Child abuse/udhalilishaji watoto...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,752
7,846
...wala sishangai... yalishanikuta hayo. Kina mama mjichunge sana hao ma hause girls mnaowafunga ndani, wengine walitu/wanawa-abuse (vitoto vya kiume) na kutuachia psychological scars for life...

Hakuna cha hausigel wala hausboi siku hizi wote ni wabaya tu!
Ilishatokea mtoto wa kiume wa miaka 6 kukutwa na magonjwa ya zinaa.Uchunguzi ukabaini kuwa Hausigel ndiye alimuambukiza mtoto.Mbu unaonaje ukaanzisha thread ya manyayaso ya watoto wa kiume?...
 
...naomba nim quote ndugu yangu Sipo kwenye mada yake hii pia...
Sipo
user_online.gif

icon1.gif
Re: Mashoga nchini Tanzania

Imebidi nirudi kwenye mada hii pamoja na kwamba nilishahitimisha kwa upande wangu lakini nimefanya hivi ili kuweka wazi kile ambacho mwanzoni nilikisema na na wadau wengine pia walikisema. Suala hili lililonihuzunisha ambalo nililolisoma kwenye gazeti la Nipashe la tarehe 6 October, 2009. Suala hili lilihusu houseboy mmoja aliyekuwa anamuingilia/anamlawiti mtoto wa bosi wake wa kiume.

Kwa mujibu wa mwandishi Hamisi Kibari houseboy huyu alikuwa amepewa majukumu ya kumuhudumia mtoto huyu wa bosi wake kwa kumpeleka shule pamoja na kuwa naye nyumbani wakati wazazi wake wakiwa kazini. Pamoja na kazi nyingine kijana huyu alkuwa anamuogesha huyu mtoto. Sasa katika kumuogesha uko akaanza kumfanyia UNYAMA huu wa kutisha sana kwa kumlawiti uku akimtisha huyu mtoto mdogo kwa vitisho vingi. Na kwakuwa muda mrefu huyu houseboy ndie alikuwa anakaa na mtoto huyu mara nyingine wazazi walimkuta mtoto keshalala na wakiulizia maendeleo ya mtoto walikuwa wakiambiwa na houseboy huyu kuwa mtoto yuko okey hana problem. Na ikumbukwe kuwa wazazi wa mtoto huyu walikuwa na imani kubwa sana kwa houseboy huyu kwa kuwa alikuwa ndie anampleka shule na kwenda kumchukua kwenye basi mchana.

Kwahiyo huyu kijana akawa ndie anafanya kazi zote za ndani na ikawa kila siku anamuogesha huyu mtoto kitu ambacho kiliwapa moyo hawa wazazi kuwa kijana huyu anafahamu kazi yake ipasavyo kumbe alikuwa fisi mla watu. Kadri siku zilivyokwenda ndivyo yule mtoto alivyokuwa anaharibikiwa sehemu za nyuma na kuanza kutoa HAJA KUBWA pasipo kujitambua. Huyu houseboy alivyogundua akaanza kumwekea pamba kwenye ****** ili haja kubwa isiwe inaonekana na kuchafua nguo anapokwenda shule na muda anapokuwa na wazazi wake. Just imagine mtoto wako anajazwa MAPAMBA kwenye ****** ili haja kubwa inayotoka bila breki isionekane JESUS CHRIST MY LORD.

Sasa kilichosababisha kugundulika kwa unyama huu ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa ni weekend na huyu kijana alikuwa bado hajamuogesha huyu mvulana na ilibid aende kumpokea mgeni wa bosi wake stendi kabla hajamuogesha huyu mvulana. Hoseboy huyu aligoma kabisa kwenda kumpokea mgeni yule kwa madai kuwa mpaka amuogeshe mtoto yule jambo lilipingwa sana na mabosi wake kwa nguvu zote. Lakini kutokana na kuwa mabosi wana nguvu yule houseboy ilibidi aende shingo upande.

