Combination ya Makinda na JK imeingiliwa na mapepo wabaya!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
Hawa ni viongozi wakuu wa hii mihimili 2 ya dola yaani serikali na bunge.Hata hivyo ni bahati mbaya sana kuwa viongozi hawa wameshindwa ku-deliver tena kwa kiasi kikubwa katika kusimamia hiyo mihimili wanayoiongoza.

Kwa mfano,serikali imekuwa haietekekezi maazimio mbalimbali ya bunge kama vile maazimio kuhusu Richmond,Jairo na mengine mengi.Pia kila mwaka bajeti zinazotengwa kwa kila wizara hazitimii yaani fedha zinazotengwa sizo zinazotumika,matumizi ya fedha yasioidhinishwa na bunge n.k.Hiyo ni mifano michache ya "madudu" ya serikali ambayo yamegeuka wimbo kwa wabunge na kero kama sio mzigo kwa watanzania.

Bunge kama chombo kinachotakiwa kuisimamia na kuishauri serikali,kimekuwa ni chombo cha kuilinda na kuitetea ssrikali kwa gharama ya mtanzania masikini.Bunge hili chini ya Makinda limekuwa ni bunge la ndio hata kwa hoja za "kijinga" na bajeti za "kiinimacho"!

Ukichunguza kwa makini utagundua wazembe ni mwenyekuti wa baraza la mawaziri ambae ndio Raisi wa nchi kwa kushindwa kusimamia vikao vya baraza na kuja na maamuzi au mipango iliyo bora na badala yake wanafanta maamuzi ya kisiasa zaidi kwa mfano kuitengea wizara moja fedha nyingi kuliko wizara zingine kila mwaka ili waje wajisifu kuwa wamejenga barabara na iwe mtaji mwaka 2015!Ovyo kabisa!

Uzembe mwingine uko katika uongozi wa Bunge kwani bunge limegeuka kuwa mtetezi wa serikali!Spika wa bunge kama kiongozi mkuu wa chombo hiki,akisikia serikali inasemwa vibaya bungeni "atafura" kwa hisia ni CCM na siyo serikali ndio inayosemwa!Hii ni hatari sana.Spika badala ya kusimama kidete kuibana serikali kazi hiyo anaona si yake wala bunge bali ni kazi ya wabunge wachache wa upinzani ambao hata hivyo hoja zao zingine atazizima kibabe ili kuiokoa serikali!

Nadhani tangu uhuru hatujawahi kuwa na combination mbovu kama hii na ni imani yangu kuna mkono wa pepo mchafu miongoni mwa viongozi hawa wa mihimili hii.
 
Hapo ndipo ninapopandwa na hasira na pressure nikiyafikiria hayo uliyoyasema. CCM walaaniwe kabisa.
 
Huyo Mama alichaguliwa ili mafisadi watekeleze azma yao,ndio maana waliamua kumtosa mzee wa speed na viwango.
Hali halisi inawaumbua sasa,hali ya maisha kwa Mtu mmoja moja imekuwa ngumu sana kwa sasa kuliko vipindi vingine vilivyopita hapa Tanzania.
Time will tell.2015 si mbali kwa Watanzania kufanya maamuzi magumu.
 
Eti watu wanakaa kusikiliza bajeti,bajeti ambayo ikiwa imeandikwa kwa figure huku pesa harisi haonekani itatoka wapi

Bajeti ambayo tokea imeanza kusomwa hakuna wizara imewahi kupata walau 70% ya pesa iliyoandikwa vitabuni

Huwa sielewi katika mazingira ya hivi serikali inatoa wapi mbwembwe kila mwaka huku hesabu za jana kamwe hazitimii,hizi ni bajeti za mdomoni tu.
 
Mkuu huu uzembe wa serikali ni matokeo ya kuwa na bunge "kibogoyo"!
 
Huyo Mama alichaguliwa ili mafisadi watekeleze azma yao,ndio maana waliamua kumtosa mzee wa speed na viwango.
Hali halisi inawaumbua sasa,hali ya maisha kwa Mtu mmoja moja imekuwa ngumu sana kwa sasa kuliko vipindi vingine vilivyopita hapa Tanzania.
Time will tell.2015 si mbali kwa Watanzania kufanya maamuzi magumu.

watanzania Wabongo sahau labda watanzania wengine.
 
