Chikawe awakemea Mwakyembe na Sitta: Waache kuzungumzia DOWANS

Ndugu zangu wa JF,

Habari Leo limetoka na habari kuwa waziri wa utawala bora mathias chikawe amepingana na kulaumu kauli za mhe. Sitta na mhe. Dr. Mwakyembe za kutaka serikali isiilipe Dowans kwani ni kampuni ya kitapeli.

Anachosema kina mantiki kwamba wao kama mawaziri wana channels zao za kufikisha uamuzi wowote wanaoupinga ndani ya serikali badala ya kutumia vyombo vya habari.

Binafsi siwalaumu mzee sitta na dr. Mwakyembe kwani pamoja na uelewa wao wa taratibu zinazozungumzwa na chikawe lakini wameshindwa kuvumilia kukaa kimya kutokana na uzalendo kwa nchi yao. Wote wawili wanalifahamu vizuri suala la Dowans na wana uhakika kuwa ni utapeli tena mbaya zaidi unaofanywa na watanzania wenzetu. Suala la Dowans linatia uchungu tena mkubwa sana.

Kwa mtazamo wangu, ni bora viongozi wetu hao (sitta na mwakyembe) ili kulinda heshima yao kwa kujiondoa kwenye serikali inayotetea na kusimamia maamuzi ya kunyonga wananchi wao maskini.

Ndugu yangu, kwa haya tunayoyaona na kuyasikia unadhani Serikali ya Tanzania ya leo ina utaratibu wowote unaofuatwa? Kwa maoni yangu heshima ya Sitta na Mwakyembe itazidi kukua na kulindwa na wananchi endapo wataendelea kuwa kwenye vyeo walivyonavyo na kusaidia kuikosoa Serikali ipasavyo kwa mtindo huo huo wakiwamo ndani ya Serikali kuliko wakiwa nje!
 
.........................Ndugu yangu ukifuatilia utaona kuwa Sitta ni mtu dhaifu katika vikao vya taratibu lakini akiwa mbele ya Umma hujitutumuwa na kutumia uelewa mdopgo wa wananchi. Kama kweli huyu jamaa ni mkweli wa nafsi yake kwanini alikubali kukashifiwa na CCM alipokuwa Spika wa Bunge walipotaka kumuondowa uanachama? Umefika wakati kumwangalia Sitta vitendo vyake na sio matamshi yake!

Mkuu Ngekewa.............unaingia ktk mtego ule ule uliomnasa Chikawe...........unataka kutuambia nini hapo juu in relation na issue at hand?................wengi tunajua udhaifu wa Sitta......lakini udhaifu wake hauondoi common sense (akili) aliyonayo..............WIZI NI WIZI TU aseme Sitta aseme Chikawe utabakia kuwa ni WIZI.............
 
Chikawe wewe ni mtu mzima na tunakuheshimu, lakini kama unataka kuwa kama Mzee Makamba, BASI JARIBU Kutetea Ufisadi Uone
 
Kwa bahati mbaya hawakulazimishwa na walikuwa na bado wanahaki ya kukataa nafasi zile. Hizi kauli zao zinatofauti gani na wafanyakazi wanaomwibia mwajiri wao? Au marketing officer anayachafua bidhaa za kampuni aliyoajiriwa. Upuuzi wa namna hii haupo. Hapa ninasisitiza aidha watoke serikalini au wafunge midomo yao.

Mimi nafikiri kuna maadili ya kazi.
Sitta na Mwakyembe wamepewa job descriptions wanachapa kazi yao katika wizara zao lakini ya weizara nyingine wao ni sawa na watazamaji raia so wana haki ya protest popote kutokana na utashi wa taaluma yao.
Na kama kweli wamekiuka maadili ya kazi na kupelekea kumuudhi mkulu wao nadhani mkulu awafukuze kazi kama kweli wanaongea uongo na sheria haziwaruhusu.
 
Back
Top Bottom