Chanzo cha mauaji ya mfanyabiashara ni hela

Polisi imeingilia kati ili ripoti isitoke...up todate sasa hv marehemu ndo anazikwa
 
Kwa karne hii hufai kufanya hivyo hata kama una hela zimejaa dunia nzima, sehemu ya kutunzia zipo zimejaa tele kwa nini ku - risk?
Ya nini na kwa mahitaji gani uweke 300 ml home?

Mkuu nadhani hujamwelewa jamaa anasema na nature ya business mie binafsi hii biashara ya madini nimeifanya mzigo unachimbwa ndani ndani huko...

Lets say maganzo ndani ndano huko au igombe (tabora) access za kibenki bado sana mtu kuwa na pesa kama hii sio inshu ni jambo la kawaida sana kwa wafanyabiashaa wa madini...

Ni kama baadhi ya watu kuwa na laki nane nyumbani sio issue...
 
Mm naona uwekaji wa hela nyumbani kiasi kikubwa km 50,000,000.00 ni kutokuwa na akili kwani hakuna utajiri wa kijinga km huo, hivi kwanini usiwekeze katika Ardhi au Majengo?
Mmeshuhudia Zombe akizibeba fedha hizo hivihivi na Kesi kushinda
Wewe unakuwa una milioni 100 na mkeo anajua, kwnini tusiamini huo ni mchoro wa Wanafamilia kuwatonya POLISI kuwa hapa pana Mzigo. Kawaida ya matajiri wa namna hii humalizwa na vimada au nyumba ndogo, huwezi sikia Bakharesa, Mengi, Uhuru Kenyata au Odinga eti kaficha hela uvunguni au kwenye Heater
Kwa vile hii story haijaifikia vyombo vya Habari hata Blogu bado naamini huyu jamaa ana ugomvi na POLISI na km alivyoeleza ngonani humu JF

Nani alikuwa na marehemu kabla hajauwawa ambaye wali hesabu wote zile hela?acheni ushabiki wa ajabu ajabu,marehemu alimjeruhi polisi kituoni kwa hasira za gari lake kukamatwa,kisha akaimbilia kwake,alikuwa amelewa na confused,akaenda kwa jirani akakwapua combat,alipoona nyumba imezingirwa akajipiga risasi tumboni,mkewe aliruka na kumkumbatia akimbembeleza asijue,yeye aakmuamrisha mkewe aondoke mara moja ama sivyo atamuuwa,kitendo cha mkewe kumpa nafasi akajiongeza ya pili usoni.Suala la risasi mbili au tatu mwilini sio issue,inategemea amejipiga wapi.Kama angekuwa na matundu mawili ya risasi kichwani then hio ni habari nyingine,lakini tumboni alafu kichwani ni kitu cha kawaida.Mimi sitetei polisi ila tu nawashangaa mnajadili sana bila kuulizia maendeleo ya askari aliyepigwa risasi kadhaa na marehemu,bila shaka angeuwawa polisi mgesema ni sawa
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na aina ya biashara aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu hapo. Wafanyabiashara wengi wa madini huwa wanakuwa na pesa Kama hizo au zaidi nje ya mabenki. Ukiletewa mzigo usiku wa milioni 20 utafanyaje na huku mabenki yanakuwa yamefungwa. Mara nyingi hao wauzaji wadogo wadogo wanataka hela hapo hapo hamna habari ya njoo kesho uchukue hela.

Hamna cha ajabu kwa mfanyabiashara wa aina hiyo kuwa na kiasi Kama hicho nyumbani kwake au ofisini. Benki ni wasumbufu sana haswa mikoani...kuna watu wananielewa namaanisha nini hapa
.
Mkuu nimekusoma sawia, ila inahitaji uwe umeshapitia hizi biashara ndio ujue. Unaletewa jiwe watu wanataka kwenda "kuweka heshima bar" au kwa kina joyce, huna cash anauziwa tajiri mwingine. Na pengine ni jiwe lenye sifa!!

Back to the point, inanitatiza sana kuona polisi wanakuwa sehemu ya ujambazi katika matukio mengi. Nowdays there is a thin line between police and majambazi. Hizi ni dalili tu za ugonjwa lakini kuna ugonjwa mkubwa sehemu na unastahili kutibiwa wa haraka kabla hatujachelewa
 
kwa hivo sasa imefikia hatua polisi wanaua raia ili kuchukua hela zao kwa mgongo wa RPC,,
dah wananchi na wafiwa msikubali.
lazima kieleweka hela zirudi na waliohusika wachukuliwe hatua kali.
nadhani RPC anajua hili sasa tuone atachukua hatua gani
la sivo polisi wake hawatakuwa salama huko walipo
 
swala la kuweka hela ndani halina uwingi wala uchache hao polisi hata wangekuta milioni ishirini wangeua!
 
Huu Kama sio UJAMBAZI ni nini ndugu zangu????

"POLISI wa Mkoa wa Geita wametumia nguvu kuzuia msafara wa waombolezaji waliokuwa na mwili wa marehemu mfanyabiashara, Yemuga Fungungu (48), mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vurugu kubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikuwapo wakati askari wake walipoingilia msafara huo na kusababisha vurumai kubwa.
Waombolezaji hao walikuwa wakiuhamisha mwili wa marehemu Fungungu kutoka Hospitali ya Runzewa kuupeleka katika Hospitali ya Geita.

Sakata hilo la ndugu na polisi lililotokea saa nane mchana juzi Jumamosi katika Pori la Samina, Geita na polisi wakiwa kwenye magari matatu wakiwa wamesheheni silaha mbalimbali walifika na kuzuia mwili wa marehemu kusafirishwa.

Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwamo mkewe, wanadai kwamba Fungungu alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi wanaosemekana kwamba walimvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita kisha kupora mamilioni ya fedha. Wanadai kwamba alipigwa risasi tumboni na kichwani katika Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe mkoani hapa.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa kiasi cha Sh360 milioni kiliporwa. Kati ya fedha hizo, Sh60 milioni zinadaiwa kwamba zilikuwa kwenye gari wakati Sh300 milioni zilikuwa kwenye masanduku mawili yaliyokuwa ndani ya nyumba.

Pia ndugu hao walidai kwamba Sh1.2 milioni zilichukuliwa na askari wawili wa kiume baada ya kumpekua mke wa marehemu kwenye nguo za ndani.

Pia askari hao wanadaiwa kupora mali mbalimbali za marehemu zikiwamo redio mbili, video kamera moja, nguo za marehemu ikiwamo kanzu, mashine ya printer, mashine ya inventor, karatasi za picha, deki mbili za kucheza CD, pamoja na nguo za mke wa marehemu.

Mapema Kamanda Paulo alikuwa ameeleza kuwa marehemu alijiua mwenyewe baada ya kumjeruhi Polisi, Fortunatus Beatus kwa risasi lakini taarifa hizo zimepingwa vikali na ndugu na jamaa wa marehemu ambao wanadai marehemu aliuawa na polisi akiwa nyumbani kwake.

Polisi kuzuia waombolezaji

Baada ya polisi kuyasimamisha magari manane yaliyokuwa katika msafara huo wa kupeleka mwili wa marehemu kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Geita, kulizuka mabishano makali kati ya Kamanda Paulo na ndugu wa marehemu.

Inadaiwa kwamba polisi walikuwa wakishinikiza mwili huo urejeshwe Runzewe, Bukombe kwa kuwa tayari ulikuwa umefanyiwa uchunguzi jambo ambalo liliwakera waombolezaji hao.

Kabla ya kamanda huyo kufika eneo hilo, msafara huo ulisimamishwa na Polisi wa Usalama Barabarani ambao walikuwa wamefuatana na wale wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita, Leonard Makona.
Baada ya kuusimamisha msafara huo, Makona aliwataka ndugu wa marehemu kumsubiri Kamanda Paulo ambaye alifika baada ya takriban dakika 10.

Mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alishuhudia ndugu wa marehemu na Kamanda Paulo wakirushiana maneno.

“Mnapeleka wapi mwili wa marehemu, ina maana hamkuridhika na uchunguzi wa daktari wa Bukombe?” alihoji kwa ukali na kujibiwa pia kwa ukali na kaka wa marehemu, Mariatabu Fungungu: “Kwa nini mnatusimamisha? Tunaomba tuite waandishi wa habari hapa ili waje washuhudie tukio hili. Kwa nini msikae ofisini?”

Baadaye, kamanda huyo aliwaamuru askari wake kuwaingiza katika gari la polisi ndugu watano wa marehemu wakiwamo mke wa marehemu, Lucia Kilaza (23) na Mariatabu. Walifanya hivyo kwa kutumia nguvu na kisha kuondoka nao hadi katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita.

