Changamoto 10 usafiri mwendokasi

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Sina shaka hata kidogo na utendaji wa Mkurugenzi Waziri Waziri Kindamba. Hakuna chembe ya ubishi ndiye aliyeleta mapinduzi katika utendaji wa kampuni ya umma ya TTCL ambayo kabla ilikuwa 'Mortuary' ikipumua kwa msaada wa mashine.

TTCL ilitajwa kuwa miongoni mwa taasisi za serikali inayojiendesha kwa hasara huku kodi za walal hoi zikitumika kulipa mishahara na kugharamia shughuli za kila siku za kiofisi. Ni huyu Waziri Kindamba ndiye aliyeisitiri serikali na hatimaye Ttlc ikawa na uwezo wa kutegeneza faida na hata kutoa gawio srikali kuu kama sehemu ya faida. Ttcl sasa ikatajwa kama moja ya kampuni za simu inayokuwa kwa kasi nchini.

Kwa utendaji wake huo ndiyo Mamlaka zilishawishika kumteua kwenda kuongoza Mkoa wa Njomba na kisha baadae Songwe na Tanga.

Ikulu imesikia malalmiko ya wananchi juu ya huduma mbovu za Wakala wa mabasi ya Mwendokasi ambayo licha ya fedha nyingi zilizowekwa kwenye mradi huo,kila leo huduma zake zimekuwa zikififia na kufubaa kiasi cha kuwakatisha tamaa wananchi. Kwa alivyoipanga TTLc ikamfanya kuaminiwa tena kwamba anaweza kuissawqzisha UDART na mambo yakawa sawasawa.

Mheshimiwa Kindamba yupo katika kiti cha ukurugenzi cha UDART,ninamkumbusha changamoto anazopaswa kuzilabili ili kuweka mambo sawa:

1. Kusubiri magari muda mrefu
Hii ndio kero kuu pale mwendokasi. Inasemwa kwamba hivi leo mwendokasi si mwendo kasi tena,bali ni mwendo pole. Imekuwa kawaida kusubiri gari hata nusu saa tena utasubiri ukiwa umesimama wima.

Hapa naomba niongeze na hitaji la kuweka mazingira rafiki kwa abiria kusubiri mabasi,vituoni hakuna viti kwanini!??wasikwambie wameweka vibenchi viwili! Tazama kituo cha Morocco na Ubungo hata Kimara,basi na kwingine iwe hivyo.

2. Msongamano kwenye magari
Msongamano mkubwa kwenye magari ya mwendokasi ni kero isiyosimulika. Ni rahisi kusema kwamba inasababishwa na uchache mabasi,lakini kuna sababu ya management kushindwa kuyatumia mabasi mengi yaliyopo. Msongamano si suala ka kulichekea coz ni sababu ya maradhi ,inavutia vibaka lakini pia inasababisha hadha kwa baadhi . Sitaki kuamini kwamba lengo la kuleta huduma hii ilikuwa ni kuhakikisha wananchi wanaminyana kwenye magari na kusabaisha yasiyofaa.

3. Magari kuwapita abiria
Tatizo la ziada hili,tunajiuliza gari linaenda ferry,linapita tupu kabisa kituo ambacho abiria wa ferry wamejaa likiwaacha wakilitamani lileee likienda.badala yake basi lililojaaa ndio linakuja kusimama liwabebe hawa abiria dakika ishirini au nusu saa baadae. Huwa ni maelekezo maalum au ni akili tu za madereva kwa kutojali abiria wao?

4. Viburi binafsi vya wahudumu
Utakuwa shuhuda wa kilichotokea juzi,dereva wa mwendokasi sijui kala magimbi ya wapi kaamua kugombana na abiria na kwa hasira akaamua kutoshusha abiria popote. Hii ni moja tu imeonekana,naomba tujiulize,ni mangapi yanayotokea hayaripotiwi kama hili. Ukiona moja nimejidhihiri,amini kuna tisa yanayotokea hujayaona.

5. Mfumo wa malipo
Hapa ninajqribu kufikiria kwa sisi tunaotokea kigamboni ambako abiria wote tunavuka kwa kutumia kadi maalum ya malipo inaitwa N-CARD. NAJIULIZA kama ninavuka ferry na kuingia uwanja wa Taifa kwa Card ya kielektroniki,kwanini kadi hii isitumike pia kwenye mwendokasi? Kwako Kindamba hili jepesi sana.

