Chenge asimikwa mtemi wa wasukuma

This is non-public-issue. Nchi hii haina viongozi wa kikabila rasmi (yaani hawatambuliwi kikatiba). Kwa hiyo ni sawa tu kiongozi wa familia fulani akaombwa pia aongoze na familia zingine.
Naona ni kutapatapa kwa Chenge mwemyewe.
 
Wakati wamasai wanamkimbiza lowasa...wasukuma wanampa cheo cha kimila...fisadi haha labda ameununua kujikinga na mashambulizi......ila siku zao zinahesabika........
 
JE,Huu utemi unaweza kufafaninishwa na u chifu wa kinaijeria ambao hununuliwa... au ku lobby kwa bidii sana maana mwisho wa siku huo u chifu ni daraja kwa mambo mengi - kisiasa, kiuchumi na hata kijamii?
Kama yeye anaweza kuwa Mtemi na kuna wengine kama kina Jaji Bomani na Jaji Mihayo na wengine..kwanini jamii hiyo isingewapatia hao ambao hawajachafuka mbele ya umma wa Watanzania? Au wanataka kutuma ujumbe gani?
 
Nadhani kwa wanakijiji wengi wa Tanzania hawapati habari za kina kwa mambo yanavyo endelea katika nchi yao. Kuna maeneo ambaya magazeti hayafiki, redio ni tatizo. Sina hakika kama ndugu zangu kina ''ngosha'' walikuwa na taarifa za ufisadi za bwana chenge? Na kama walikuwa nazo inawezekana Chenge aliamua kumwaga vijisenti ili aweze kufanikisha sherehe hiyo.

Je mnakumbuka hata bwana Lowasa alifanyiwa hivyo hivyo baada ya kashfa ya Richmond.
 
Anatupa aibu sana wasukuma......Masanja, Sikonge mko wapi?

Ha!ha!ha!ha! bro Masa...hakianani mna kazi kweli kweli!

But I think with respect to umasikini ambao wananchi wetu huko vijijini wanao, na ukilinganisha na utajiri aliojichumia sitashangaa kuweza kumudu kununu utemi huo.....hope kutakuwa na two or five guys tu wanaopitisha maamuzi hayo sidhani kama kuna democracy katika uteuzi huo!
 
Back
Top Bottom