Chanzo cha vita ya Israel na Palestina na ni nani mmiliki halali wa eneo hilo

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,047
Hakuna mji wowote duniani ambao umekuwa ni mji wenye umuhimu sana kwa watu wengi kama ulivyo mji wa Jerusalem. Mji wa Jerusalem ni mji ambao una umuhimu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Mji wa Jerusalem unajulikana kama mji wa amani lakini Jerusalem ya leo n ahata kihistoria haujawahi kuwa mji wa amani bali migogoro.

Umewahi kuharibiwa X2, na kugombewa X16, kuzingirwa na majeshi X23, matukio ya kushambuliwa X52 na kuthibitiwa na tawala mbalimbali mara kadhaa. Jerusalem imewatenganisha wat una pia kuwaunganisha kutokana na kuwa na Imani mmoja kuwa ni mji wao mtakatifu.

Ni jambo gani linaoufanya mji wa Jerusalem kuwa Maalum lakini wenye vimbwanga?

Hebu turudi mamia ya miaka nyuma.

Mji wa Jerusalem ni mji wa kale sana ukiwa na umri wa miaka 4440 au Zaidi. Kwa Zaidi ya karne 3 ya uwepo wa mji huu, madhehebu matatu yamepigana sana ili kuudhibiti; Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Haya madhehebu matatu yote yanachimbuko kutoka kwa Nabii Abraham/Ibrahim kwakuwa haya madhehebu yote matatu yanamchukulia Abraham kama baba wao wa Imani. Vitabu vyote vya madhehebu haya yani, Tora, Biblia na Quran, vinamtaja Abraham.

Wayahudi na Wakristo wao wanadai chimbuko lao ni mtoto wa pili wa Abraham, Isack. Waislamu wanadai chimbuko lao linatoka kwa mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael. Hii imani ya chimbuko imechangia sana katika kuleta utengano baina yao, japo Jerusalem umekuwa ni mji ambao wote wanauamini kama mji mtakatifu.

Katika lugha ya Kibrania, Jerusalem unajulikana kama Yerushalayim, mji mtakatifu wa Wayahudi. Sinagogi la kwenye mlima wa Jerusalem ni eneo ambalo nyumba mbili za ibada zilizotumiwa na Wayahudi zilikuwepo kwa maelfu ya miaka.

Kwenye ukuta wa Magharibi wa sinagogi na mlima inasemekana ndilo eneo lenye mabaki ya mwisho ya nyumba hizo za ibada. Leo hii eneo hili linachukuliwa kuwa ndilo eneo takatifu Zaidi katika imani ya Kiyahudi.

Wayahudi wanaposali huelekea kwenye ukuta wa Magharibi wa Jerusalem kama ambavyo Waislamu huelekea Kaaba, Makka.

Jerusalem pia ni eneo takatifu kwa Waislamu ambapo kwa lugha ya Kiarabu inajulikana kama Al-Quds, ikiwa na maana ya eneo takatifu. Hili ndio eneo ulipo msikiti wa Al-Aqsa ambapo ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Makka na Medina.

Juu ya Sinagogi la mlimani kuna Kuba ya mwamba (Dome of the Rock). Hili ndilo eneo ambapo Waislamu wanaamini kuwa Mtume Mohammed S.W alipaa kwenda mbinguni.

Kwa Wakristo, Jerusalem ilitajwa kama Salem kwenye Biblia. Hili ni jina la kale la Kiebrania ambalo limehifadhiwa kwenye jina la sasa, Jeru-Salem. Mji huu ndipo lilipo kanisa la Kaburi Takatifu (Holy Sepulchre) ambapo yesu ndipo alisulubishwa, akazikwa na kufufuka.

Hivyo utaona kwamba Jerusalem ni sehemu muhimu katika imani ya madhehebu haya matatu.

Lakini ni nani mmiliki halali wa eneo hili?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja kwa swali hili.

Ila, Jerusalem ni mji wa wote na hakuna mwenye hati miliki yam ji huu. Kila dhehebu limeudhibiti mji huu, na karibia kila dola iliyowahi kuwa na ngumu imewahi kuishikilia na kuithibiti Jerusalem.

Lakini kwa Kauli maarufu kutoka kwa Winston Churchill aliwahi kusema, “Inabidi Wayahudi waachiwe Mji wa Jerusalem; wao ndio walioufanya ukawa maarufu.” – You ought to let the Jews have Jerusalem; it is they who made it famous.

Ni kwa namna gani Wayahudi waliifanya Jerusalem ikawa mashuhuri?

Hebu turudi nyuma tena katika historia.

Mwaka 135 CE ambapo Warumi waliwaondoa Wayahudi katika mji wa Jerusalem na kubadili jina kutoka Yudea (Judea) kuwa Palaestina. Hili ni jina la Kigiriki lililolenga kuondoa muungano wowote walionao Wayahdi kwenye eneo hilo. Wayahudi wote walipigwa marufuku kukanyaga Jerusalem.

Baada ya kuondolewa Yudea, Wayahudi walisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa chini ya utawala wa Kirumi, Ulaya ya leo. Lakini walishambuliwa kila sehemu walipoenda.

Katika karne ya 11, Wayahudi waliuawa na wapigania Kristo (Crusaders) kwa kigezo kwamba wao ndio walimuua Yesu. Kwenye karne ya 14, Wayahudi waliuawa kwa madai kwamba wao ndio chanzo cha vifo vinavyojulikana kama black death. Walituhumiwa kwa kubadili mahubiri ya Yesu na kushambilia majeshi ya Warumi.

Wayahudi waliendelea kushambuliwa mpaka karne ya 19 ambapo baadhi ya Wahudi waliunganisha nguvu ili kulinda chimbuko lao. Walianzisha kitu kinachojulikana kama Zionism. Hii ilikuwa itikadi ya kisiasa, na kidini ambayo ililenga mambo mawili.

  • Ililenga kuzuia Wayahudi kushambuliwa
  • Ililenga kuwarudisha Wayahudi Jerusalem
Wazionist waliamini kwamba Uyahudi sio tu kwamba ni dhehebu, bali ni utaifa. Walidai kwamba Wayahudi hawanabudi kuwa na taifa kama ilivyo kwa Wafaransa walivyo na taifa la Ufaransa. Harakati hizi ndizo ziliwarudisha Israel. Leo hii itikadi ya Zionism ni itikadi ya taifa la Israel.

Kufikia mwisho wa karne ya 19, harakati hizi zilisababisha Wayahudi wengi kwa makundi kuhamia Palestina. Kufikia mwaka 1903, kiasi cha Wayahudi 30,000 walikuwa tayari wameweka makazi yao Palestina. Kufikia mwaka 1914, kulikuwa kuna ongezeko la Wayahudi wengine 40,000.

Hapa sasa ndipo Vita ya kwanza ya dunia ikaanza. Dola ya Ottoman ikaanguka, huku Waingereza na Wafaransa wakiyatawala makoloni ya Asia. Palestina ikawa chini ya Waingereza.

Mwanzoni, Waingereza waliruhusu Wayahudi kuendelea kuhamia Palestina. Lakini, kadri Wayahudi walivyoongezeka mvutano baina ya Waarabu na Wayahudi nao ukaongezeka. Pande zote zilishambuliana huku kila upande ukidai unaonewa. Hivyo, kufikia mwaka 1930, Waingereza walianza kudhibiti Wayahudi kuhamia Palestina.

Kuibuka kwa Nazi – Ujerumani

Mambo yalibadilika tena baada ya kuibuka kwa itikadi ya Nazi. Inakadiliwa kwamba Wayahudi milioni 6 waliuawa. Waliosalia walikimbilia Marekani na Palestina kwa idadi kubwa. Kufikia mwaka 1944, idadi ya Wayahudi wanaoishi Palestina ilifika 33% ya wakazi wote. Hii ilisababisha nchi za magharibi kuanza kuunga mkono kuundwa kwa taifa la Wayahudi. Lakini nchi nyingi za Kiarabu hazikutaka jambo hili litokee.

Mwaka 1947, uadui baina ya Wayahudi na Waarabu uliongezeka. Umoja wa Mataifa ulipitisha mpango wa kuigawa Palestina katika nchi mbili. Moja iwe ya Wayahdi na iitwe Israel na nyingine ibaki kwa ajili ya Waarabu, Palestina. Ambapo Israel iwe na ukubwa wa 56.5% la eneo lote huku Palestina ikibaki na 43.5% ya eneo.