Sasa Mama Mzazi wa yule mtoto alipotaka kumuogesha yule mtoto alikataa katakata hali iliyomshtua Mama mtu na kumuita Baba mtoto (mumewe) ili yeye amuogeshe lakini bado yule mtoto alikataa mpaka alipotishiwa kuchapwa. Sasa kwenda bafuni na kuanza kumuogesha yule mtoto ndipo Baba mtoto alipopata mshtuko wa milele pale alipokuta mwanae amejazwa MAPAMBA matakoni. Na alipodadisi kwa undani ndio akapewa story nzima. Kijana alikamatwa yuko polisi lakini ndio hivyo mtoto keshaharibika kwa kiwango kikubwa.

Lengo langu la kuweka makala hii hapa ni kujaribu kuonyesha yale ambayo niliyasema na pia kusemwa na wadau wa jamvi hapa kuhusu kuharibiwa kwa watoto wetu wa kiume pamoja na wadogo zetu wa kiume jambo ambalo linawapelekea kuwa na tabia za ajabu ikiwa ni pamoja na tabia za kishoga hapo baadae baada ya kuizoea hali hii ya kinyama.

MUNGU ATUSAMEHE NA ZAIDI ATULINDE NA KUWALINDA WATOTO NA WADOGO WETU WA KIKE NA WA KIUME WAKUE CHINI YA ULINZI WAKE WA KIMUNGU. AMEN
 
...na hii pia...

Sipo
user_online.gif

icon1.gif
Re: Mashoga nchini Tanzania

Lakini pia ikumbukwe kuwa si wavulana tu wanahoharibiwa bali pia watoto wa kike nao wamekuwa waathirika wakubwa wa vitendo hivi ambavyo vinafanywa na watu wazima wenye akili ambao ni ndugu wa karibu au wafanyakazi wa ndani wa familia hizi.
Kimsingi ONYO kubwa ni kwetu sis walezi na ndugu ambao tuna wadogo wetu ambao tumejua haya matendo machafu na ya kisodoma na kigomora kuwa makini na malezi ya watoto na wadogo zetu vingnevyo tutakuja kuwa na kizazi cha ajabu sana miaka michache ijayo. Kuna masuala ya muhimu sana ya kufanya kwa mzazi au mlezi yeyote ili kumkinga mtoto wake na mahayawani hawa:-

1. Tuhakikishe kwa watoto wetu hawalali na wageni wanaokuja kututembelea majumbani mwetu kutokana na uhaba wa vyumba.

2. Tuhakikishe kuwa watoto wetu wanapokwenda na kurudi nyumbani kutoka shule tunajaribu kuangalia maendeleo yao kiafya na kielimu pia

3. Tuhakikishe kuwa tunaangaalia marafiki wa watoto wetu tabia zao na za wazazi wao kwani kuna watoto wengine ambao wanaiga tabia chafu kutoka kwa wazazii wao ambao wamepoteza mwelekeo wa maisha kwahiyo wanaweza kuwa wanakuja kujaribu madhambi hayo wakiwa na watoto wetu.

4. Tuhakikishe kuwa kuna uangalizi binafsi wa watoto wetu mbali na ule wanaopewa na ma-housegirl na ma-houseboy kwani kuna wakati sisi wazazi na walezi tunayasahau majukumu yetu kwa hawa wafanyakazi kwa kisingizio cha kazi, harusi, sendoff, kitchen parties na nyingine nyingi.

5. Tuwape watoto wetu muda wa kuongea nao kila jioni na weekends tuache tabia ya kukuta watoto wamelala kila siku na kuridhika na tabia hiyo kwani ina madhara makubwa kama yaliyomkuta mtoto huyu wa kiume.

6. Tuwaombee watoto wetu kwa MUNGU ili awalinde wanapokuwa mashuleni, kwenye vyombo vya usafiri, wakiwa nyumbani na hawa wafanyakzi wa ndani (houseboys na housegirls) kwani kwa akili zetu na nguvu zetu za kimwili pekee hatutaweza jamani.
 
