Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,632
- 4,378
Baada ya kufuatilia kwa karibu ajali zinazotokea mara kwa mara hasa zinazohusisha magari makubwa nimegundua kuwa, zaidi ya nusu zimesababishwa na overtaking (kupita gari la mbele bila kuchukua tahadhari. Mara nyingi mwendokasi umeweza kusababisha ajali pale dereva anapoacha kufuata taratibu na sheria za barabarani ikiwemo hiyo ya overtaking
Hivyo basi, nashauri kuwepo na kampeni ya kukumbusha madereva uhatari wa overtaking na wapi hawatakiwi kabisa kufanya hivyo au niseme kuovertake kwa kupiga ramli
Mimi napenda kukumbusha yafuatayo;
Hivyo basi, nashauri kuwepo na kampeni ya kukumbusha madereva uhatari wa overtaking na wapi hawatakiwi kabisa kufanya hivyo au niseme kuovertake kwa kupiga ramli
Mimi napenda kukumbusha yafuatayo;
- Usi overtake kwenye kona kwani huwezi kujua kama kuna gari nyingine
- Usioveratake kwenye bonde kwani huwezi kujua nini unaweza kukutana nacho (gari/ Wanyama nk)
- Usiovertake kama gari la mbele limepunguza mwendo au kusimama kabla ya kujua kwa nini lipepunza
- Usiovertake kama gari lako halina nguvu ya kupita gari lililo mbele yako kwa haraka (mf malori mengi yana hii changamoto)
- Usiovertake kwa kufuata mkumbo au kufuta gari la mbele yako bila kujihakikishia usalama wako kwani yaweza kuwa mwenzako amejipimia umbali wake anaoweza kumaliza
- Usioveratke sehemu iliyokatanzwa hasa kama haujui kwa nini imekatazwa
- Usiovertake kama uko karibu na njia ya mchepuko au kusimama au kushusha abiria
- Usiovertake kwenye vivuko vya miguu/ bumps
- Usiovertake kwenye daraja
- Usiovertake kwenye Barabara nyembamba za nje yamji