DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 72
- 108
Chuo Kikuu cha Dodoma kuna tatizo, Wanachuo tumelipa ada na kujisajili mapema lakini mpaka tunafika mwisho wa mhula hatuna Vitambulisho.
Kibaya zaidi Sheria au utaratibu wa hapa ulivyo haturuhusiwi kuingia kwenye mtihani bila kitambulisho hai (active), yaani unatakiwa kuwa na ID ambayo haijaisha muda wake, tofauti na hapo hauwezi kuruhusiwa kufanya mtihani.
Mfano 22-02-2023, hadi umefika muda wa kuingia kwenye mtihani baadhi ya wanafunzi hatuna vitambulisho, tunalazimishwa ku-pex mitihani tufanye mitihani maalum yaani Special Examination mwezi Septemba.
Nimeshuhusia baadhi ya Wanafunzi Wanawake wakiangua kilio kwa kushindwa kupata kitambulisho na muda wa mtihani ukiwa unakaribia.
Unadhani hapo utaingia ukiwa na akili tulivu hata kama itatokea umekipata dakika za mwisho, baadhi yao walikuwa wameshaamua kusogeza mbele muda wa kufanya mtihani walipoona hadi 2 hours before mtihani hawajapata vitambulisho, wakaamua kuingia katika mfumo wa chuo na kubadili ratiba zao.
Ajabu wakati wakifanya hivyo wengine wakaambiwa wanaweza kutumia vitambulisho vya zamani kufanya mtihani, kwa ufupi ni mvurugano, hiki ni chuo kikubwa lakini kwa matendo kama haya inakuwa sio sawa.
Kingine ambacho tunajiuliza ni kuwa, je, tunaosogeza mbele muda wa kufanya mitihani hizo gharamia za nauli, chakula na nyinginrzo watazitoa wao? Huu ni uzembe wa uongozi wa chuo na tukifuatili hakuna sababu ya msingi wanazotoa, inaumiza sana.
Majibu ya UDOM- Madai ya UDOM kuchelewesha vitambulisho vya Wanafunzi, chuo chasema chanzo ni uzembe wa Wanafunzi