Mbu nashukuru kuwa umeitikia wito na kuanzisha hii mada kuntu.
Unyanyaswaji wa watoto wa kiume umekuwa ni jambo linalofichwa sana.Mara nyingi ukisikia unyanyaswaji basi utasikia ni mtoto wa kike.Hii inatokana na mfumo tuliouzoea kwamba wanaonyanyaswa ni wanawake.Matokeo yake ni kufichaficha vitendo wanavyofanyiwa watoto wa kiume.Hata ile Sheria ya makosa ya kujamiiana ( Sexual Offences Special Provisions Act KWA KIFUPI SOSPA 1998 ilitengenezwa ikimlenga na kumlinda zaidi mtoto wa kike na siyo wa kiume na ndio maana hadi sasa hujasikia mwanamke akifungwa miaka 30 na kuendelea kwa kumnyanyasa kijinsia mtoto wa kiume.Tunajua kuwa sasa hivi ma hausigel wanawanyanyasa sana kijinsia watoto wa kiume.
Binafsi nadhani ni wakati muafaka kuvunja ukimya na kuanza kuongea kwa nguvu zote kuhusu unyanyasaji wa wavulana.Hao serengeti boys tunaosikia wanawake wakiwatokea, wengine hawajafikia hata miaka 18.Iweje basi tunyamazie kero hii?
 
kuna mambo makubwa sna, kiasi kwamba mtu ukiyasikia huwezi amini hadi likutokee kwenye familia yako ndio utaamini kuwa kumbe hili nalo lipo. Tuwe makini jamani
 
Mbu nashukuru kuwa umeitikia wito na kuanzisha hii mada kuntu.
Unyanyaswaji wa watoto wa kiume umekuwa ni jambo linalofichwa sana.Mara nyingi ukisikia unyanyaswaji basi utasikia ni mtoto wa kike.Hii inatokana na mfumo tuliouzoea kwamba wanaonyanyaswa ni wanawake.Matokeo yake ni kufichaficha vitendo wanavyofanyiwa watoto wa kiume.Hata ile Sheria ya makosa ya kujamiiana ( Sexual Offences Special Provisions Act KWA KIFUPI SOSPA 1998 ilitengenezwa ikimlenga na kumlinda zaidi mtoto wa kike na siyo wa kiume na ndio maana hadi sasa hujasikia mwanamke akifungwa miaka 30 na kuendelea kwa kumnyanyasa kijinsia mtoto wa kiume.Tunajua kuwa sasa hivi ma hausigel wanawanyanyasa sana kijinsia watoto wa kiume.
Binafsi nadhani ni wakati muafaka kuvunja ukimya na kuanza kuongea kwa nguvu zote kuhusu unyanyasaji wa wavulana.Hao serengeti boys tunaosikia wanawake wakiwatokea, wengine hawajafikia hata miaka 18.Iweje basi tunyamazie kero hii?

...hivi mtoto wa kiume tuseme wa miaka kati ya 5-9yrs akifanyishwa tendo la ngono na mwanamke wa over 18yrs, kitendo hicho kinaitwa Ubakaji, au udhalilishaji kwa mtoto huyo?
 
...hivi mtoto wa kiume tuseme wa miaka kati ya 5-9yrs akifanyishwa tendo la ngono na mwanamke wa over 18yrs, kitendo hicho kinaitwa Ubakaji, au udhalilishaji kwa mtoto huyo?

Ni udhalilishaji ... ubakaji ni pale kitu kitakapomuingia au kujaribiswha kumuingia mtoto ( intromission/penetration)...
Mwanamke anachofanya ni kulazimisha mtoto kumuingia au yeye kumshikashika n.k.Imewahi kutokea mtoto alipata magonjwa ya zinaa na uchunguzi ukaonyesha kuwa hausgel alikuwa anamwambia mtoto amkojolee haja ndogo sehemu yake ya siri... sasa hapo aliyemuingia mwenziwe ni huyo mtoto wa kiume.
 