Ndugu wa marehemu walilalamikia kitendo hicho wakisema kilikuwa na lengo la kuficha ukweli wa tukio hilo.

Mke wa marehemu

Kilaza alidai kuwa kifo cha mumewe kilitokea baada ya zaidi askari 20 kuvamia nyumbani kwake yapata saa tisa usiku na kumwamuru Fungungu kutoka nje na alipogoma, ndipo walipoanza kupiga risasi na kuvunja vioo vya madirisha na milango na risasi kumpata marehemu. Pia alidai kuwa walipiga mabomu ya machozi.

Alisema baada ya tukio hilo, walivunja mlango na kuingia ndani kisha kumchukua mumewe ambaye tayari alikuwa amefariki na kumtupa nje... “Mimi pia walinichukua wakanitupa nje ya uzio baadaye wakaanza kunipekua nguo za ndani na kuchukua Sh1.2 milioni ambazo nilikuwa nimezificha baada ya kuona wameanza kufyatua risasi.”

Wakizungumzia tukio hilo, Mbunge wa Bukombe, Profesa Kalikoyela Kahigi na Diwani wa Runzewe, Yusufu Fungameza walisema Serikali inatakiwa kuingilia kati suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika katika tukio.

Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, Kamanda Paulo aliwaahidi waandishi wa habari kwamba angelitolea ufafanuzi jana Jumatatu. Hata hivyo, alishindwa kufanya hivyo kwa madai kwamba anapisha kwanza uchunguzi wa mwili wa marehemu kwenye Hospitali ya Geita" - Gazeti la Mwananchi.
 
mbona hata huko bank majambazi wanakkwapuabhana tatizo ni kwamba ci tunaona ajabu kinoma kuona hao jamaa wanaiba huto tu sh mil mia 3 b sasa na wale walio tuibia watanzania wote kuanzia richmond epa itpl tanzanite tunaongeaje bhana
 
Kutokana na aina ya biashara aliyokuwa anafanya hakuna cha ajabu hapo. Wafanyabiashara wengi wa madini huwa wanakuwa na pesa Kama hizo au zaidi nje ya mabenki. Ukiletewa mzigo usiku wa milioni 20 utafanyaje na huku mabenki yanakuwa yamefungwa. Mara nyingi hao wauzaji wadogo wadogo wanataka hela hapo hapo hamna habari ya njoo kesho uchukue hela.

Hamna cha ajabu kwa mfanyabiashara wa aina hiyo kuwa na kiasi Kama hicho nyumbani kwake au ofisini. Benki ni wasumbufu sana haswa mikoani...kuna watu wananielewa namaanisha nini hapa
.
Ni kweli mkuu kwa biashara ya madini inavyofanyika wala hakuna cha ajabu hapo. Tatizo watu wanajifanya wanajua kila kitu na wanakosoa na kulaumu tu.
 
posili posili ah! samahani, jeshi la polisi lilianza kuharibika toka mfumo wa vyama vingi uanze,ccm waliwafundisha uhalifu wa aina mbalimbali kiasi kwamba ccm sasa hawawezi tena kuwarekebisha, kwa kifupi polisi ndio waalifu namba 1 hapa tanzania wanavuta bangi, wanapiga wake zao tena hadharani, wanaiba, wanaua, wanabaka rushwa ni halali.
 
Ni kweli mkuu kwa biashara ya madini inavyofanyika wala hakuna cha ajabu hapo. Tatizo watu wanajifanya wanajua kila kitu na wanakosoa na kulaumu tu.
Hili ndio tatizo letu kubwa Watanzania mkuu.
 
Yaani sasa watanzania tutakuwa hatuogopi kukutana na majambazi bali tutaogopa kukutana
na polisi,maana wao ni wauaji kuliko majambazi.

Majambazi wanaweza kuchukua pesa wakakuacha hai lakini polisimajambazi pesa wanachukua na wanakuua"
 
Wingu la sintofahamu kuhusu kifo cha mfanyabiashara wa madini aliyedaiwa na polisi kujiua mkoani Geita (runzewe) baada ya ndugu wa marehemu kukataa kuuzika mwili wa marehemu mpaka uchunguzi (postmortem) ufanyike na hela zinazokadiriwa 300m alizokuwa nazo nyumbani kwake zilichukuliwa na polisi zipatikane.

