Chonde Chonde Wanasiasa na Helikopta Zenu...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Wanajamvi,

Kwa kipindi hiki cha mwaka, huwa ni mwanzo wa mvua kwa maeneo ya huku Arusha na Kanda nzima ya Kaskazini.
Kwa wanaofika Arusha, wataona bila kuambiwa kuwa eneo la Mlima Meru na maeneo ya jirani yake yako kwenye ukungu muda mwingi.

Na kwa bahati, mbaya, eneo hili ndipo mahali panapo husika na tukio la Uchaguzi, utakaotanguliwa na kampeni za kunadi sera!

Tumeshuhudia tokea miaka ya karibuni vyama kadha vimekuwa vikitumia Helikopta katika kampeni zao, kwa lengo la kuyafikia maeneo mengi katika muda mfupi unaopangwa kwaajili ya kampeni.

Kwa eneo hili la Arumeru, nawatahadharisha sana vyama vyote vitakavyohusika, Visithubutu kutumia helikopta, maana Arumeru yote ni eneo la mlima na vilima, ambavyo kwa majira ya sasa kumefunikwa na Ukungu.

Aidha natambua kuwa Helikopta inahitaji clearance kubwa ya Visibility na Obstacle -Free Zone ili rubani aweze kuona kwa usahihi horizon lines, ambapo kwa eneo la Arumeru kwa sasa hali hiyo ni negotiable.


Wagombea wetu wote tunawapenda sana, na hatutaki kampeni zigeuke kuwa msiba kwa jambo ambalo linaepukika.
Nawasilisha.
 
Tena wale waliopotea Igunga ndo kabisaa wasithubutu!! Maana kama walipotea huko kweupe itakuaje Arumelu?
 
good alert. but wewe unafikiri watumue alternative gani kwa kuwa lengo lilikuwa kuwafikia wapiga kura wengi kwa wakati mdogo.
 
..Sitashangaa nikisikia CCM wameunda Tume/Timu kuchunguza iwapo watumie au wasitumie Helikopta!!!!!!!
 
Tena wale waliopotea Igunga ndo kabisaa wasithubutu!! Maana kama walipotea huko kweupe itakuaje Arumelu?
Kwa hali iliyopo Arumeru si ya kufanya mzaha hata kidogo...Inataka uwendawazimu kuwazia kupeleka ndege Meru!
 
good alert. but wewe unafikiri watumue alternative gani kwa kuwa lengo lilikuwa kuwafikia wapiga kura wengi kwa wakati mdogo.
Mkuu,
Njia ya uhakika inayobaki ni magari...kabla ya mambo ya helikopta magari yalifanikisha kampeni vizuri tu mkuu!
 
PJ, kama hali ni 'negotiable' tutanegotiate hatutashindana.

Anyway kwa jimbo hilo ninavyolijua hakuna haja ya kutumia helkopita kwa sababu maeneo mengi yanapitika na kuna barabara za uhakika.
 
Back
Top Bottom