Ni udhalilishaji ... ubakaji ni pale kitu kitakapomuingia au kujaribiswha kumuingia mtoto ( intromission/penetration)...

...alaaa! ndio maana inaonekana kosa halina uzito!!!

Mwanamke anachofanya ni kulazimisha mtoto kumuingia au yeye kumshikashika n.k.Imewahi kutokea mtoto alipata magonjwa ya zinaa na uchunguzi ukaonyesha kuwa hausgel alikuwa anamwambia mtoto amkojolee haja ndogo sehemu yake ya siri... sasa hapo aliyemuingia mwenziwe ni huyo mtoto wa kiume.

...pheewww!

unaona sasa! ...hilo ulilosema hapa lishawahi kunitokea!
am scarred for life kila nikifikiria madhara yaliyompata yule dada
kwa kumkojolea mkojo!
 
wazazi wengi wamejenga ikani kubwa kwa wasichana walezi wa watoto wakidhani ati hao wako salama.Wasichojua ni kuwa wanawaharibu watoto kwa kiwango kikubwa mno kuliko hata wale ma hausboy! Nimewahi kuelezwa na mlezi wa shule ya bweni kuhusu kisa cha mtoto wa kiume wa miaka kama 7-8 ambaye kila shule ikifunguliwa, alikuwa anapata kama depression akiulizwa nini kinamsumbua hadi hawezi kuwa makini darasani- jibu lilikuwa " im missing our housegirl"!!
Sasa hebu pateni picha..huyu hausgel alikuwa ameshajenga mahusiano mazito na huyu mtoto, alikuwa analala naye kitanda kimoja na mama aliona ni sawa tu " mwanangu anampenda sana hausgel wetu jamani.Yaani"!..hakuja kuwa yale yalikuwa mapenzi kweli.Ukiangalia umri wa mtoto ni dogo mno kuingia kwenye mapenzi.
 
...Inawezekana pia sio mapenzi kwa maana ya mapenzi, bali ni ile Guilty conscious mtoto anayobakia nayo na kukua nayo.

Katika maisha yangu yote sijapata kumsimulia mtu yeyote yaliyonikumba utotoni. kwanza, kitendo kile nilijua wazazi wakijua ni bakora kwa kwenda mbele...

Pili, nilijua iwapo yule dada ataathirika kwa lolote mimi ndiye mkosa sababu nilimkojolea mkojo! Vile vile kwa wakati ule nilimuonea huruma huenda angetimuliwa kazi, au kuadhibiwa vibaya mno... hivyo kunifanya nimbebee mzigo wake wa dhambi!

Tatu, Japokuwa kitendo hicho kilinitokea nikiwa na miaka mitano tu, bado nakikumbuka mpaka leo (kwa woga ule) na kuna wakati natamani kumhadithia mzazi wangu kilichotokea ingawa na hofu anaweza kupata pigo la moyo kali sana kwa kuteleza kwenye malezi.

Kwenye jukwaa huru hili kidogo naweza kuwa muwazi, lakini kwa kweli najua waathirika wenzangu wanavyojisikia (kifungoni) baada ya kudhalilishwa huko utotoni kwa namna moja au nyingine...

Mtoto wa kike kubakwa, au wa kiume kulawitiwa ni rahisi kidogo kujulikana...lakini kitendo kama nilichotendewa maana yake nilibeba jukumu kuliko umri wangu ulivyokuwa.

Bahati mbaya, vitendo hivi bado vinaendelea,... na wazazi wakiwa wakali ndio kabisaaaa ...wanakosa kujua yanayowaathiri watoto wao.
 
Mbu
Thats a traumatic experience by any standards.
MZAZI YEYOTE ATAUMIZWA SANA kujua kuwa mwanae mpendwa anaishi maisha ya ukimbizi nyumbani kwake!Jamani..ndio maana wakati mwingine watu hutaka akina mama wakae nyumbani walee watoto wao.
 