Mwili umekutwa na tundu mbili za risasi kichwani na tumboni kitu kinacholeta wasiwasi kama kweli alijiua.

Juhudi za RPC wa Geita kuwatisha wazike zimeshindikana na marehemu amekwamia Geita Hospital

[h=1]Polisi watumia nguvu kuzuia maiti kusafirishwa Geita[/h]POLISI wa Mkoa wa Geita wametumia nguvu kuzuia msafara wa waombolezaji waliokuwa na mwili wa marehemu mfanyabiashara, Yemuga Fungungu (48), mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vurugu kubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikuwapo wakati askari wake walipoingilia msafara huo na kusababisha vurumai kubwa.
Waombolezaji hao walikuwa wakiuhamisha mwili wa marehemu Fungungu kutoka Hospitali ya Runzewa kuupeleka katika Hospitali ya Geita.

Sakata hilo la ndugu na polisi lililotokea saa nane mchana juzi Jumamosi katika Pori la Samina, Geita na polisi wakiwa kwenye magari matatu wakiwa wamesheheni silaha mbalimbali walifika na kuzuia mwili wa marehemu kusafirishwa.

Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwamo mkewe, wanadai kwamba Fungungu alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi wanaosemekana kwamba walimvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita kisha kupora mamilioni ya fedha. Wanadai kwamba alipigwa risasi tumboni na kichwani katika Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe mkoani hapa.

Katika tukio hilo inadaiwa kuwa kiasi cha Sh360 milioni kiliporwa. Kati ya fedha hizo, Sh60 milioni zinadaiwa kwamba zilikuwa kwenye gari wakati Sh300 milioni zilikuwa kwenye masanduku mawili yaliyokuwa ndani ya nyumba.

Pia ndugu hao walidai kwamba Sh1.2 milioni zilichukuliwa na askari wawili wa kiume baada ya kumpekua mke wa marehemu kwenye nguo za ndani.

Pia askari hao wanadaiwa kupora mali mbalimbali za marehemu zikiwamo redio mbili, video kamera moja, nguo za marehemu ikiwamo kanzu, mashine ya printer, mashine ya inventor, karatasi za picha, deki mbili za kucheza CD, pamoja na nguo za mke wa marehemu.

Mapema Kamanda Paulo alikuwa ameeleza kuwa marehemu alijiua mwenyewe baada ya kumjeruhi Polisi, Fortunatus Beatus kwa risasi lakini taarifa hizo zimepingwa vikali na ndugu na jamaa wa marehemu ambao wanadai marehemu aliuawa na polisi akiwa nyumbani kwake.

Polisi kuzuia waombolezaji

Baada ya polisi kuyasimamisha magari manane yaliyokuwa katika msafara huo wa kupeleka mwili wa marehemu kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya Geita, kulizuka mabishano makali kati ya Kamanda Paulo na ndugu wa marehemu.

Inadaiwa kwamba polisi walikuwa wakishinikiza mwili huo urejeshwe Runzewe, Bukombe kwa kuwa tayari ulikuwa umefanyiwa uchunguzi jambo ambalo liliwakera waombolezaji hao.

Kabla ya kamanda huyo kufika eneo hilo, msafara huo ulisimamishwa na Polisi wa Usalama Barabarani ambao walikuwa wamefuatana na wale wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita, Leonard Makona.
Baada ya kuusimamisha msafara huo, Makona aliwataka ndugu wa marehemu kumsubiri Kamanda Paulo ambaye alifika baada ya takriban dakika 10.

Mwandishi wa habari hii ambaye alikuwa katika eneo la tukio, alishuhudia ndugu wa marehemu na Kamanda Paulo wakirushiana maneno.

“Mnapeleka wapi mwili wa marehemu, ina maana hamkuridhika na uchunguzi wa daktari wa Bukombe?” alihoji kwa ukali na kujibiwa pia kwa ukali na kaka wa marehemu, Mariatabu Fungungu: “Kwa nini mnatusimamisha? Tunaomba tuite waandishi wa habari hapa ili waje washuhudie tukio hili. Kwa nini msikae ofisini?”

Source: Mwananchi

Hili Jeshi letu lina mambo, hata kusafirisha mwili wa marehemu hadi RPC aruhusu? Ipo namna hapo si bure!
 
Back
Top Bottom