Chenge outshines Werema

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,067
Chenge amekuwa ana chip in mara kwa mara katika mijadala hot na mara nyingi akiikosoa na kusahihisha hata lugha.
Werema anatakiwa ajitahidi sana kwani naona kila mara anakuwa kama mtu mwenye hasira.
 
Werema alifanyafanyaje mpaka kapata u AG?

Ana-reflect aina ya wataalamu wetu tulionao katika mhimili ule wa kutafsiri Katiba na sheria zetu na hatimaye kutoa hukumu. Huyu Bwana alikuwa, na, ni Jaji wa mahakama kuu ya JMT! Nikimkumbuka yule jaji wa Arusha na wengineo kadhaa waliowahi kuhukumu kesi kiutata ukichanganya na huyu Mwanasheria Mkuu kweli nchi yetu ina safari ndefu mno!

Sikatati hakuna binadamu aliye mweledi wa kila kitu lakini inapotokea "gwiji" kama Werema always hatoi maelezo yaliyonyooka katika fani yake inanipa shida sana. Haongei sentensi tatu bila kuchemsha, na huyo ndio mshauri mkuu wa serikali kisheria - kazi ipo.

Naanza kuamini wanopigania kuwa na mahakama zao kwa ajili ya masuala yao wana hoja. Kama mahakama yetu kuu inaweza kuwa na majaji dizaini hii sijui zile za mwanzo kukoje jamani! Tuna tatizo kubwa sana na mifumo yetu mingi ukiwapo wa sheria.
 
chenge ni mkali sana.sema ufisadi tu ndio unaomwangusha.kama umesoma LL.B UTAMKUBALI SANA.HAVARD SIO MCHEZO KAKA.

Nasikia Bachelors yake alisomea Harvard. Lakini bahati mbaya sana, kama yanenavyo maandiko, rushwa hupofusha hata mtu kusahau fani na wajibu wake.
 
Pamoja na Chenge kuwa mkali wa sheria, lakini kwa issue ya Werema kum-outsmart wala hata haihitaji nguvu nyingi! ameonesha kupwaya katika nafasi ya AG!
 
wakati wa chenge tumeshuhudia nchi ikiingizwa mkenge wa mikataba mibovu!
Mimi nawaona wote ni wale wale tu yaani ni kama kutoa nafuhu na kuingiza afadhali.
 
ndiyo madhara ya katiba yetu kwa nin spka achaguliwe na wabunge halafu mhimili mwingine achagua mtu mmoja kwa manufaa yake, akili ku nywele
 
Andrew Chenge ...pamoja na kukabiliwa na kashfa mbili tatu......ni mwanasheria competent na mwenye akili sana...hata ukiongea na wanasheria ..wanakubaliana na Hilo .....ni graduate wa prestigious Harvard law school...

Unapoongelea wanasheria waliopita Kama wanasheria wakuu ...ambao Angalau Walihimili changamoto za pale ni Mark BOmani, Joseph Warioba, Damian Lubuva na Andew Chenge. Angalieni namna Huyu wa sasa Werema na Yule aliyemtangualia Mwanyika wanavyopelekeshwa bungeni.........
 
Nasikia Bachelors yake alisomea Harvard. Lakini bahati mbaya sana, kama yanenavyo maandiko, rushwa hupofusha hata mtu kusahau fani na wajibu wake.

KUSOMA NI SWALA MOJA NA UADILIFU NI SWALA LINGINE. CHENGE KINACHOMGALIMU NI KUTOKWA MWADILIFU HIVYO ANATUMIA ELIMU YAKE ya HARVARD KUIBA NA KUHAKIKISHA KUWA HAKUNA USHAHIDI WA KUMTIA HATIANI. SHERIA NAIITUMIA ANAVYOTAKA
 
Chenge amekuwa ana chip in mara kwa mara katika mijadala hot na mara nyingi akiikosoa na kusahihisha hata lugha.
Werema anatakiwa ajitahidi sana kwani naona kila mara anakuwa kama mtu mwenye hasira.

Ushauri wangu ni kwamba, Chenge anapashwa kumsaidia Werema kwa kwenda kuzungumza naye au kumpa karatasi kuliko kunyanyuka na kuanza kutoa ufafanuzi wa kumfanya Werema aonekane anapwaya vile - hiyo aipendezi hata kidogo.
 
Chenge aligundua mapema kuwa pamoja na kusoma sana na kusugua kipara chake pale harvard, angeweza kufa masikini ndo maana aliposoma alama za nyakati akaamua kuchukiua chake mapema.
Nchi yetu haihitaji uadilifu maana utakuta mwadilifu mmoja ila waliokuzunguka wote wanaiba sasa ina maana gani?
Mwacheni ale vijisenti naamini hata sisi tungepata hiyo nafasi wala tusingechelewa kubeba mapesa.

Tunaolalamika ni wale tusio na uwezo wa kula hela za serikali, ila tukipata hiyo nafasi hamtatusikia tukilalamika.
 
Back
Top Bottom