Daah, haya mambo yanakasirisha na kusikitisha sana.

Kuna kisa kimoja kuhusiana na haya mambo nimeisikiliza HAPA kwenye dullonet.com kwenye hekaheka za Clouds FM ya tarehe 11-11-2009. Inasikitisha.
 
...Inawezekana pia sio mapenzi kwa maana ya mapenzi, bali ni ile Guilty conscious mtoto anayobakia nayo na kukua nayo.

Katika maisha yangu yote sijapata kumsimulia mtu yeyote yaliyonikumba utotoni. kwanza, kitendo kile nilijua wazazi wakijua ni bakora kwa kwenda mbele...

Pili, nilijua iwapo yule dada ataathirika kwa lolote mimi ndiye mkosa sababu nilimkojolea mkojo! Vile vile kwa wakati ule nilimuonea huruma huenda angetimuliwa kazi, au kuadhibiwa vibaya mno... hivyo kunifanya nimbebee mzigo wake wa dhambi!

Tatu, Japokuwa kitendo hicho kilinitokea nikiwa na miaka mitano tu, bado nakikumbuka mpaka leo (kwa woga ule) na kuna wakati natamani kumhadithia mzazi wangu kilichotokea ingawa na hofu anaweza kupata pigo la moyo kali sana kwa kuteleza kwenye malezi.

Kwenye jukwaa huru hili kidogo naweza kuwa muwazi, lakini kwa kweli najua waathirika wenzangu wanavyojisikia (kifungoni) baada ya kudhalilishwa huko utotoni kwa namna moja au nyingine...

Mtoto wa kike kubakwa, au wa kiume kulawitiwa ni rahisi kidogo kujulikana...lakini kitendo kama nilichotendewa maana yake nilibeba jukumu kuliko umri wangu ulivyokuwa.

Bahati mbaya, vitendo hivi bado vinaendelea,... na wazazi wakiwa wakali ndio kabisaaaa ...wanakosa kujua yanayowaathiri watoto wao.

Kumbe tuko wengi wenye shida hii. Mimi nilipokuwa mtoto wa miaka 10 nilikuwa nafanyishwa ngono na mamangu mdogo (tumbo moja na mamangu mzazi), yeye alikuwa na miaka karibu 20 hivi. Na sikuwahi kumwambia mtu yeyote, kwa hofu aliyokuwa ananijengea ya litakalotokea kama hicho kitu kingejulikana.

Lakini hadi leo najiuliza, suppose yule mamdogo angekuwa na ugonjwa wowote, sijui hata kama wazazi wangejua shida ilikotokea. Tatizo ni kwamba, wazazi wawalinde watoto wao dhidi ya nani? Maana hata nduguyo unayemuamini anaweza kumfanyizia mwanao.
 
Daah, Wewe Mtu B umepitia mengi sana maishani.
 
Mtu B ni mtu B kweli..... ina maana uliposema kule kuwa ulikuwa mbaya ni kweli?..
ubaya uliambukizwa na mama mdogo au?
Mimi ndio maana nina wasiwasi na mtu yoyote kujenga mazoea sana na mtoto wangu! SIPENDI KABISA.
 
