Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,211
- 42,073
Tumekuwa tukisikia hapa Duniani hasa Tanzania kuwa huwa kuna degree za bure na wengine wamekuwa wakisema kuna degree za chupi, lakini sijawai kusikia au kuona watuhumiwa wakikiri kufanya uhalifu kabisa hadharani!
Chuo cha Ardhi ni chuo kizuri lakini ikifika hatua ya watu kisa tuu mapacha wanaweza kufanyiana mitihani na wana kiri hadharani kuwa walifanyiana mitihani tena ya supplimentary basi ujue hii ni hatua kubwa na dharau kubwa sana kwa taasisi hasa ya Elimu ya juu na inayo aminika.
Hawa mabinti wanasema waliweza kufanyiana mitihani na walimaliza chuo kikuu Ardhi(ARU) mwaka 2021 hakuna aliyegundua na sasa wanakwenda hadharani kusema kuwa waliweza kufanya hivyo ni wazi dharau sana kwa taasisi hii ya Elimu na inathibitisha kuwa taasisi hii haiko makini na kuna walakini kwenye hutoaji wa Elimu.
Watu wana hangaika sana kupata elimu halafu watu wanaidhalilisha elimu kiasi hiki, hii ni aibu kwa chuo cha Ardhi na Wizara ya Elimu pia.
Watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka sana Elimu zetu hasa utoaji wake na sasa ni wazi wahalifu wameanza kutoa ushahidi wa mashaka kwenye hizi degree zilizojaa mtaani.
Ni matuamaini yangu taasisi itachukua hatua kali dhidi ya uhalifu huu wa kielemu uliofanywa na hawa mapacha na kwenda kukiri hadharani kwenye chombo cha habari Wasafi FM.
Source: Wasafi FM
Pia soma: Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo