Chama cha Mapinduzi(CCM) wamtoa machozi Eric Shigongo, wamwambia kunywa maji

Dumelo

Senior Member
Apr 23, 2015
139
235
Akiongea kwa masikitiko huku akitoa machozi, amesema amesikitishwa sana na Chama cha Mapinduzi kwan kwa muda mrefu amekua akikipigania Chama cha Mapinduzi kwa Hali na Mali Lakini leo kinamtoa machozi.

Akiandika kupitia Gazeti lake la Ijumaa Wikienda lakini Pia kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook amekilalamikia chama cha mapinduzi kuendelea kumzungusha kuhusu malipo yake zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa tangu Afanye Biashara na Chama hicho, aliendelea kulalamika kua Amefanya jitihada za ziada kumpigia Katibu mkuu wa Chama hicho Abdalah Kinana bila mafanikio kwani amekua hapokei simu zake wala kujibu sms.

Anasema Pamoja na kwenda ofisi za Chama hicho Lumumba alikutana na mweka hazina wa Chama hicho Mamma Zhakia Meghji lakini aliambulia kupewa Maji ya Kunywa Bila kupata Pesa zake.

Kinacho muuma Bw Shigongo ni alivyoacha Biashara zake na Kufanya Kampeni karibu Mikoa 10 huku akimpigia Kampeni Rais mstaafu wa wakati huo Dr. Jakaya Kikwete.

Akiongea kwa masikitiko amesema mpaka sasa Mali zake zipo Mbioni kupigwa Mnada wakati wowote kutokana na kwamba ndizo alizoweka Bond ili aweze kupata mkopo ambao alitumia ku supply baadhi ya materials kipindi cha Kampeni za Uchaguzi 2015.

Kwa maelezo zaidi ameahidi kutoa week ijayo katika ukurasa wake na kwenye Gazeti la Wikienda. Na Amesema ataweka wazi ni Kiasi Gani anakidai chama cha Mapinduzi.

Pole sana Brother Eric Shigongo, Endelea kupigania Haki yako ili wakulipe, ni Matumaini yangu Mwenyeketi wa Chama cha apinduzi amesoma Ujumbe wako na atalifanyia kazi ili uweze kulipwa Pesa zako

============================

NOVEMBA 19,2016 JUMAMOSI YA MCHOZI KWANGU

Nawaomba radhi sana wananchi wa Singida, sikuweza kuwepo Namfua baada ya waandaaji kuahirisha tamasha, ipo siku tutakutana.

Nimekwishasema mara nyingi kwamba, hata mimi, kama ilivyo binadamu wengine huwa nina siku mbaya na nzuri katika maisha yangu, kwa sababu kwa watu wengi tafsiri ya maisha bora ni kuwa na gari, nyumba, kazi, fedha nk. Ni rahisi kudhani kwamba ninaishi maisha ya furaha kila siku, si kweli, kuna siku natokwa na machozi kama binadamu mwingine, naomba nikushirikishe sasa siku yangu ya Novemba 19, 2016, siku ya Jumamosi iliyopita, ili upate uhalisia wa maisha.

Usingizi ulikata saa tisa na nusu usiku, nikaanza kuyapitia maisha yangu na changamoto ninazokutana nazo, mambo ninayoyafanya lakini pia kufanyiwa na watu. Mawazo yangu haya yananifikisha kwenye uhusiano wangu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kwa muda mrefu sana nimekuwa kada wake, mara kadhaa nikijitoa mhanga mimi mwenyewe kukitetea na kukipigania nikiamini ndiyo chama pekee kinachoweza kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli.

Naipenda CCM, nakiamini chama hiki hata kama kuna baadhi ya watendaji ndani yake natofautiana na jinsi wanavyofanya mambo kiasi cha kuathiri hatma ya chama hiki kama taasisi, wapenzi, mashabiki na wanachama wake.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara nimewahi kuacha kazi zangu na kuzunguka karibu nusu ya nchi yetu nikipiga kampeni na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, lakini kwa sababu mtu yeyote anayeonesha mapenzi kwa CCM hasa akiwa mfanyabiashara hutafsiriwa anajipendekeza au mwoga, pengine hivyo ndivyo ninavyoitwa, lakini kwangu mimi ambacho hunisukuma kufanya mambo haya ni mapenzi na imani niliyonayo kwa CCM kama taasisi na zilivyo sera zake.

Kama nilivyosema hapo awali, tatizo langu kubwa huwa ni watendaji wa CCM, ambao wakati mwingine hufanya mambo ambayo huathiri mapenzi yangu kwa taasisi yenyewe, hali hii imewavunja moyo watu wengi sana waliokuwa na mapenzi pamoja na imani kubwa kwa CCM.

