China: Dada mwafrika anyongwa (kosa la kujihusisha na madawa ya kulevya)

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wakati Tanzania tunawabembeleza na kuwakumbatia wale wote wanaojishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya,china watu hao hawadhubutu kuchezea nchi yao,kisa hiki kimemkuta mdada mmoja kutoka Afrika ya kusini

soma zaidi hapa
111212180056_china_execution_304x171_afp_nocredit.jpg


China imempa adhabu ya kifo mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini kwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha dawa za kulevya, ikikataa ombi la Rais Jacob Zuma la kumwachia.
Janice Bronwyn Linden, mwenye umri wa miaka, 38, aliuliwa zaidi ya miaka mitatu baada ya kukamatwa.


Mashirika ya kutetea haki za binadamu tayari yamekuwa yakilaani China mara kwa mara kwa kutekeleza sheria ya hukumu ya kifo, yakisema mfumo wake wa sheria hauna haki.
Serikali ya Afrika Kusini imesema hatua hiyo haitoathiri mahusiano ya karibu ya kidiplomasia na China.
Serikali ya China iliwaruhusu dada zake wawili Bi Linden kukaa naye kwa saa nzima kabla ya kutekeleza hukumu hiyo kwa sindano ya sumu, gazeti binafsi la Afrika Kusini e. News, likimnukuu mwandishi kutoka China.
'Haijashughulikiwa vya kutosha'

Bi Linden alikamatwa Novemba 2008 baada ya kukutwa na kilogramu tatu za methamphetamine alipowasili uwanja wa ndege mjini Guangzhou kusini mwa nchi hiyo.
Aliendelea kutetea nafsi yake, akisema dawa hizo za kulevya zilitumbukizwa kwenye sanduku lake bila yeye kujua.
Hata hivyo, mahakama kuu ya Guangdong na ya rufaa huko Beijing zilikataa rufaa yake.
Msemaji wa idara ya uhusiano wa kimataifa, Clayson Monyela, aliiambia BBC kuwa Bw Zuma aliingilia kati kutaka hukumu hiyo ibadilishwe na apewe kifungo cha maisha.
Bw Monyela alisema, "Tumefanya kila namna kumnusuru hata katika nyanja zote za juu."
Alisema, serikali ya China itakabidhi majivu yake kwa familia yake, kufuatia kuchomwa maiti yake, kulingana na makubaliano yaliyofanywa baina ya mataifa hayo mawili.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa upinzani wa chama cha Democratic Alliance (DA) wa Afrika Kusini, Stevens Mokgalapa, amesema serikali haikufanya vya kutosha kuokoa maisha ya Bi Linden , gazeti binafsi la Afrika kusini Times Lives limeripoti.
 
hivi jamani kwanini wanaharakati wa haki za binadamu hatuwaoni uchina,wao wanang'ang'ania Tanzania tu
 
huyu ndio Zuma alikuwa akimpigia vuvuzela kwa wachina? nafikiri ili kuwe na utii wa sheria hizi sheria kali zikitumika inasaidia
 
Hi nkali tena yawasha lakini nataka niulize yule msanii wet2 watamzania yeye mbona alipenya ktk fagio la chuma au coz watamzania na uchina wanaukaribu sana au urafiki?
 
Hi nkali tena yawasha lakini nataka niulize yule msanii wet2 watamzania yeye mbona alipenya ktk fagio la chuma au coz watamzania na uchina wanaukaribu sana au urafiki?

weeeeeeeeeeee
huyo bana hawakumkuta na hatia,achana na china mkuu,wao wakikukuta na hatia huna la kujitetea hata kama USA uingilie ama wanaojiita haki za binadamu wao hawatambui hilo,

mwambie arudie tena atakiona chamoto
 
huyu ndio Zuma alikuwa akimpigia vuvuzela kwa wachina? nafikiri ili kuwe na utii wa sheria hizi sheria kali zikitumika inasaidia

kwa kweri hizi sheria bana zinasaidia sana tena sana,kwani hawajamaa wana adabu na mali za uma,hata kama rushwa zipo lakini ole wako utiwe mkononi chamoto utakiona
 
Back
Top Bottom