Chino alalamika kubaguliwa na Wasanii wenzake

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Msanii anaefanya vizuri kwenye mziki wa Amapiano nchini Chino Kidd, amelalamika kukosa ushirikiano toka kwa wasanii wenzake kwenye Tamasha lake la Wanaman Experience.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Instastory), Chino amesema kuna baadhi ya wasanii wenzake wamemnyima ushirikiano kuelekea Event yake huku akisema kuwa yeye amekuwa ni mtu wa kujitolea sana kwenye mambo ya Wasanii wenzake lakini wao wanashindwa kumsapoti.

Screenshot_20240130-155158.jpg


Written by Mjanja M1
 
Kulalamika lalamika ni weakness.

Fanya wema nenda zako, usingoje shukurani.

Mwanamuziki ukifanya wema kwa wenzako, halafu wao wasikurudishie, hilo ni kosa lako.

Wewe umeshindwa kuwa na ushawishi. Inabidi utafakari, umekosea wapi?

Sasa mwanamuziki ukishindwa kuvutia wanamuziki wenzako wachache tu, mashabiki wengi utaweza kuwavutia?
 
Chino wanamane sio msanii na hana shabiki yoyote. Unawezaje kuandaa show sehemu kama kidimbiw ukitegemea mwanangu mwanangu

Ni kijana aliyetrend kwenye muziki kama kina hamorapa jaiva nk
Hii ni SPANA na Semi umepiga kwenye bajaji si utauua?
 
Huyu dogo anajiona mkubwa kuliko uwezo wake...Huyu na marioo wamakurupa kama malegends vile kumbe bado chipukizi.
Mimi napenda ngoma yake ile aliimba na fid ile sijui anamtaja yesu nyingine nazisikia sikia tu hasa ile intro yake chino wanaman nikiisikia natabasamu.
Mbona mimi namwona ni jamaa mmoja mtaratibu anapenda kusupport wenzake na kurudisha alipotoka.
Sema ngoma zake zinaenda sana hasa kwa mabodaboda siwezi pitapita nisisikie chino wanaman
 
Chino wanamane sio msanii na hana shabiki yoyote. Unawezaje kuandaa show sehemu kama kidimbiw ukitegemea mwanangu mwanangu

Ni kijana aliyetrend kwenye muziki kama kina hamorapa jaiva nk
akipelekwa wasafi hapo kwa mziki wake huo huo wa kitapeli{trends}ataiingizia kampuni pesa kuliko msanii yeyote aliyewahi kusajiliwa hapo ukiondoa harmonize😂😂.
 
Back
Top Bottom