Changamoto nayopitia bank ya FNB

Hatuwakatazi kuwa wajuaji lkn mnapopigwa mnakuja kwetu washamba kutafuta huruma maana yake nini?? Punguza ujuaji wakati hujui
Nilishawahi kukufata kutaka Huruma yako?

Local banks huduma ni mbovu mbona hutaki kukubali.

NMW wameanzisha card yao ile ya Prepaid, ni mataputapu matupu. Sijawahi pata shida Equity na KCB.

KCB nikipataga shida simu za wahudumu zinafululiza mpaka wanamake sure wamenitatulia tatizo langu. Wanajali.

Siyo hizi bank uchwara.
 
Siku ukitumia Barclays kwa sasa ABSA utagundua hivyo vi bank vyenu vya kizalendo vina uswahili mwingi sana.
Uko sahihi mkuu,mfano saizi kuna shida ya Dollars sana,NMB wanakupa mwisho Dollars elf moja tu hata kama una account,ila jana nimeenda ABSA tawi lipo pale City Mall japo Sina account wamenipa elf 2,nimeenda siku 3 nimepata elf 6😂 bila shida........nawaza kuwa na account huko .....
 
Huwa najiuliza benki zooooooote za Kizalendo zilizopo mtu anapata wapi ujasiri wa kuweka pesa zake KCB, BOA, FnB nk nk anyway Mkuu ukiamua kununua Gari la Mzungu tegemea kulia kama hivvi acha sie tuendelee na NMB/TOYOTA zetu
Nmb ,crdb ndio za pekee tu
 
NMB CRDB NBC hizi ndiyo bank za TANZANIA za uhakika na salama muda wote... Tatizo lenu WaTz mnapenda sana vya bure mnataka muweke pesa bank isikatwe hata shilingi mia, sasa bank itajiendeshaje kama sio kufa na kudhulumu wateja...
Lkn CRDB hapana
 
Kwanza pole. FNB bank walikua acquired na Exim bank, mwaka 2022 mwezi july..so all assets and liabilities (customer deposits) za fnb zilihamishiwa Exim bank.

Therefore that being a case all complains regarding your fnb account zinatakiwa kua handled na Exim bank..so endapo jitahada zitagonga mwamba Basi nenda BOT dawati/section ya customer compliant watashughulikia issue yako immediately.

(kumbuka BOT walitoa regulation inayohusina na consumer protection kwa wateja wa mabenki..na kuweka timelines(SLA ya kila tatizo na duration ya kutatuliwa such that hiyo duration ikizidi basi mteja a lodge complain yake BOT.
Ushauri mzuri sana
 
Huwa najiuliza benki zooooooote za Kizalendo zilizopo mtu anapata wapi ujasiri wa kuweka pesa zake KCB, BOA, FnB nk nk anyway Mkuu ukiamua kununua Gari la Mzungu tegemea kulia kama hivvi acha sie tuendelee na NMB/TOYOTA zetu
Nmb ,crdb tu ila zingine za kisalendo ninjinga mtupu Eti mwanga community ,Mara kcccbl Mara njombe community hao hawna mitaji ya kufanya Kaz Ni full matezo

Standard ,stanbik na kcb , equity nazo uhakika
 
Bank bora kwasababu ya huduma.. nazunguka sana na ndio bank nayotumia
unazunguka dsm, mwanza, dodoma na nje ya nchi nini? Hufiki wilayani, btw hata baadhi ya makao makuu ya mikoa hayana bank hii, kigoma mmojawapo, Mimi pia mteja wa absa since barclays days, lakini ukosefu wa mtandao wa matawi ni big weakness. Hao na kina Equity, Eco bank etc ni bank za mijini tu
 
Kwanza pole. FNB bank walikua acquired na Exim bank, mwaka 2022 mwezi july..so all assets and liabilities (customer deposits) za fnb zilihamishiwa Exim bank.

Therefore that being a case all complains regarding your fnb account zinatakiwa kua handled na Exim bank..so endapo jitahada zitagonga mwamba Basi nenda BOT dawati/section ya customer compliant watashughulikia issue yako immediately.

