Changamoto wakati wa Covid19: Safari ya basi kwa sasa kutoka Tunduma mpaka Afrika Kusini

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
14,597
25,721
Kuanzia Tunduma ambapo niligonga passport kwa kulipia chanjo ya Corona Kama dereva wa Roli ambayo ilikua Tsh 10,000 nikapanda bus asubuhi ambayo ilifika Lusaka siku hiyo hiyo usiku wa saa mbili power tools kampuni ya Zambia, nikalala pale hotel zao mpaka asubuhi baadae nikaelekea eneo la Intercity kujua taratibu za kusafiri nikaambiwa tunatakiwa kupima corona kwa gharama ya usd 100 ambayo unapata majibu baada ya siku mbili hapo UTH Hospital ambapo kampuni mnayosafiri nayo ndio watakaopewa majibu na kugawa kwa abiria wote siku ya safari.

Siku ya safari ilikua Jumapili saa kumi na moja alfajiri muda tofauti na hapo mwanzo kabla ya janga la corona ilikua tunatoka saa nne asubuhi. Na pia kwa kuwa mipaka ya Zimbabwe kufungwa, makampuni mengi wameamua kupita Botswana ambao mipaka yao ipo wazi ila magari mwisho wa kutembea ni saa tatu usiku.

Tulisafiri kama masaa Saba baada ya kufika Kazungura mpaka wa Botswana na Zambia upande wa Zambia tukamaliza vizuri mtihani wa rapid test ukaanza tena upande Botswana unaonyesha karatasi ya Lusaka unapimwa kama hauna safari inaishia hapo na wapo ambao safari iliishia hapo kwa kupata majibu ya hiyo test kwa abiria wote ni karibu masaa kumi na mbili kila abiria ni dk 15 tukamaliza kupima pale ingawaje wapo wadada watatu tukaambiwa vipimo vimeleta postive hawaruhusiwi kusafiri, wakachukuliwa na ambulance za Botswana na kupelekwa huko karantini zao.

Tukaambiwa usiku huu bus halitoruhusiwa kuendelea na safari inatakiwa mlale maeneo karibu na haya na tuliambiwa ni marufuku kwa abiria yeyote kutembea kwa muda huo.

Mimi nikaona ngoja nikatafute chakula ingawaje Watswana wana mfumo wao wa kimagharibi mno kuhusu chakula tukatoka pale kundi kufata chakula moja ya garage zilizo karibu cha ajabu baada ya kununua chakula police walikua nje wanatusubiri watupige fine ya Pula 100 au Rand 200 kwa kuvunja sheria ya kutembea usiku kipindi cha corona.

Ikabidi tubishane pale ila haikusaidia chochote maana gari ziliongezeka kama hutaki kulipa unapelekwa police ukalipe mahakamani kesho ikabidi tuwalipe hiyo hela na kurudi kwenye bus huku watu wakiwa hawana kabisa na hamu tena na chakula tena.

Safari ilianza tena alfajiri kama kawaida kuitafuta border ya Martindrift ambayo haina usumbufu tofauti na hii ya kupitia Gaborone kabla hatujafika Francistown tena abiria wote tulishushwa ukaanza ukaguzi wa vyeti vya corona cha Zambia na Botswana hapo wote walikua navyo hatukupata usumbufu maana hapo ni madaktari na wanajeshi tu.

Safari ikaanza ya kuelekea mpakani ambapo tulifika saa nane hapo palikua hapana abiria wengi zaidi ya truck Kama tano tuu tukapimwa joto tuu na kuangalia vyeti vya corona kwa nchi tulizotoka wakafanikisha ndio unaruhusiwa kwenda kuwaona maafisa uhamiaji kwa ajili ya kugongewa tuliingia na kugongewa abiria wote na kuendelea na safari ya JHB ambayo tulifika saa nne usiku.

Kwa mazingira hayo wakitoa chanjo itakua abiria wanasafiri na kadi ya chanjo tuu maana sasa hivi hawakagui tena hiyo kadi ya chanjo ya homa ya manjano inatakiwa hiyo ya corona tu.

Nadhani kazi ndio Kwanza inaanza ila kwa madereva wa truck wao wanapimwa SA tu na kulipia Kama rand 200 pekee huko kwingine wanapimwa joto tu.
 
Weka hata vipicha vya njiani na huko mipakani tuone hata jua la huko linawakaje.

BTW ungesema na lifestyle ya huko kupoje na mambo mengine uliyoyaona tofauti na Tz ili uzi huu uwe ja tija.
 
Halafu unakutana na pimbi mmoja anakwambia eti hizo chanjo ni zao tu kwetu ni marufuku!!bila kufikiria, kwani kitakachofuata ni hicho, kwenda nchi yoyote lazima uwe na card ya chanjo ya covid19!!hapo utaikwepa vipi?halafu ni msomi wa kiwango cha prof. Tulipofikia ni rahisi kumpinga MUNGU, lakini sio MEKO!!!inasikitisha sana,
 
Back
Top Bottom