Jamani sio ma hausigirl tu hata ndugu. hiki kisa kilinitokea mimi mwenyewe nikiwa km 5 yrs, mama yangu alifariki nikiwa 3 yrs old baadaye baba alioa mwanamke mwingine, yule step mother alimchukua mtoto wa dada yake wa kike tulianza ishi naye toka akiwa darasa la tatu, nakumbuka nilikuwa nalala naye kitanda kimoJa ingawa nilikuwa na kaka yangu niliyepishana naye miaka minne alikuwa analala chumba kimoja na houseboy weTu mie nilionekana mdogo so wale dada zangu walionekana kuniangalia. alipofika darasa la tano alikuwa anapenda sana kuniogesha na kuchezea dudu yangu mie sielewi kinachoendelea kumbe mwenzangu mzuka unapanda. usiku tukilala anajidai hebu vua kaptura utakojolea so nalala naked kumbe mwenzangu usiku anachezea nyeti zangu, usiku mmoja naona mzuks ulimpanda mno akaamua kunibaka niliposhtuka akaniaMbia nisiseme ataninunulia biscuti, kweli niliogopa sikujua nini cha kufanya, baba yangu alikuwa mkali sana na kweli sikuweza mwambia mtu, sikuweza mwambia hata My step mom basi ndo ukawa mchezo wake ikifika usiku siku nyingine nashtuka nakuta mkono wangu kwenye kinembe nachezeshwa tu pale. huyu dada alikuwa ananipenda sana tena sana mpaka my step mom akawa anamsifia yule dada. for 3 yrs mpaka akamaliza std seven akaja kwa mama yake dar. kwa kweli hiki kitu hakijafutika akilini mwangu na mtu ambaye nimemwambia ni wife wangu only coz alianza tabia ya kumwamini sana hg wetu nikampa hiyo story, roho ilimuuma sana
 
Mtu B ni mtu B kweli..... ina maana uliposema kule kuwa ulikuwa mbaya ni kweli?..
ubaya uliambukizwa na mama mdogo au?
Mimi ndio maana nina wasiwasi na mtu yoyote kujenga mazoea sana na mtoto wangu! SIPENDI KABISA.

...ha ha ha... VeraCity, unachunga weee lakini mianya ipo mingi wakiamua kuhujumu. La msingi kuwa karibu na mwanao, kuwa muwazi, ikibidi mdadisi... lakini angalia usimtishe!

Chimunguru na Mtu B, poleni sana, ...I empathise with you. Wameshatuwekea doa maishani lisilofutika, ..kila siku ya mungu iendayo unajihisi kama umebebeshwa mzigo fulani...
 
Hakuna cha hausigel wala hausboi siku hizi wote ni wabaya tu!
Ilishatokea mtoto wa kiume wa miaka 6 kukutwa na magonjwa ya zinaa.Uchunguzi ukabaini kuwa Hausigel ndiye alimuambukiza mtoto.Mbu unaonaje ukaanzisha thread ya manyayaso ya watoto wa kiume?...

wajameni hili tatizo ni kubwa kuliko tunavyodani aisee!!! our kids are in avery risky environment. Kuna binamu yangu mtoto wake alikuwa akilambishwa ile kitu akapata very serious infection kwenye mdomo na koo... it took heavy antibiotics na dawa nyingine kumponya maana mwanzo walijua ni toncils

Tatizo ni kwamba ukitaka kuwa na uhakika wa safety ya mtoto, then you need to stay at home
 
...ha ha ha... VeraCity, unachunga weee lakini mianya ipo mingi wakiamua kuhujumu. La msingi kuwa karibu na mwanao, kuwa muwazi, ikibidi mdadisi... lakini angalia usimtishe!

Chimunguru na Mtu B, poleni sana, ...I empathise with you. Wameshatuwekea doa maishani lisilofutika, ..kila siku ya mungu iendayo unajihisi kama umebebeshwa mzigo fulani...

Poleni sana ndugu zanguni - Mtu B, Chamunguru na Mbu....
njia moja ya kufuta hii traumatic experience mioyoni na akilini mwenu ni kuliongelea kama mnavyofanya hapa.Huenda mnahitaji kuongea zaidi na zaidi ili liondoke kwenye system zenu. Inaweza kuwa ni kitu cha zamani sana lakini hakika njia hii inasaidia sana.Mimi binafsi nimewahi kuwa na experiences mbaya japo hazifanani na hizi zenu lakini baada ya kuzungumza nilipata ahueni sana. Hakuna mzigo mzito kama ule ulioubeba moyoni.
 
Back
Top Bottom