(kumbuka BOT walitoa regulation inayohusina na consumer protection kwa wateja wa mabenki..na kuweka timelines(SLA ya kila tatizo na duration ya kutatuliwa such that hiyo duration ikizidi basi mteja a lodge complain yake BOT.
Hii ni last option mkuu,maana ukienda huko bank inapigwa faini kubwa sana
 
unazunguka dsm, mwanza, dodoma na nje ya nchi nini? Hufiki wilayani, btw hata baadhi ya makao makuu ya mikoa hayana bank hii, kigoma mmojawapo, Mimi pia mteja wa absa since barclays days, lakini ukosefu wa mtandao wa matawi ni big weakness. Hao na kina Equity, Eco bank etc ni bank za mijini tu
Kwangu bank bora ni ABSA.. nimeanza tumia pia tangu ikiwa barclays.. hilo la wao kutokuwa na branch sio issue. Ila mda wowote nao taka hela napata
 
Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa hii bank ya Fnb kwa muda mrefu sana na sikuwahi kupitia changamoto yeyote hadi wiki iliyopita ndio nikakutana na kizaazaa!

Ipo hivi hii bank huwa natumia kusave vipesa navyopata kwa malengo ya muda mrefu kwavile huwa hawana makato ya hapa na pale!

Sasa wiki iliyopita nikawa na shida na pesa yakuzungushia kwenye biashara yangu inabidi niende kuchukua kama milioni 3 hivi mara naambiwa akaunti yangu imeblokiwa kwahiyo siwezi kufanya muamala wowote!

Sema kweli nilichanganyikiwa kutokana nilikuwa nahitaji hiyo pesa haraka sana iwezekanavyo!

Ikabidi niulize kulikoni kufunga account ya mteja bila taarifa yeyote bila sababu za msingi? Nikajibiwa kwamba inabidi nijaze taarifa zangu upya za ki bank!

Kweli nikafanya hivyo na ukizingatia pia nilishajaza taarifa zangu upya miaka miwili tu iliyopita,lkn cha ajabu hadi leo siku ya 8 hawajafungua akaunti yangu ni danadana tu kwa kwenda mbele,nimeenda bank mara mbili mwendo ni kujaza fomu kila kukicha!

Nimejaribu kupiga simu huduma kwa wateja wanasema ombi langu wanalishughulikia hadi nimechoka wakuu!
Msaada wakuu nina ninachotakiwa kufanya maana mipango yangu imesimama huku nikiteseka na pesa zangu mwenyewe!
Kiukweli ingenitokea mm ni either ningekuwa ngome au ingekua habari mtaani,haiwezekan pesa ikawa yangu halafu mnanizingua
 
Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa hii bank ya Fnb kwa muda mrefu sana na sikuwahi kupitia changamoto yeyote hadi wiki iliyopita ndio nikakutana na kizaazaa!

Ipo hivi hii bank huwa natumia kusave vipesa navyopata kwa malengo ya muda mrefu kwavile huwa hawana makato ya hapa na pale!

Sasa wiki iliyopita nikawa na shida na pesa yakuzungushia kwenye biashara yangu inabidi niende kuchukua kama milioni 3 hivi mara naambiwa akaunti yangu imeblokiwa kwahiyo siwezi kufanya muamala wowote!

Sema kweli nilichanganyikiwa kutokana nilikuwa nahitaji hiyo pesa haraka sana iwezekanavyo!

Ikabidi niulize kulikoni kufunga account ya mteja bila taarifa yeyote bila sababu za msingi? Nikajibiwa kwamba inabidi nijaze taarifa zangu upya za ki bank!

Kweli nikafanya hivyo na ukizingatia pia nilishajaza taarifa zangu upya miaka miwili tu iliyopita,lkn cha ajabu hadi leo siku ya 8 hawajafungua akaunti yangu ni danadana tu kwa kwenda mbele,nimeenda bank mara mbili mwendo ni kujaza fomu kila kukicha!

Nimejaribu kupiga simu huduma kwa wateja wanasema ombi langu wanalishughulikia hadi nimechoka wakuu!
Msaada wakuu nina ninachotakiwa kufanya maana mipango yangu imesimama huku nikiteseka na pesa zangu mwenyewe!
Na tunavyoongea hapa Kampuni imeshauzwa(imeuzwa kwa nani story nyingine) hata baadhi ya wafanyakazi waliachishwa mapema kuanzia January to March.
Njia pekee kutana na meneja ongea nae after there baba wao BOT anahusika kusimamia haki za wateja but visit FNB manager don't roam around with Brunch managers /customer care you cannot have enough information related to your problem by accessing hao subordinates.
 
Barclays Stanbic FNB ni vikoba vilivyochangamka
Vicoma ni hizo local bank.

Nakupa rule of thumb.

Ukishaona bank ukitaka kutoa pesa nyingi maswali yanakuwa mengi Hiyo bank uchwara aka kikoba kimbia haraka sana.
 
Back
Top Bottom