Chungu ya Mke wa Mtu...

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
WAPENZI wawili jana walijikuta wakiwa kwenye wakati mgumu baada ya kumaliza shughuli zao za kimapenzi [kujamiiana] kushindwa kuachiana baada mwana baba huyo kushindwa kutoa nyeti zake kutoka kwenye nyeti za mpenzi wake.

Tukio hilo la ajabu na la mwaka lilitokea jana majira ya saa 12:45 jioni huko maeneo Tandale katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Hans Gest.

Tukio hilo la kusisimua ambalo watu wengi walioshuhudia tukio hilo waliliita ni la mwaka kwa kuwa watu wengi waliouwa wakisikia lakini jana walijionea wenyewe kwa macho watu hao wanaita [live].

Chanzo cha kuaminika cha habari hii kilisema kuwa watu hao waliingia kwenye nyumba hiyo wageni majira ya saa 10 jioni na walichukua chumba kimoja kwa ajili ya kupumzika kwa ajili ya wikiendi.

Inasemekana kuwa baada ya wapenzi hao wawili kutimiza azma yao iliyowapeleka hapo walijikuta wameshindwa kuachiana baada ya baba huyo kushindwa kutoa uume wake kutoka kwenye uke wa mpenzi wake na kusababisha aombe msaada kwa wahudumu ili waje kumsaidia.

Inasemekana baada ya kujitahidi kila aina ya ujanja wake alishindwa kujinasua kwa mwanamke huyo na kuamua kuchukua umamuzi wa kupiga kelele ili wahudumu waingie waje kumnasua.

Wahudumu walisikia mayowe yakitokea katika chumba hicho na kukimbilia na kukuta mlango umefungwa, wapenzi hao walipotakiwa kuufungua mlango huo kwa ndani walishindwa mana hakuna aliyeweza kuinuka mahali hapo na kwenda kufungua mlango huo mana walikuwa wameng’anga’niana.

Wahudumu hao walichofanya ni kuvunja mlango huo na kukuta baba huyo akishindwa kujinasua kutoka kwa mwanamke huyo.

Wahudumu hao wakijikuta wamepatwa na kigugumizi cha ghafla na kushindwa la kufanya.

Kadri muda ulivyozidi kwenda hali ilizidi kuwa mbaya kwa baba huyo ilibidi wahudumu hao watoe taarifa kituo cha polisi ili kuja kuwachukua watu hao na kuwakimbiza hospitali.

Pindi polisi walipofika mahali hapo walijaribu kuwauliza wapenzi hao ilikuwaje na kujielezea na mwanamke huyo alipojaribu kuwaeleza alisema yeye ni mke wa mtu na inawezekana atakuwa ametegewa na mume wake akitembea nje ya ndoa ajue.

Alisema amehisi hivyo baada kukumbuka kuwa siku moja mumewe huyo aliwahi kumtamkia kuwa asimuige yeye na kutembea na mwanaume mwingine nje mana akifanya hivyo yeye atajua tu, alishindwa kumuelewa na kujua ni mkwara tu wa wanaume walio wengi.

Alisema labda inawezekena mumewe huyo atakuwa amemfanyia madawa ya kiswahili akikutana na mwanaume ashindwe kutoka ili amkomoe ingawa na yeye anafanya vitendo hivyo kwa kuwa wanawake wa nje.

Askari waliofika katika tukio hilo walimuamuaru dada huyo kutoa namba ya simu ya mumuwe na kuonekana kutokuwa tayari lakini aliamua kutoa ili aweze kujinasua na dhahama hilo.

Askari walimpigia mume wa dada huyo na kumuuliza mahali alipo alisema yuko nyumbani, walipomuuliza mkewe yupo alijibu kuwa mke wake hayupo amemuaga amekwenda kwenye sherehe za akina mama yaani “Kitchen Party” atarudi baadae.

Polisi walimwambia mke wako anaumwa yuko hapa na kumuelekeza mahali hapo na mwanaume huyo kufika na kukuta umati wa watu wakiwa wamezunguka eneo hlo bila kujua kilichotokea, na kuingizwa kwenye chumba hicho na kukuta mke wake akiwa kitandani na mwanaume mwingine akiwa wamegandiana.

Alipoulizwa ni kwa nini ilitokea hivyo hakuwa na jibu na kudai kuwa amedhalilishwa na mke wake huyo na kudai yeye hajui ni kwa nini na kusema kuwa kwa kuwa ameshaona mwenyewe kwa macho yake alitaka apewe ruhusa aende nyumbani baada ya muda wataweza kuwa huru.

Inasemekana baada ya masaa matatu watu hao waliweza kujinusuru na kuachiana na kila mmoja akiwa na aibu tele ya kile kilichowakuta.

Baadae mtu wa karibu wa mwanamke huyo majira ya saa tano ya usiku iliambiwa kuwa watu hao waliweza kuachiana mTukio hilo la ajabu na la mwaka lilitokea jana majira ya saa 12:45 jioni huko maeneo Tandale katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Hans Gest.
 
kwa hiyo kitchen party ndo ilikuwa guest kweli mungu mkubwa ameabika kweli huyo mwanamke?jama alikuwa anakula T..o au ilinasa wapi?
 
Hii ni hadithi ya kutunga..... Hakuna mtu aliyeenda shule atakekubali hizi fiksi zako kwenye karne hii.
 
Hii ni hadithi ya kutunga..... Hakuna mtu aliyeenda shule atakekubali hizi fiksi zako kwenye karne hii.

Naishi maeneo ya Tandale, hakuna Guest inayoitwa iitwayo Hans Gest. This a pure fabrication and distortion of reality....
 
Picha ya huo umati lazima itakuwepo ikiwa hii hadithi si ya kutungwa.
 
Hii itakua ni fiksi tuu!siamini hata kidogo kwenye ulimwengu huu wa utandawazi!ina maana hata mzee akilala itang'ang'ania tuu?haiingii akilini kabisa!labda angesema jogoo aligoma kupanda mtungi kidogo ingeinga akilini!
 
Mleta thread, kupunguza speculation ili JF tupate taarifa sahihi zenye credibility ni vyema ukaleta chanzo cha habari yako, tafadhali.
 
Hii itakua ni fiksi tuu!siamini hata kidogo kwenye ulimwengu huu wa utandawazi!ina maana hata mzee akilala itang'ang'ania tuu?haiingii akilini kabisa!labda angesema jogoo aligoma kupanda mtungi kidogo ingeinga akilini!

Mimi naamini ilitokea hata kwenye medical history kuna kitu kama hiki. Mwanamke anaweza kuwa na uoga fulani muscles zake zika tight mwanaume akashindwa kutoka. Msibishe waulize ma dakitari
 
Hiyo case siyo ya kwanza nasikia watu wa Tanga wanafanyiana sana. Iliwahi kutokea Kampala miaka ya nyuma.

Hata mimi niliwahi kusikia kipindi fulani nikiwa Mkoa wa Mbeya.Kwa kweli hayo mambo yapo hasa mnapokuwa mnapeana maahadi ya kutosalitiana kwa shingo upande.

Na kama hii ni kweli mwanamke alikiri kuwa siku mwanamke wa huyu jama akicheat basi mshikaji atajua mwanamke akafikiria ni jokes tu sasa ikabidi ajaribu ili aone kama mumewe atajua.

Wakuu hii kitu ipo tena sana naomba mtu anayebisha aende Mkoa wa mbeya au Tanga akaulizie hayo ni mambo ya kawaida tu.

Kikubwa tu ni kuelewa mke wa mtu ni sumu pita mbali naye ila ukijifanya kuna utandawazi wa kutotokea haya mambo katika ulimwengu huu surely haya mambo yapo.

na kuna wengine wanafanya zindiko la kutokuwa na hamu ya kudo na mke wake pindi anapoamua kucheat ya mashine haionekanai kabisa ila ukitoka nje ipo ukiingia hakuna kitu.

