Chinua Achebe akataa kupokea tunzo!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Hii ni mara yake ya pili kufanya hivyo akisema matatizo yale yale yaliomfanya asikubali tuzo hiyo miaka saba iliyopita bado yamesalia.

Chinua Achebe ni mojawapo wa magwiji wa Afrika katika utunzi wa hadithi na riwaya ambaye sifa zake zimeenea duniani kote.Kwa hiyo matamshi yake yana uzito mkubwa. Alipokataa tuzo kuu ya heshima ya kamanda wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria mnamo mwaka 2004 alilalamika kwamba nchi yake inageuzwa kuwa himaya iliyozama katika ufisadi na vurugu.

Akiikataa kwa mara ya pili tuzo hiyo alisema matatizo yale yale bado yapo hayajashughulikiwa seuze kusuluhishwa. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameelezea mshangao na masikitiko yake kwa uamuzi huo. Rais huyo amesema anatumai kwamba Bwana Achebe atapata fursa ya kuizuru Nigeria kutoka Marekani anakoishi na kuona jinsi serikali ya Nigeria inavyozidi kupiga hatua.
 
achebe.jpg
Mwandishi mashuhuri wa riwaya nchini Nigeria,Chinua Achebe amekataa kupokea mojawapo ya tuzo kubwa za heshima za Nigeria.
Hii ni mara yake ya pili kufanya hivyo akisema matatizo yale yale yaliomfanya asikubali tuzo hiyo miaka saba iliyopita bado yamesalia.

Chinua Achebe ni mojawapo wa magwiji wa Afrika katika utunzi wa hadithi na riwaya ambaye sifa zake zimeenea duniani kote.

Kwa hiyo matamshi yake yana uzito mkubwa. Alipokataa tuzo kuu ya heshima ya kamanda wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria mnamo mwaka 2004 alilalamika kwamba nchi yake inageuzwa kuwa himaya iliyozama katika ufisadi na vurugu.

Akiikataa kwa mara ya pili tuzo hiyo alisema matatizo yale yale bado yapo hayajashughulikiwa seuze kusuluhishwa. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameelezea mshangao na masikitiko yake kwa uamuzi huo. Rais huyo amesema anatumai kwamba Bwana Achebe atapata fursa ya kuizuru Nigeria kutoka Marekani anakoishi na kuona jinsi serikali ya Nigeria inavyozidi kupiga hatua.
source-bbcswahili
 
Nigeria na Achebe wao, sisi na akina Kabudi wabwabwajaji, lol, kazi tunayo. Hivi ccm huwa inawanunua kwa shilingi ngapi hata wadhalilishe taaluma zao?
 
Chinua anafikiri katika utendaji wa kazi zake. Prof. Kabudi yeye anaambiwa na wanasiasa afanye nini ili apandishwe cheo au apewe chakula. hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya Chinua na wanaojiita wasomi wa Tanzania ambao hawezi kuishi nje ya mfumo uliooza kama wa Tanzania
 
chinua.jpg

Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, rais Jakaya Kikwete aliwatunukia watu mbali mbali wakiwamo wanaofaa na wasiofaa nishani, nchini Nigeria gwiji wa fasihi Chinua Achebe amekataa nishani kama hiyo.

Wakati kwetu watu wanahoji kwanini kwa mfano Spika wa bunge la sasa Anna Makinda amepewa nishani wakati hafai, nchini Nigeria mambo ni tofauti. Achebe alikataa nishani ya Commander of the Federal Republic award-nishani ya rais, kwa madai kuwa mhusika hajashughulikia mambo muhimu ambayo Achebe ameataka yatekelezwe ambayo ni kupambana na ufisadi, umaskini na vurugu havijashughulikiwa. Achebe alitoa changamoto mwaka 2004 alipokataa nishani kama hii. Je ni nani ana ubavu wa kukataa nishani Tanzania ambapo nishani, shahada za kupewa na kughushi, kujuana katika ulaji na udugu ni madhambi yaliyohalalishwa. Waulize waliotoa na waliopokea nishani kama kuna mwenye udhu na ubavu wa kuhoji kama Achebe. Je Kikwete aliyeingia madarakani kupitia wizi wa EPA na Richmond ana udhu wa kuweza kutoa nishani yenye kuweza kuitwa nishani na kuheshimika? Kama anao basi anaweza kutoa nishani si kwa maana ya nishani bali kituko.

Kwa Achebe kitu muhimu si nishani bali matendo. Kwake rais mharifu ni mharifu sawa na kibaka. Tieni akilini na mtafakuri kwa kina. Je waliopewa nishani wamepewa nishani na mamlaka yenye udhu au wamepewa dharau na aibu? Inashangaza ni kwanini Rostam Aziz na Andrew Chenge hawakupewa nishani hizi zenye maana kinyume na tunavyoelezwa. Aibu ni kwamba marehemu Mwalimu Julius Nyerere amepewa nishani hii chafu na mikono michafu iliyoitoa! Kweli simba akifariki ngozi yake yaweza kugugunwa na panya. Imetokea tena Tanzania.
Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
 
ni lini Malecela amelilia hiyo nishani? au unataka kuvutia wasomaji? si vizuri kupakaziana
 
Kati ya wote waliopewa nishani, Makinda lazima atakuwa aliikimbilia haraka kabla Rais hajabadili mawazo kwani anajua kuwa hakustahili kupewa, kwani hadi sasa alichoifanyia Nchi ni udhaifu wa hali ya juu na uwezo mdogo kwa nafasi nyeti ya uSpika aliyozawadiwa.
 
Back
Top Bottom