Katiak azimio hilo, mji wa Jerusalem ulipaswa kubaki kuwa eneo la kimataifa kwa kuwa madhehebu yote yanalichukulia kama eneo takatifu. Mpango huu ulishindwa kabisa kufanikiwa.

Waingereza walishindwa kuzuia machafuko, hivyo kujiondoa kabisa na kuwaachia wahusika wadundane wenyewe. Wao waliondoka wakiacha machafuko nyuma. Wayahudi wao walikubaliana na mpango wa Umoja wa Mataifa.

Tarehe 14 Mei, 1948 Wayahudi walidai uhuru wa taifa lao na kuunda taifa lao la Israel. Wapalestina waliona jamb hili ni wizi, na Wayahudi wamewaibia eneo lao. Basi kilichofuata ni migogoro na uadui baina ya Wayahudi na waarabu.

Kwa Zaidi ya miaka 70, wamepigana zidi ya vita 8 zilizo rasmi huku mashambulizi madogo madogo ambayo hayana idadi.

Katika vita hizi na migogoro hizi, Israel aliendelea kujinyakulia maeneo ya Palestina.

Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1947.

before.JPG




Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1948, baada ya vita ya Israel dhidi ya Waarabu

baada 2.JPG




Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1967, baada ya vita ya siku 6.

Baada 3.JPG




Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 2020.

baada 4.JPG




Katika ramani ya mwisho eneo la mashariki la Jerusalem liko chini ya udhibiti wa Israel, huku maeneo ya Palestina yakiwa ni makazi madogo madogo tu.

Mwaka 2021, mapigano baina ya Israel na Palestina yaliibuka tena ambapo mji wa Jerusalem ulishambuliwa sana. Haya ndio yalikuwa mapigano makali toka mapigano yam waka 2014. Nini kilipelekea mapigano haya?

Kama kawaida ni kipande cha ardhi.

Hii ilitoka na Wayahudi kutaka kuchukua eneo la makazi ya Wapalestina lijulikanalo kama Sheikh Jarrah liliko Mashariki mwa Jerusalem.

Na hili ni tukio la Kihistoria pia. Baada ya Israel kuyashikilia maeneo yanayozunguka Sheikh Jarrah, wakulima wa Kiyahudi walifungua kesi za madai wakidai maeneo hayo yalikuwa ya kwao. Walidai kwamba haya maeneo waliyaopteza wakati wa vita yam waka 1948. Israel ilipitisha sheria ya kukubaliana na madai hayo na kubariki uvamizi wa maeneo hayo, pale tu ambapo wadai wangedhibitisha umiliki wa maeneo hayo.

Jambo hili lilisababisha familia nyingi za Kipalestina kuondolewa katika makazi haya. Lakini hata kabla ya Wayahudi kutoa Ushahidi walianza kuvamia maeneo hayo.

Video moja ilisambaa Myahudi mmoja akiwa amevamia shamba na nyumba ya familia ya Kipalestina akitaka waondoke. Mama akawa anamwambia kuwa eneo lake kwanini anataka kuliiba. Myahudi akamjibu, nisipoliiba mimi atakuja Myahudi mwingine aliibe.

Jambo hili lililea hasira sana kwa Wapalestina na Hamas wakaanzisha mashambulizi ya rocket za kurusha yakaanza. Israel ikajibu mashambulizi na mapigano makubwa yakatokea.

Je, ni nini kinaweza kuleta amani baina ya Wayahudi na Wapalestina?

Je, ni nani ana haki ya eneo hilo na ni kwanini washindwe kuishi Pamoja?

Makala hii nimeandika kwa msaada wa Gravitas kutoka kwa mwadada machachari Palki.
 
Mtume alikuwa anaeneza dini kwa kuvamia usipokubali kuwa mwslam anakukata kichwa
Ile syria,iraq,uturuk ni nchi ya wayahudi

Wapalestina waache fujo
Almost dini nyingi zimefanya haya, soma historia ya kanisa katoliki jinsi watu walivyouawa kwa misingi ya imani. Sema historia hii uwa haisemwi sana.
 
Almost dini nyingi zimefanya haya, soma historia ya kanisa katoliki jinsi watu walivyouawa kwa misingi ya imani. Sema historia hii uwa haisemwi sana.
Amesahau wale waliokuwa wakijiita crusaders, anakumbuka waislamu tu.
 
Back
Top Bottom