Hivyo tuweni makini wakuu!!!!!
Nawasilisha.
 
wakati nasoma tosamaganga miaka ya 2000, niliwahi kuugua sikio na kwenda hosp ya mkoa kutibiwa. kwa macho yang mawili niliona polisi wanaleta pale hosp watu wawili walioshindwa kuachiana wakati wanafanya mapenzi, ilikuwa kazi kweli kweli
vitu hv vipo, kwa wale ambao hamuamini shauri yenu.
mume alirud baada ya siku 4 ndo akafanya manuva yake ndo wakaachiana na alifanya hvyo baada ya kulipwa pesa lukuki na ndugu wa jamaa aliyeshindwa kuchomoa
 
wakati nasoma tosamaganga miaka ya 2000, niliwahi kuugua sikio na kwenda hosp ya mkoa kutibiwa. kwa macho yang mawili niliona polisi wanaleta pale hosp watu wawili walioshindwa kuachiana wakati wanafanya mapenzi, ilikuwa kazi kweli kweli
vitu hv vipo, kwa wale ambao hamuamini shauri yenu.
mume alirud baada ya siku 4 ndo akafanya manuva yake ndo wakaachiana na alifanya hvyo baada ya kulipwa pesa lukuki na ndugu wa jamaa aliyeshindwa kuchomoa


Mhhhh tutasikia stories hata zisizofanana na ukweli ili mradi kututishia wake wa wenyewe....!
 
Ungeniambia ni story kama hii iliyotoka kwenye gazeti la mwananchi ningekubali.....

Hali ya mkazi wa Ilboru aliyepondwapondwa uume kisha kukatwa ,inazidi kuwa mbaya kutokana na maumivu aliyoyapa.

Kijana huyo alinusurika kufa katika tukio lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Ilboru saa 12.00 jioni baada ya kudaiwa kukutwa chumbani kwa mtu akiwa amejipumzisha na mke wa mtu .

Hadi jana, kijana huyo alikuwa katika afya iliyozorota na huku akilia na kuwaomba ndugu na jamaa zake kufika katika hospitali hiyo ili kumjulia hali yake.

Akiongea kwa taabu ,alisema bado anapata maumivu makali nyakati za usiku na kwamba alikuwa na wasiwasi kama atapona kutokana na maumivu hayo.

Baadhi wauguzi wanaomhudumia mgonjwa huyo, walisema hali ya kijana huyo inazidi kuwa mbaya kadiri siku zinavyozidi kwenda kutokana na uume wake kupondwa kwa kiasi kikubwa.

Alisema wanaendelea na jitihada za kunusuru maisha ya kijana huyo, ingawa hali ya afya yake inazorota kila kukicha .

Baadhi ya watu wa karibu na mgonjwa huyo waliwaambia waandishi wa habari kuwa watu waliomponda hawakuwa waungwana na kwamba wamehama katika mitaa waliyokuwa wakiishi baada ya kutenda kosa hilo.

Waliliomba jeshi la polisi mkoani hapa kufanya jitihada za makusudi ili kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kijana huyo alidai alikuwa na uhusiano na mwanamke huyo kwa siku nyingi na kwamba alimwambia kuwa hana mume na alishangaa siku ya tukio akigongewa mlango na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mume wa mwanamke huyo kisha kuanza kumponda ponda uume na kumkata.
 
Naishi maeneo ya Tandale, hakuna Guest inayoitwa iitwayo Hans Gest. This a pure fabrication and distortion of reality....

Ndugu kuishi sehemu sio kujua kila kitu,mimi sehemu ninayoishi simjui hata jirani yangu,au wewe ni mtumiaji mzuri wa hizo Guest house?
 
Back
Top Bottom