Chocolate kukufanya mwembamba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
120327100344_chocolate_144x81_afp_nocredit.jpg


Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya. Karibu watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao.
Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya muda.Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta.
Hii siyo mara ya kwanza wanasayansi wameelezea umuhimu wa Chocolate. Utafiti wa awali umeonyesha Chocolate inasaidia moyo.Baadhi ya chocolate zinasaidia kupunguza msukumo wa damu, kiwango cha sukari mwilini pamoja na mafuta.
Lakini kuna onyo la kuwa makini na Chocolate unayoila kwani baadhi zina sukari na mafuta mengi.Ikiwa unataka kuwa na afya bora, jaribu kula mboga na matunda mengi BBC Swahili - Kwa Kina - Chocolate kukufanya mwembamba
 
....Haya bana MziziMkavu!!! utaacha watu wafakamie :):) chocolate kwa kudhani kwamba watapunguza vitambi vyao. Si unajua tena credibility yako ilivyo juu hapa jamvini.
 
tehe....tehe.....tehee..... nimesoma kutoka kwenye source lakini makosa ya mbadala y w tu yameondoa maana kwenye paragraph ya mwisho. hata hivyo asante kwaushauri
 
....Haya bana MziziMkavu!!! utaacha watu wafakamie :):) chocolate kwa kudhani kwamba watapunguza vitambi vyao. Si unajua tena credibility yako ilivyo juu hapa jamvini.
Nanajuwa lakini kwa mujibu wa watafiti wa Kimarekani Wana Sayansi mimi nimekopi na kuweka hapo sijafanya utafiti lakini Wa Marekani ndio walifanya huo Utafiti na mimi ninamini hivyo mkuu.

Mmh mbona wengine tukifanya diet huwa tunakatazwa tusile chocolate??!!
Poleni sana kwa kukatazwa hivyo mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom