Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India
2205634.jpg

Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India Tuesday, June 09, 2009 9:17 PM
Chura anayebadilika rangi tofauti tofauti muda wote ambaye aligunduliwa hivi karibuni nchini India na mwanaume mmoja wakati akimwagilia maji bustani yake amekuwa kivutio kikubwa kiasi cha kwamba mamia ya wahindi wanamiminika kumuona na wengine wanamuabudu kama mungu. Mamia ya wahindi wanamiminika kwenye mji wa Kerala kumuona na kufanya maombi yao kwa chura ambaye muda wote anabadilika badilka rangi na kuwa na rangi tofauti.

Reji Kumar, mkazi wa mji wa Kerala alimgundua chura huyo kwenye bustani yake wakati akimwagilia maji na baadae alimuhifadhi kwenye chupa.

Reji anahofia chura huyo anaweza akafariki baada ya kugoma kula tangia mamia ya watu walipoanza kumiminika nyumbani kwake kumuona.

"Tatizo ni kwamba huyu chura ameacha kabisa kula, najaribu kila njia kumlisha lakini amegoma kabisa".

Chura huyo alikuwa rangi nyeupe wakati Reji alipomgundua baada ya muda mfupi aligeuka kuwa njano na alipomfikisha nyumbani kwake chura huyo alibadilika na kuwa wa kijivu.

"Usiku ulipofika alibadilika na kuwa rangi ya njano iliyokolea na baadae akabadilika tena na kuwa na rangi iliyoonyesha viungo vyake vya ndani " alisema Reji.

"Ni kama muujiza vile chura kuwa na uwezo wa kubadilika rangi mbali mbali watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi kumuona na kupiga dua zao".

Profesa Oommen V. Oommen wa chuo kikuu cha Kerala University alisema kuwa si kawaida kwa wanyama kubadilika rangi.

"Chura hubadilika rangi kuwatishia maadui zao wanapokuwa hatarini, lakini chura wa Reji kwa jinsi anavyobadilika rangi tofauti tofauti kila mara si jambo la kawaida" alisema Profesa Oommen.

Wataalamu wa wanyama nchini India wana mpango wa kumchukua chura huyo kumfanyia uchunguzi kujua inakuwaje anabadilka badilika rangi namna hiyo.

Chura ni miongoni mwa wanyama wanaoabudiwa nchini India, miungu mingine ya wahindi ni njiwa na ng'ombe.
 
chura anayebadilika badilika rangi aabudiwa kama mungu india
2205634.jpg

chura anayebadilika badilika rangi aabudiwa kama mungu india tuesday, june 09, 2009 9:17 pm
chura anayebadilika rangi tofauti tofauti muda wote ambaye aligunduliwa hivi karibuni nchini india na mwanaume mmoja wakati akimwagilia maji bustani yake amekuwa kivutio kikubwa kiasi cha kwamba mamia ya wahindi wanamiminika kumuona na wengine wanamuabudu kama mungu. Mamia ya wahindi wanamiminika kwenye mji wa kerala kumuona na kufanya maombi yao kwa chura ambaye muda wote anabadilika badilka rangi na kuwa na rangi tofauti.

Reji kumar, mkazi wa mji wa kerala alimgundua chura huyo kwenye bustani yake wakati akimwagilia maji na baadae alimuhifadhi kwenye chupa.

Reji anahofia chura huyo anaweza akafariki baada ya kugoma kula tangia mamia ya watu walipoanza kumiminika nyumbani kwake kumuona.

"tatizo ni kwamba huyu chura ameacha kabisa kula, najaribu kila njia kumlisha lakini amegoma kabisa".

Chura huyo alikuwa rangi nyeupe wakati reji alipomgundua baada ya muda mfupi aligeuka kuwa njano na alipomfikisha nyumbani kwake chura huyo alibadilika na kuwa wa kijivu.

"usiku ulipofika alibadilika na kuwa rangi ya njano iliyokolea na baadae akabadilika tena na kuwa na rangi iliyoonyesha viungo vyake vya ndani " alisema reji.

"ni kama muujiza vile chura kuwa na uwezo wa kubadilika rangi mbali mbali watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi kumuona na kupiga dua zao".

Profesa oommen v. Oommen wa chuo kikuu cha kerala university alisema kuwa si kawaida kwa wanyama kubadilika rangi.

"chura hubadilika rangi kuwatishia maadui zao wanapokuwa hatarini, lakini chura wa reji kwa jinsi anavyobadilika rangi tofauti tofauti kila mara si jambo la kawaida" alisema profesa oommen.

Wataalamu wa wanyama nchini india wana mpango wa kumchukua chura huyo kumfanyia uchunguzi kujua inakuwaje anabadilka badilika rangi namna hiyo.

Chura ni miongoni mwa wanyama wanaoabudiwa nchini india, miungu mingine ya wahindi ni njiwa na ng'ombe.
wahindi kwa kuabudu abudu kila wanachokiona..
Hakika ni mabingwa,.
David beckham alitembelea india naye alipewa hadhi ya umungu...
Cha ajabu wakija hapa kwetu wao ndio wanageuka miungu na watawala wetu wanawaabudia
 
Back
Top Bottom