Changamoto ya kiwango cha elimu Tanzania

Zamazangu

JF-Expert Member
May 16, 2015
794
412
Nchi yetu ya TANZANIA kwa muda mrefu sasa imekuwa ikionesha kuwa elimu inayotolewa katika taasisi zake Ina shida. Haiwapatii wahitinu wake kila ngazi kinachostahili.

Sababu za changamoto hiyo zimetajwa kuwa ni pamoja na:

1. Kiwango Cha baadhi ya watoa elimu kuwa chini hivyo kuathiri uwezo wao wa kufikisha maarifa kwa wanafunzi.

2. Mfumo wa elimu kuwa na sehemu kubwa ya nadharia na sehemu ndogo sana ya vitendo.

3. Watoa elimu kukosa Ari ya kufanya kazi kutokana na malipo kidogo ya KAZI.

4. Mazingira ya ufundisha na ujifunzaji kuwa duni hivyo kuathiri zoezi Zima la ufundishaji.

5. Mada nyingi za masomo anayofundishwa mashuleni na vyuoni kutoenda na wakati hivyo kupoteza maana na sababu au matumizi ya elimu hiyo katika jamii ya sasa.

Kwa kiangalia hayo yote yaliyosemwa hapo juu Kuna kila sababu ya kiangalia upya mfumo wetu wa elimu ili uendane na mazingira ya sasa.
 
Back
Top Bottom