Coming very soon....'majeruhi wa mapenzi'...

Tatizo wachapishaji wetu wa kibongo maringo jamani; watu wanataka uwabembelezeeeee. Unatuma email hawajibu au hata kuacknowledge, unapiga simu hawapokei, ukikaa kimya wanakuandikia email "mambo yanaendeleaje".. wakati kuna mtu Kenya anabembeleza ati niachapishe huko na ananimwagia advantage kibao!!!
 
Mkuu, huu ni ulimwengu wa ushindani, ikiwa umepata wachapishaji kutoka Kenya au kokote watumie halmuradi tu iwe kuna maslahi. Mara nyengine uzalendo inabidi utushinde. Kila la heri.
 
Companero umenikumbusha Agoro Anduru

Mbona huyo Rosa Mistika ni wa Euphrase Kezilahabi, ukiacha Nunda mla Watu wa Ben Mtobwa hakuna mwanamke mjeruhi mapenzi kama huyo katika riwaya za Kitanzania!

Kama Erica kawazidi Nunda na Rosa nitanunua nakala zaidi ya moja nigawe kwa majeruhi wengine wa mapenzi ila nahisi ni mchovu maana inaonekana kazidiwa na Dkt Shedrack Smith!
 
Mwanamkijiji, hii hadithi utaiweka humu JF au ni kitabu kitauzwa mitaani?

Yeah, sasa hivi mgogoro uliopo ni uamuzi wa wapi kipigwe chapa; maana kuna wengine wanasema China, wengine Bongo (nichangie ajira n.k) na wengine wanasema hapa hapa kijijini kwani itakuwa rahisi kufuatilia hatua zake mbalimbali... bado hatujaamua labda in aweek or so tutakuwa tumepata mawazo ya kutosha..

@all, thanks!!!
 
Mbona huyo Rosa Mistika ni wa Euphrase Kezilahabi, ukiacha Nunda mla Watu wa Ben Mtobwa hakuna mwanamke mjeruhi mapenzi kama huyo katika riwaya za Kitanzania!

Kama Erica kawazidi Nunda na Rosa nitanunua nakala zaidi ya moja nigawe kwa majeruhi wengine wa mapenzi ila nahisi ni mchovu maana inaonekana kazidiwa na Dkt Shedrack Smith!

Well... right on kwenye Kezilahabi sijui ni ipi imenikumbusha Agoro Anduru.. I promise you hujamsoma mwanamke kama Erica kwenye stori yoyote before!! Ni mtundu kuliko Rosa Mystica, mjeuri kama Helen Jeuri ana mbwembwe kumpita Betina lakini kupenda kwake kunazidi yule mwanamke wa Joram Kiango!
 
Marketing strategy ya uhakiki wa kitabu inaendelea huku UDADISI: Rethinking in Action: NI ZAIDI YA MAPENZI?

Nimependa take yako; ila ni riwaya ya mapenzi na "yaliyomo"... maudhui yake makubwa ni "nature ya mahusiano".. inajaribu kujibu swali - je mtu anaweza kuumizwa katika mapenzi na kubakia na makovu yasiyopona? Inakuwaje kama makovu hayo hutoneswa toneswa katika maisha? na maswali mengine yanayohusiana na saikolojia na uchumi wa mapenzi
 
Mwanamkijiji, hii hadithi utaiweka humu JF au ni kitabu kitauzwa mitaani?

Kitakuwa kitabu cha kuuzwa mitaani - almost a 200 pages; so si kitabu cha watu wanaopenda stori fupi fupi. Kina maneno yasiyopungua 50,000!!!
 
Well... right on kwenye Kezilahabi sijui ni ipi imenikumbusha Agoro Anduru.. I promise you hujamsoma mwanamke kama Erica kwenye stori yoyote before!! Ni mtundu kuliko Rosa Mystica, mjeuri kama Helen Jeuri ana mbwembwe kumpita Betina lakini kupenda kwake kunazidi yule mwanamke wa Joram Kiango!

femme fatale!
 
Tatizo wachapishaji wetu wa kibongo maringo jamani; watu wanataka uwabembelezeeeee. Unatuma email hawajibu au hata kuacknowledge, unapiga simu hawapokei, ukikaa kimya wanakuandikia email "mambo yanaendeleaje".. wakati kuna mtu Kenya anabembeleza ati niachapishe huko na ananimwagia advantage kibao!!!
Bongo ni kawaida sana muuza duka kumwambia mteja "katafute chenji ni nikuuzie" yaani eti wee mnunuzi urudi utafute hela ndogo ndo upate huduma wakati mwenye duka kakaa tu, kitu ambacho ni ukikuti kwa wa ganda au wakenya!
 
...nice cover, lakini mpaka nisikie watu wa kikisifu baada ya kukisoma ndio ntanunua...."don't judge a book by lokin its cover"
 
"Erica, kifo cha Alex hakiingii akili kabisa" alianza kujielezea na sauti yake ikipata uhai wa aina fulani. "Yaani, it doesn't make any sense kabisa; yaani alikuwa na furaha muda wote na wewe unajua hivyo sasa ni kitu gani kingemfanya aamue kuutoa uhai wake?" Lilikuwa swali ambalo Erica hakutegemea kuja kuulizwa na mara moja alijisikia kifua kinabana. Alihisi hasira na kukereka kupita kiasi. Alianza kuingiwa na ghadhabu ambayo ilikuwa inajaa taratibu kama bia kwenye glasi au kupanda kwa moshi kwenye volcano ya mlima wa Eldonyo Lengai; kuwa kwanini Husna rafiki yake wa tangu utoto anaingia kwenye eneo ambalo hakupaswa kuingia. "Huwezi kujua Husna labda alikuwa na matatizo yake" "Matatizo gani ya ghafla namna hiyo Erica, fikiria. He was really happy!" "Husna muache kaka wa watu apumzike kwa amani" alisema na kuchukua glasi yake ya maji na kuisogeza mdomoni. "Erica unajua kilichomfanya Alex ajiue?" Mwiko ulivunjwa na swali ambalo lilikuwa mawazoni mwa Husna lilitokea kama mwali akitolewa nje wakati wake ukifika. Kulikuwa na ukimya wa ajabu uliofuata ambao ulikuwa ni kama ukimya wa kati ya radi na ngurumo. Swali la Husna lilikuwa ni radi. Ngurumo ilikuwa inasubiriwa.... MAJERUHI
 
mmmmh aya bwana still waiting...........
 
Back
Top Bottom