Yesu ni mwokozi wangu, daima nitazungumza ukweli, hata kama utanigharimu! Nakumbuka huko nyuma nimewahi kuzungumza ukweli kuhusu CCM kwenye ukurasa huu, baadhi ya viongozi wa juu hawakufurahishwa na nilichokiandika, Katibu Mkuu Kinana nikiongea naye ofisi kwake aliniambia “Eric wewe ni kijana wa hapa, siku nyingine ukiwa na suala la kuzungumza tueleze sisi moja kwa moja, usilipeleke barabarani!”

Nilikubaliana naye na sikuwa tayari kabisa kusema maneno yaliyotokana na mawazo yangu ya usiku gazetini tena, kwani nilimuahidi nisingefanya hivyo, lakini nifanye nini, nisemee wapi? Kama katibu mkuu wangu nampigia simu kila siku hapokei? Namuandikia ujumbe kwa njia ya WhatsApp na unaonekana umesomwa lakini hanijibu, tafsiri yangu ni ya haraka ni kwamba ananidharau ingawa mimi namuheshimu kama baba na kiongozi wangu, angalau angekuwa anapokea simu hata kunipa tu matumaini, nisingefikia hatua ya kuzungumza hapa.

Kuanzia usingizi ulipokata saa tisa na nusu usiku, nilifikiria mambo mengi sana juu ya namna ambavyo baadhi ya watendaji wa CCM wamekuwa wakinifanyia pamoja na kujitoa kwangu kote kwa chama hicho, moyo unaniuma mno kwani sistahili hata kidogo kufanyiwa mambo ambayo leo natendewa na chama ambacho mimi binafsi naamini nimejitoa kiasi kikubwa mno kukitumikia kwa akili, muda na mwili wangu.

Inahitaji usiwe mtu mwenye hofu au uliyekata tamaa kufungua mdomo na kuzungumza nitakayoyasema leo, ndugu zangu, Watanzania wenzangu, moyoni mwangu pamejaa uchungu mwingi mno, acha niseme labda nitakuwa mwepesi! Sijui kitakachonipata, Mungu anajua, mimi ni msema kweli, nionavyo mimi ni bora kuzungumza ukweli ukapata matatizo kuliko ubaki hai ukiendeleza unafiki, NASHINDWA.

Mawazo haya juu ya CCM yananitoa machozi mke wangu akiwa usingizini kando yangu, sitaki kumuamsha, sitaki kumshirikisha kinachoendelea, mimi ni mtoto wa kiume mambo mengine natakiwa kukabiliana nayo mwenyewe, kwa muda mrefu naendelea kuwaza nikiwapitia viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia mwenyekiti mstaafu, mwenyekiti aliyeko madarakani, katibu mkuu na mweka hazina.

“Mama!” saa kumi na mbili na dakika kumi namuamsha mke wangu.
“Bee!”
“Tulikubaliana kwenda hospitali Muhimbili kusalimia mgonjwa.”
“Kweli.”
“Mzima lakini?”
“Naendelea vizuri, wewe?”
“Mimi mzima, nina mafua tu kidogo!” nilimjibu hivyo kwa sababu sikutaka agundue kilichokuwa kimetokea.

Kawaida ya wanawake ni kujiandaa taratibu sana, mpaka tunaondoka kwenda Muhimbili tayari ilikuwa ni saa moja asubuhi, tumechelewa muda wa kuona wagonjwa. Mbele ya Jengo la Mwaisela, alipolazwa mgonjwa ambaye ni mkamwana wa mama mmoja aitwaye Mama Swai, ambaye tulikuwa tukiabudu naye Kanisa la Word Alive kabla hatujahamia Victory Christian Center, tunakutana na mlinzi mkali kama pilipili.

“Muda wa kuona wagonjwa umekwisha.”

“Tusaidie kaka” nambembeleza kwa muda, hatimaye akionekana kunionea huruma, anasema “basi aende mmoja tu, tena mwanamke, maana hii wodi ni ya wanawake.”
“Mama nenda basi wewe!”

Mke wangu anaondoka na kuniacha nimesimama peke yangu nje ya wodi, mawazo yananirejesha tena kwa CCM baada ya kubaki peke yangu, najiuliza ni kitu gani nimekikosea chama hicho mpaka kunitendea mambo wanayonitendea! Roho inaniuma, nasikia huzuni kubwa moyoni mwangu, niko chini kabisa kiroho leo, sina furaha hata kidogo, mawazo ya CCM na mambo wanayonitendea, wakati mimi nilishafanya mema mengi kwao yamenivuruga.

Dakika ishirini baadaye mke wangu anatokeza kutoka wodini, alikuwa amepewa muda mfupi sana, pamoja tunaongozana mpaka kwenye gari, namfungulia mlango, anaketi nami nakaa kwenye usukani na kuanza kuendesha kuelekea ofisini, anawahi kazini kwake kwa sababu leo ana sherehe ya watu waliokodisha hoteli.

Njiani nasikia wimbo wa vijana kutoka Kenya waitwao Sauti Sol, uitwao ‘Kuliko Jana’ nilishawahi kuusikia wimbo huo kabla, lakini leo unaonekana kuwa wimbo mpya kabisa kwangu, maneno yake yananigusa sana moyo, namshikirisha Vene kwenye wimbo huo, anaonekana kama hanielewi au ninachokiongea hakimgusi, bila shaka anawaza sherehe inayofanyika hotelini kwake.

“Hawa vijana wanaimba sana, natamani siku moja niwaalike hapa Dar es Salaam, nifanye tamasha kubwa la vijana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu, bure! Nifundishe vijana wa taifa hili uzalendo na kupenda nchi yao.”

Natamka maneno hayo ingawa moyoni mwangu kuna uchungu mwingi;

Bwana ni mwokozi wangu,
Tena ni kiongozi wangu,
Ananipenda leo kuliko jana!
Baraka zake hazikwishi si kama binadamu habadiliki,
Ananipenda leo kuliko jana,
Kuliko jana, kuliko jana,
Yesu nipende leo kuliko jana,
Kuliko jana, kuliko jana,
Yesu nipende leo kuliko jana,
Nakuomba Mungu uwasamehe
Wangalijua jinsi unavyonipenda
Mimi wasingenisema
Na maadui wangu nawaombea
Maisha marefu wazidi kuniona ukinibariki
Ujue binadamu ni watu wa ajabu sana
Walimkana Yesu mara tatu kabla jogoo kuwika…

Safari inaendelea, wimbo uliokuwa ukipigwa redioni umefika mwisho, kwa kutumia simu yangu nilitafuta ‘You tube’ kisha kuuchagua wimbo huo ambao unaendelea kupiga mpaka namfikisha mke wangu ofisini kwake, kila unapokwisha naurudia tena, unanizidishia uchungu moyoni, namshusha mke wangu na kuendesha tena kuelekea ofisini kwangu.

Mawazo ni mengi, kichwa kimevurugika, Mariam, msaidizi wangu anaingia na kunitayarishia chai, nakunywa lakini haipandi. Baadaye anaondoa vyombo na kuniacha peke yangu, muda mfupi baadaye aliingia mzee Mbizo, sijui kama alinielewa kwa hali aliyonikuta nayo, nilikuwa kwenye siku yangu mbaya, niko chini sakafuni nawaza, baada ya salamu tu tofauti na siku nyingine zote ambazo mimi na yeye huongea mambo machache, anaaga na kuondoka.

Nabaki peke yangu nikiendelea kufikiria, naikumbuka siku ya mwisho nilipofika ofisi ndogo ya CCM pale Lumumba, ambako nilikwenda nikitarajia kulipwa fedha zangu ninazodai kwa kazi niliyoifanya (kwa leo sitataja ni kiasi gani) kama nilivyokuwa nimeahidiwa baada ya kuwa nimesubiri mwaka mmoja na miezi sita, hapo katikati nikiwa nimelipwa fedha kidogokidogo sana.

Tofauti na matarajio kwamba siku hiyo ningelipwa fedha zote, nikalipwa kiduchu tena! Nikiwa ndani ya ofisi ya mweka hazina wa chama, mama Zakia Meghji, yeye ni shahidi, kama nasema uongo au ukweli anajua, machozi yalinitoka! Hali yangu kibiashara ni mbaya, fedha nyingi ziko mikononi mwa CCM na nina madeni makubwa ninayodaiwa, baadhi ya wadai wanataka kupiga mnada mali zangu! Chama Cha Mapinduzi kimeniingiza kwenye matatizo makubwa.

Nakumbuka alichokifanya mama huyu ni kunipa chupa ndogo ya maji ya Kilimanjaro na kuniambia “Kunywa maji mwanangu, upunguze uchungu!” nikayapokea na kuyanywa, niliondoka ofisini hapo nikiahidiwa kwamba ningelipwa muda si mrefu, lakini haikuwa hivyo, siku zinazidi kusonga na hali inazidi kuwa mbaya na hakuna anayeonekana kujali.

Kwenye saa 5: 00 asubuhi hivi, naamua kuachana na mawazo hayo kwani maisha bado yanaendelea na kuamua kwenda kuungana na wenzangu kwenye kikao cha asubuhi kujadili maendeleo ya Gazeti la Ijumaa Wikienda ili nifute kilichokuwa kikiendelea kichwani, nafanikiwa kufanya kikao hicho bila mtu yeyote kugundua kilichokuwa kikiendelea akilini mwangu na baadaye narejea ofisini ambako naendelea kuusikiliza Wimbo wa Sauti Sol huku nikizidi kuhuzunika.

Muda mfupi baadaye anaingia Davina Lema, msimamizi wa kampuni yetu ya Blue Mark Real Estate ambayo inajishughulisha na upangishaji wa nyumba, tunaongea naye kuhusu biashara na namna ya kufanya biashara katika kipindi hiki kigumu, nampenda Davina, alianza kazi hii akiwa hajui chochote lakini sasa amemudu kazi, baada ya mazungumzo hayo ndiyo naanza kumweleza kidogo kuhusu maisha na namna ambavyo mtu unaweza ukatenda wema lakini ukalipwa ubaya.

Sikuweza kuzungumza hadi mwisho, machozi yananitoka mbele ya mfanyakazi wangu, si jambo jema lakini sikuwa na jinsi, siandiki haya ili nionewe huruma la hasha! Nawaeleza muone baadhi ya siku zangu ambavyo huwa zinakuwa, mtu asinione napita barabarani akadhani maisha yangu ni keki kila siku, kuna mateso na maumivu makubwa nyuma yake!

Alichofanya Davina ni kunitafutia tishu za kufutia machozi kisha kuondoka baada ya meneja wetu mkuu, Abdallah Mrisho kuingia na kunikuta katika hali mbaya niliyokuwa nayo, akaketi chini na kuanza kunidadisi ni kwa nini nilikuwa nalia! Kwikwi ilikuwa imenishika sikuweza kuongea, kuna jitu lilikuwa kooni ambalo nahisi ni hasira.

“Braza inaniuma sana, nimejitahidi maishani mwangu kuwa mtu mwema, nikikusanya senti tanotano kwa njia halali mpaka kufika hapa nilipo, mimi ni tofauti sana na wanasiasa ambao wanaweza kutia saini mkataba mmoja tu wa kifisadi wakaingiza bilioni ishirini au watoto wa viongozi wanaoweza kutumia majina ya wazazi wao kujipatia mikataba minono ya kuwatajirisha, kaka unajua mimi nadunduliza kila siku nikijinyima na kuishi maisha ya kawaida ili niwaachie watoto wangu urithi, leo hii nahisi kabisa nataka kunyang’anywa haki yangu niliyoitesekea kwa muda mrefu, inaniuma!

Kwa mwili huu nilikuwa na uwezo wa kushika bunduki na kuingia benki kuchukua fedha au kwenda Brazil kupakia mzigo mkubwa wa heroin au Cocaine na kuleta hapa nyumbani kuja kuharibu watoto wa watu akili, sikutaka kufanya hayo yote kwa sababu sitaki kufanya dhambi au kupata fedha ambazo baadaye nitajilaumu, nimechagua kufanya biashara halali kuanzia gazeti la shilingi mia moja mpaka leo shilingi elfu moja, kwa nini sasa kikundi fulani cha watu kininyime haki yangu? Sitakubali, ni bora nife kuliko kubaki hai wakati haki yangu inataka kuchukuliwa na wanaoona kwamba wana nguvu na hawawezi kufanywa chochote.”

Wakati nayasema maneno hayo yote nilikuwa nikilia kwa uchungu mno, meneja mkuu alijaribu kunituliza lakini alishindwa, roho ilikuwa ikiniuma sana, mimi mtoto wa maskini, niliyetoka chini kimaisha nikapambana mpaka hapa nilipo, unidhulumu kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo? (nitakitaja hivi karibuni). Hapana, ni bora kufa au kupigania haki mpaka tone la mwisho, huko ndiko kunaitwa kuwa mwanaume.