..mihimili yote mitatu chini ya utawala huu imeoza.....umesahau mahakama....nako kumeoza.....kesi kubwa haziishi.....haswa zinazowahusu vigogo.......wanaofungwa jela ni wezi wa kuku na simu....lakini wauza unga wanaokamatwa kila kukicha airport husikii wakihukumiwa.....ama majizi makubwa ya fedha za umma...kesi zao zinapigwa tarehe tu.....kwa kifupi mihimili yote ya nchi hii imeoza na inahitaji total overhaul....ambayo ingeanzia kwenye katiba mpya....ambayo nayo kwa bahati mbaya sana sana utawala huu unaichakachua rasimu ambayo ingeleta mapinduzi kwenye mihimili hii.....nchi hii imeoza....
 
Hawa ni viongozi wakuu wa hii mihimili 2 ya dola yaani serikali na bunge.Hata hivyo ni bahati mbaya sana kuwa viongozi hawa wameshindwa ku-deliver tena kwa kiasi kikubwa katika kusimamia hiyo mihimili wanayoiongoza.

Kwa mfano,serikali imekuwa haietekekezi maazimio mbalimbali ya bunge kama vile maazimio kuhusu Richmond,Jairo na mengine mengi.Pia kila mwaka bajeti zinazotengwa kwa kila wizara hazitimii yaani fedha zinazotengwa sizo zinazotumika,matumizi ya fedha yasioidhinishwa na bunge n.k.Hiyo ni mifano michache ya "madudu" ya serikali ambayo yamegeuka wimbo kwa wabunge na kero kama sio mzigo kwa watanzania.

Bunge kama chombo kinachotakiwa kuisimamia na kuishauri serikali,kimekuwa ni chombo cha kuilinda na kuitetea ssrikali kwa gharama ya mtanzania masikini.Bunge hili chini ya Makinda limekuwa ni bunge la ndio hata kwa hoja za "kijinga" na bajeti za "kiinimacho"!

Ukichunguza kwa makini utagundua wazembe ni mwenyekuti wa baraza la mawaziri ambae ndio Raisi wa nchi kwa kushindwa kusimamia vikao vya baraza na kuja na maamuzi au mipango iliyo bora na badala yake wanafanta maamuzi ya kisiasa zaidi kwa mfano kuitengea wizara moja fedha nyingi kuliko wizara zingine kila mwaka ili waje wajisifu kuwa wamejenga barabara na iwe mtaji mwaka 2015!Ovyo kabisa!

Uzembe mwingine uko katika uongozi wa Bunge kwani bunge limegeuka kuwa mtetezi wa serikali!Spika wa bunge kama kiongozi mkuu wa chombo hiki,akisikia serikali inasemwa vibaya bungeni "atafura" kwa hisia ni CCM na siyo serikali ndio inayosemwa!Hii ni hatari sana.Spika badala ya kusimama kidete kuibana serikali kazi hiyo anaona si yake wala bunge bali ni kazi ya wabunge wachache wa upinzani ambao hata hivyo hoja zao zingine atazizima kibabe ili kuiokoa serikali!

Nadhani tangu uhuru hatujawahi kuwa na combination mbovu kama hii na ni imani yangu kuna mkono wa pepo mchafu miongoni mwa viongozi hawa wa mihimili hii.

muite mama yako awe spika
 
..mihimili yote mitatu chini ya utawala huu imeoza.....umesahau mahakama....nako kumeoza.....kesi kubwa haziishi.....haswa zinazowahusu vigogo.......wanaofungwa jela ni wezi wa kuku na simu....lakini wauza unga wanaokamatwa kila kukicha airport husikii wakihukumiwa.....ama majizi makubwa ya fedha za umma...kesi zao zinapigwa tarehe tu.....kwa kifupi mihimili yote ya nchi hii imeoza na inahitaji total overhaul....ambayo ingeanzia kwenye katiba mpya....ambayo nayo kwa bahati mbaya sana sana utawala huu unaichakachua rasimu ambayo ingeleta mapinduzi kwenye mihimili hii.....nchi hii imeoza....

Jeshi linatakiwa lifanye yale mambo alafu system ikisharekebishwa chini ya usimamizi wao wang'atuke madarakani.
 
Back
Top Bottom