Chupuchupu Chinjachinja ya CCM Arusha

Nero

Member
Apr 24, 2012
93
21
Ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni nikiwa natoka maeneo ya daraja mbili kuelekea relini,ndipo nikakutana na manjemba 2 mmoja alikuwa na panga mwingine alikuwa na kipande cha chuma (nondo). Baada ya kuwaona nikasimama gafla mara nikaona 1 ananipita kwa upande wa kulia na mwingine kushoto. Nilipoona hivyo nilitoka nduki kupita upande wa kuchoto kwa mwenye nondo gafla akataka kunilenga na ile chuma bahati nzuri hakunipata akalenga nyumba ambayo nilipita karibu. Wadau nilicho ona ni kipande cha tofali ikipaa juu. Wana JF nipeni ushauri nifanyeje napata wasiwasi ya kuishi ktk mji huu japo ndiyo home. Asante mungu kwa kuninusuru ktk chinjachinja ya Ccm.
 
Pole Mungu amekunusuru angalia namna ya kuokoa maisha yako na jamaa yako pisha kidogo hapo.
 
Mkuu, I can feel you. Pole sana mwana!
Caution na muda wa kutembea nyakati hizi.
Nikiwa pande za huko huwa sijiamini sana, nahisi vulnerable. Hasahasa taarifa za m/kiti wa CDM kuuawa kinyama.

Usitembee late, penye kidistance kama umechelewa chukua bodaboda, elfu tano si kitu, hasara roho.

Usionyeshe itikadi zako za chama waziwazi popote. Huwezi jua mbaya wako licha ya kwamba anakutabasamia.

Mshukuru sana Mungu!
 
kaza uzi bro! Ingekuwa dini ningesema ufe ili sisi wenye shida tuokolewe na mdomo wa chama cha mafisadi, lakini nakuomba sasa nawe uwe ngangari hasa kujua kila kona ya hao chinjachinja na ikibidi upite naye mmoja kimtindo ili wajue jamii huru iko nyuma yako, unaweza kuweka kambi maalumu mahali hapo hapo jijini na wanacdm wa rocky city tuko pamoja nawe kupambana.
 
Pole sana ndugu. Muombe mungu wako mkuu. Napataga story kuwa maeneo hayo ni hatari sana hapo jijini arusha hasa nyakati za jioni na usiku pia. 4 sure mungu amekurehemu.
 
Nashindwa kukiafiki ulicho kizungumza kwa kuwa daraji II/relini napa fahamu vizuri sana hembu weka kwanza wazi ilikuwa ni majira ya saa ngapi?. Kwani ninavyo fahamu mimi kabla na baada ya kuvuka hilo daraja kuna nyumba kibao ziko hapo na watu wana kuwepo nje mpaka mida ya saa tano na vilevil watu waki kusudia kuku tite kwenye hilo daraja siyo rahisi utoke!
 
ripoti polisi na ninajua arusha ni mabingwa wa sungusungu kwani walimaliza dhahma ya kambi ya fisi

undeni sungusungu ya chadema mmalize hiyo shida inayowashinda polisi
 
Pole sana ila kamanda kuwa mwangalifu usipende tembea usiku sasa hapo arusha naona hali si shwari. Au ilikuwa ni muda gani huo hiyo kash kash ilikupata?....
 
Ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni nikiwa natoka maeneo ya daraja mbili kuelekea relini,ndipo nikakutana na manjemba 2 mmoja alikuwa na panga mwingine alikuwa na kipande cha chuma (nondo). Baada ya kuwaona nikasimama gafla mara nikaona 1 ananipita kwa upande wa kulia na mwingine kushoto. Nilipoona hivyo nilitoka nduki kupita upande wa kuchoto kwa mwenye nondo gafla akataka kunilenga na ile chuma bahati nzuri hakunipata akalenga nyumba ambayo nilipita karibu. Wadau nilicho ona ni kipande cha tofali ikipaa juu. Wana JF nipeni ushauri nifanyeje napata wasiwasi ya kuishi ktk mji huu japo ndiyo home. Asante mungu kwa kuninusuru ktk chinjachinja ya Ccm.

pole ndugu kwa yaliyokusibu lakini ni jinsi gani umenisononesha kwa uwoga uliyokuwa nao na vipi hapo kwenye chama kimeusikaje ?
 
how sure are we? Pengine umetumwa!!!! Haya pole na usirudie kutembea usiku watu wanahasira na arumeru bado, wasikumwenyekiti bure.
 
Nunua pisto mkuu ujilinde mwenyewe. Wamarekani hawakuwa wajinga kujipa uhuru wa kumiliki silaha kwa lengo la kujilinda.
Before I take off my watch,
I'll aim at your chest trying to take off your heart.
Silaha ni muhimu kwa maisha ya siku hizi.
 
Kwanini umewahusisha jamaa na CCM?walikuwa na sare za ccm?au silaha zao zilikuwa na rangi ya kijani?Kwann usidhani kuwa labda ni vibaka?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom