Elections 2010 Chama kinaruhusiwa kuteua mgombea mpya baada ya aliyeteuliwa awali kuenguliwa na NEC?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Baada ya kusoma habari hii: NEC sasa kuengua CCM kwenye Gazeti la Raia Mwema nimepata mshituko kidogo. Kwa wale ambao ni wajuzi wa Sheria labda wanaweza kutusaidia kutuelewesha.

Kwenye habari hiyo Mzee Kinana anasema kwamba:

Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulraham Kinana alisema uamuzi wowote wa NEC ni wa mwisho kisheria na kwamba kama hali itakuwa hivyo chama chake kitarejea kwenye taratibu zake ili kuteua wagombea wengine kuziba pengo la watakaoenguliwa.

“Ni vizuri zaidi kusubiri matokeo ya Tume kuhusu pingamizi hizo, lakini taratibu zinafahamika kama katika maeneo ambayo wagombea wetu walitangazwa kupita bila kupingwa watarejeshewa wapinzani, maana yake watabaki kuwa wagombea wetu.

“Lakini ikitokea wagombea wetu waliowekewa pingamizi wakaenguliwa Tume, tutumia vikao vyetu kwa mujibu wa taratibu za CCM kuteua mgombea mwingine kutoka kwenye orodha ya wagombea waliojitokeza kwenye kura za maoni,” alisema Kinana.

Source: Raia Mwema - NEC sasa kuengua CCM

Kama deadline ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea kutoka ofisi za NEC imeishapita, hao wagombea wapya wa CCM wataingizwaje kwenye uchaguzi?

Ina maana vyama vya upinzani huwa havina uwezo wa kuteua wagombea wapya ili kujaza nafasi ya mgombea aliyeenguliwa?

Sheria ya Uchaguzi inasemaje iwapo mgombea akiwekewa pingamizi na likakubaliwa, je, chama chake kinaruhusiwa kuteua mgombea mwingine?
 
hapa ndipo watajichanganya hadi wachoke.

wale wabunge kumi waliopita bila kupingwa (kwa kuondoa wapinzani wao kwa mapingamizi) wameanza kuonja joto la jiwe.
 
hapa ndipo watajichanganya hadi wachoke.

wale wabunge kumi waliopita bila kupingwa (kwa kuondoa wapinzani wao kwa mapingamizi) wameanza kuonja joto la jiwe.

Mkuu wangu Mwafrika,

Nyani huwa haoni kundule (samahani kwa Mheshimiwa NN) ... angalia huyu Mzee Kinana kwenye habari nyingine anasema kwamba watu wanakimbilia kuweka mapingamizi na ilihali mabingwa wa kuweka mapingamizi ni CCM. Ila kwa kuwa JK kawekewa pingamizi, tayari anaona kwamba siasa za mapingamizi hazifai.

Kinana alishauri CHADEMA watumie hoja kushawishi wapiga kura na si kuzusha kashfa, kuhangaika kuweka pingamizi au kukimbilia mikutano na waandishi wa habari, akisisitiza ni muhimu kukimbilia kujinadi kwa wapiga kura ili kueleweka na kuchaguliwa.

Source: Raia Mwema - Jino kwa jino CUF, CCM na CHADEMA

.... eti kashfa za kuzusha, kama ni za kushusha si waliozushiwa waende mahakamani ili wakapewe haki yao, wanasubiri nini?

.... eti wanahangaika kuweka pingamizi, mbona wabunge wa CCM walipokuwa wakiweka pingamizi sikumsikia akisema waende kupiga kampeni badala ya kusaka ushindi wa mezani.

.... eti wanakimbilia kuitisha press conference, jamani Makamba ndio alikuwa wa kwanza kuitisha press conference kwamba CHADEMA wametumia lugha ya matusi, baada ya hiyo press conference ndipo Prof. Baregu alipoitisha ya kwake kujibu hoja za Makamba.

Kinachofanywa na CCM ni sawa, lakini vyama vingine vikifanya hivyo ni makosa. Kaazi kweli kweli!

Pingamizi la CHADEMA limewaweka pabaya, maana hawajui Tendwa atasema nini na pia hawajui maamuzi ya Tendwa kama yatakubaliwa na CHADEMA na pia hawajui next move ya CHADEMA kama itakuwa ni mahakamani au watakaa kimya.
 
Kuna sheria zingine za NEC ni za kufurahisha kama si kusikitisha eti mgombea mwenye sifa zote anaenguliwa kwa kukosea tarehe ya kuzaliwa, kwa nini asiambiwe arekebishe. Au kwa nini wasipewe second chance kama watu wengine wanavyopewa kujisahihisha.

Mfano mtu kaandika kazaliwa tarehe 18/08/2010 anaenguliwa, hivi anayepokea fomu na kuona hilo kosa kwa nini asitumie busara za kibinadamu, mimi sioni kama kosa hilo ni kubwa kiasi cha kumwengua mtu. Mgombea kama huyo adhabu yake iwe ni kusafiri kwenda mwenyewe ofisi za NEC Dar na kurekebisha na si kuenguliwa. Tutakuwa tunaacha wagombea wazuri kwa vijisababu vya kijinga.

Makosa kama kutiwa hatiani na mahakama au kutolipa kodi au uraia hayo ndiyo yanaweza kupelekea kukosa sifa lakini si kukosea jina au kusahau kuweka sahihi. Sometimes NEC wajifunze kuwa tolerant kwa vile wana dill na binadamu wanaoweza kukosea, hata wao NEC they are not 100% perfect.
 
Mkuu Luteni,

Makosa madogo madogo kama ya kukosea tarehe ya kuzaliwa, nakubali kwamba ni uzembe wa mgombea lakini pia ni uzembe wa msimamizi wa uchaguzi. Kiutaratibu, kabla fomu ya mgombea haijapokelewa lazima huwa inakaguliwa kama imejazwa vyema na kama kuna makosa, mhusika huambiwa hapo hapo. Makosa hayo ya kukosea tarehe ya kuzaliwa ni minor na inawezekana sababu ya pressure mtu anaweza kukosea. Kama ulivyosema, kumuengua is not fair, apewe nafasi ya kurekebisha badala ya kubaka demokrasia kwa kututangazia ushindi wa bila kupingwa.

Kwenye mapingamizi haya kuna kitu kingine nina mashaka nacho. Mfano, mgombea X atajuaje kwamba wadhamini wa mgombea Y majina yao hayako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura? Ina maana mgombea X anajua majina yote yaliyo kwenye hilo daftari? Hapa pananitatiza sana.

Wagombea wengi akishamuuliza mdhamini kama shahada ya kupigia kura na akakubali, sidhani kama ana muda wa ku-verify kwamba shahada hiyo imeandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Kutengua uteuzi wa mgombea aliyedhamiwa na wadhamini ambao shahada zao hazijaandikishwa kwenye daftari la kudumu, ni kuwaonea.
 
Ni upumbavu mkubwa sana kumuondoa mgombea eti tu kwa sababu amekosea kujaza fomu. it is high time sasa NEC waliangalie upya hili. Watofautishe sifa za mgombea na ujazaji wa fomu. Kukosea kujaza fomu hakumuondelea sifa mgombea kwa sababu makosa ya kujaza fomu yanarekebishika. Lakini mgombea akikosa sifa , kwa mfano alishawahi kufungwa kwa muda unoelekezwa kwenye sheria, si raia, hajafikisha umri wa kugombea kwa mujibu wa sheria n.k. hayarekebishiki hivyo mgombea anaweza kuenguliwa. NEC liangalieni upya hili.
 
Mbona NEC haikuwapa Chadema kuweka mgombea mbadala katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini mwaka juzi baada ya yule wa awali alipoenguliwa na Tume hiyo kutokana na pingamizi la CUF?
 
Kuna sheria zingine za NEC ni za kufurahisha kama si kusikitisha eti mgombea mwenye sifa zote anaenguliwa kwa kukosea tarehe ya kuzaliwa, kwa nini asiambiwe arekebishe. Au kwa nini wasipewe second chance kama watu wengine wanavyopewa kujisahihisha.

Mfano mtu kaandika kazaliwa tarehe 18/08/2010 anaenguliwa, hivi anayepokea fomu na kuona hilo kosa kwa nini asitumie busara za kibinadamu, mimi sioni kama kosa hilo ni kubwa kiasi cha kumwengua mtu. Mgombea kama huyo adhabu yake iwe ni kusafiri kwenda mwenyewe ofisi za NEC Dar na kurekebisha na si kuenguliwa. Tutakuwa tunaacha wagombea wazuri kwa vijisababu vya kijinga.

Makosa kama kutiwa hatiani na mahakama au kutolipa kodi au uraia hayo ndiyo yanaweza kupelekea kukosa sifa lakini si kukosea jina au kusahau kuweka sahihi. Sometimes NEC wajifunze kuwa tolerant kwa vile wana dill na binadamu wanaoweza kukosea, hata wao NEC they are not 100% perfect.
Subiri uangalie ile kashfa ya chenge kutolipa ushuru na bima ya gari! Unafikiri ataenguliwa?
 
The boss (CCM) is always right. CCM wanaweza kupindisha sheria yeyote na kumshinikiza hakimu/jaji/NEC/tume ya uchaguzi wakubaliane nao. Wao wana tafasiri yao tofauti ya kila sheria hapa nchini. Ukiwashinda kwa tafasiri halali wanaibuka na ya kwao na kukushinda kwa nguvu. Their days are numbered. We are not fools. Aiseee
 
Akienguliwa kwa makosa ambayo yamethibitika sheria ilivujwa ndiyo basi, hivi ndivyo ninavyofahamu. CCM wancheza na media kuvuriga hali ya hewa tu, sometime one can win battle kwa maneno tu! (creating fear to the opponent!)
 
Back
Top Bottom