6. Baadhi ya maeneo kukosa huduma
Kigamboni ni moja ya maeneo yanayokuwa kwa kasi sana na pia lenye changamoto ya usafiri hasa nyakati za asubuhi na jioni. Kea minajiri ya huduma ya usafiri dar es Dalaam,UDART sasa inasimama kwenye nafasi ya ile iliyokuwa USAFIRI DAR ES SALA(UDA).
Kigamboni tunahitaji hiyo huduma haraka sana mheshimiwa.

7. Msongamano kwenye madirisha ya tiketi
Ninarudia kuitumia kigamboni kama darasa la mfano,pale mamia ya abiria wanavushwa na kivuko kwa wakati mmoja,then wakifika kwenye dirisha la mwendokasi wanakutana ni madirisha mawili tu yanayotoa huduma ya kuuza tiketi,hapa watalazimika kukaa kwenye foleni kati ya dakika tano mpaka kumi kukata tiketi tu. Hii si sawa, ni aidha yaongezwe madirisha ya kutoa huduma hiyo au rejea huduma yabkielectroniki itakayoua kabisa hii foleni ya kununua tiketi. Chukia foleni kwenye huduma yako.

8. Muda wa kutoa huduma
Awali,njia zote ambazo mwendokasi barabara imepita kulikuwa na daladala ambazo zilikuwa zikitoa huduma hiyo hata saa sita usiku. Mwendo kasi wamemonopolyse huduma hii lakini wao wanaishia saa nne usiku tu. Hii maana yake ni kwamba ninalazimishwa kurudi nyumbani chini ya saa nne usiku ili nisiachwe na mwendokasi. Dar es salaam ya sasa ipo hai masaa 24,why mwendokasi waishie saa nne usiku?

9. Madereva kupuuza alama za barabani
Hii ni moja ya sababu za ajali ulizowahi kuzisikia zikihusisha mwenndokasi. Hii ilisababishwa na baadhi ya viongozi kuwaamknisha madereva wa mwebdokasi kwamba wao ni watukuufu. Hata pale inapowezekana kufunga breki kumpisha mvuta bangi wa bodaboda apite salama, dereva wa mwendokasi ndo kwanza anakoleza moto. Ajali nyingi za mwendokasi zinatokea kwenye mataa ya kuongozea magari. Dhima kwako ni kuwakumbusha kwamba wao wanawajibika kwenye sheria kama madereva wengine,hii uwakumbushe na jeshi la Polisi pia,wawajibishe madereva wa mwendokasi kama ilivyo kwa madereva wengine. Nimeshuhudia mara kadhaa kwa macho yangu wakivuka taa nyekundu na gari za kawaida kulazimika kumsubiri mwendokasi apite.

10. Wapi tupeleke malalamiko?
Kwenye kila kituo cha mwendokasi ninashauri awepo mtu au kuwepo na namba ambayo ipo hai,inapotokewa sijaridhishwa na huduma niwasilishe malalamiko yangu haraka na nishuhudie yakifanyiwa kazi. Wale walinzi na wakata tiketi huwa hawana msaada wowote pindi abiria anapotaka kuwasilisha dukuduku lake kwa mamlaka. Hii namaanisha mamlaka iwe karibu na wateja wake tuna mengi ya kuzungumza kwa nia ya kujenga,. Hii iende sambamba na kutembelea field mara kwa mara na kuzungumza na abiria wako utajifunza mengi ya msingi. Na pia iende sambamba ma ile tabia ya kifanya ziarq za kustikiza ujionee mwenyewe mambo yanavyokwenda.

Kiongozi wangu kindamba bado kijana sana,ninatamani ukainyooshe UDART wana Dar es salaam tunaimani nawewe.
Screenshot_20240322-105257_Google.jpg
 
Mradi wa mwendokasi ni takataka nyingine, kwanza isiitwe mwendokasi iitwe magari yanayopita kwenye njia yake yenyewe
 
Mradi ulishashindwa huo, tumetoa maelekezo atafutwe mwekezaji kabla mwaka huu haujaisha.
 
View attachment 2944799
AKITATUA HIZO CHANGAMOTO, NIKO PALE NIMEKAA

Watendaji wengi wamepita lakini kila siku siasa siasa tu, woooi tumechoka
 
Back
Top Bottom