi kwa sasa namuona Mwabukusi kama ana element hizo kwa sana sema sasa kwa mifumo yetu aise si rahisi sana watu wa karba hiyo kuiona tena ikulu. Maana ni kama hata watu wa usalama wa taifa na majeshi yote yametekwa na wanasiasa wenye nia ovu.

Ila ukweli ni kwamba viongozi wa aina ya JPM wanahitajika sana kwenye taifa nunda kama hili la kwetu. Sema wanatakiwa kurekebisha tu mapungufu kidogo yaliyokuwepo kwa JPM otherwise taifa linahitaji kiongozi thabiti asiyemuogopa yeyote linapokuja suala la maslahi ya taifa.
 
JPM alipaswa awe kiongozi wa juu wa nchi amabazo azina mfumo wa kidemokrasia, hakika angeweza kuijenga hiyo nchi.

Huku kwenye demokrasia, angeishia kama alivyo ishia, kuua, kuumiza, kunyang'anya na kupora,

Aliipenda nchi hii na kuwapenda wanao msikiliza na kumtii, Aliwachukia wote wenye mawazo mbadala na tofauti na yeye,

Kama kuna mtu anamtaka JPM mwingine, atengeneze nchi yake kisha ampeleke huko sio hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom