Chifu Usoro ajichimbia kaburi na kusherehekea mazishi yake kabla ya kifo chake

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,929
6,740
Katika kile wengi wanaweza kuelezea kama jambo lisilokuwa la kawaida, mwanamume Mnigeria Clement Usoro, ameipa maisha na kifo taswira mpya baada ya kujijengea kaburi na hata kusherehekea hafla hiyo kabla ya kuondoka kwake.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, katika mahojiano na BBC Pidgin, alisema alifanya maandalizi muhimu ya mazishi yake miaka mitatu iliyopita wakati akitimiza umri wa miaka 70. alisema tayari ameandika wosia. Hata hivyo, Usoro, alisema anaendelea kuusahisha kila wakati.

"Nimeandika wosia wangu na nitaendelea kuusahisha kulingana na muda.Nimejenga kaburi langu. Ni kaburi lenye futi 9 kwa 9. Pia nimejenga mnara kando yake. "Rafiki yangu alikwenda nami katika duka la jeneza kuona lenye nitapenda.Aliamua kuninunulia. Kama chifu, kuna mambo unatakiwa kufanya kabla ya kufa ama wafanye baada yako," alisema Usoro.

Chifu Usoro pia alifichua kuwa amelipia vitu muhimu vya ibada kwa machifu wake wasaidizi akitoa ng'ombe ili kuwazuia wanawe kuwa na wasiwasi baada ya kifo chake. Aliongezea kuwa hataki familia yake kuandaa hafla ya mazishi baada ya kifo chake akidai kuwa kusherehekea kifo chake ni kupoteza muda na pesa. Mzee huyo pia alisema aliwaagiza watoto wake kumzika siku tatu baada ya kifo chake.

85.jpg
 
Back
Top Bottom