Baadaye nilitulia, tukazungumza na braza Mrisho kwa muda mrefu akinisihi nitulie wala nisichukue hatua yeyote, yeye akiamini haikuwa rahisi kudhulumiwa wakati tulikuwa na mikataba! Jambo moja ambalo hakulifahamu ni kwamba dhamana tulizoweka kwa waliotukopesha fedha zingeweza kuuzwa, hata kama baadaye tungelipwa na CCM ingekuwa haina maana kubwa, wazungu wana msemo usemao “Justice delayed is justice denied” yaani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki ambayo haikutolewa, wakati wa kulipwa na CCM ni sasa ili tuepuke kuuziwa dhamana zetu.

Alipoondoka meneja mkuu ofisini kwangu, aliingia Nyemo Chilongani, mmoja wa vijana wachapakazi ofisini kwangu ambaye husimamia ukurasa wangu wa Facebook, aliongozana na wasichana wawili ambao aliwatambulisha kwangu kama mashabiki wa ukurasa wangu ambao walikuja ofisini kununua vitabu na walitaka niwasainie vitabu vyao na pia tupige picha pamoja.

Wasichana hawa walikuwa ni Zainabu na Dina kutokea Kigamboni, mara moja nilibadilisha muonekano wangu kama vile kilikuwa hakijatokea kitu, tukaanza kuongea mambo mbalimbali kuhusu maisha, nikiwaeleza umuhimu wa kuthamini vipaji maishani, ambavyo kila mmoja wetu anavyo, “Mtu anaweza kufeli darasani kama nilivyokuwa nikifeli mimi, lakini kipaji kikamuinua na kumfanya awe mtu mwenye mafanikio!”

Mwisho wa mazungumzo yetu nilipiga nao picha na kwa kweli walifurahi kukutana nami ambaye ujio wao na mazungumzo tuliyoyafanya ulisaidia sana kubadilisha akili yangu na kunipa uwezo wa kuketi chini na kuandika haya unayoyasoma leo.

Hivyo ndivyo siku yangu ya Novemba 19, 2016, ilivyoanza, nifuatilie wiki ijayo nipate kukueleza kwa undani kilichotokea mpaka nikajikuta katika haya niliyoyaandika leo.

Endelea kuifuatilia wiki ijayo katika Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu
 
Safi sana. Japokuwa ni story ya kusikitisha, kwa upande mwingine imetupa furaha sisi wanyonge tuliosimamia haki kuhakikisha CCM hairudi madarakani kwenye ule uchaguzi wa 2015.

Shigongo na wenzake kupitia vyombo vyao vya habari walikuwa ndio jukwaa la Kutukana, Kudhalilisha na kuzusha kila aina ya uongo dhidi ya UKAWA na Lowassa.

Malipo ni hapa hapa. Na huo ni mwanzo tu.
Magufuli kaza buti, mwendo ni huo huo.
Hapa kazi tu.
CCM oyeeeeeeeee!
 
Angekuwa analipa mikopo kama alivyokubaliana na mabenki, angekuwa huru. Tabu ni walizoea, kweli hadi benki mlizozoea kukopa bila kulipa na kutuonyesha kuwa mna maisha mazuri, leo ndio umekumbuka unaowadai.

Kwani hukuwa na t&c hata tangu uwapatie invoice hikuwa na muda umewawekea wa kikulipa.

Je kama uliweka kwanini hukufata kudai pesa kibiashara? Kuna kitu mlizoea ulikula nao sasa wamebanwa na Mkulu ndio unalia lia.

Lia lia yako kwanini umekuwa haulipi mikopo? Ni uongo kuwa CCM ndio inachangia kukuweka pabaya, bali ni tabia mbaya mlizoea kubebwa kwa kuhonga. Hata kupata hizo tender ulionga wewe, mkome. Awamu hii mtaisoma namba.

Eti zaidi ya mwaka na nusu eeeeh, utuwekee na copy za invoices na statements za unachowadai na kama kuna ppi ndani tuone. Uweke na tarehe za lini uliwatumia invoice hizo etc

Usisahau kuwataja uliowahonga wakupe kazi, ha ha haaaa fichua siri kama unamfupa

Na bado, mtaisoma namba

Kukimbilia gazeti utaonewa huruma na wenzako mliozoea vya dezo na njia za mkato.
 
Kuokoka ni dhana pana mkuu. Ni mtu wa visasi, mwenye kiburi, majivuno na mdhalilishaji. Hata kama ni tajiri wa kutupwa pesa zake zinanuka kama alivyojisemea Marehemu Ben. R. Mtobwa katika mojawapo ya riwaya zake. Naona karma imeanza kufanya kazi yake!
Mkuu Shimba ya Buyenze, leo nitakubaliana na wewe. Pale Kanisa la kilokole la WORD ALIVE Sinza huyu jamaa alikuwa mzee wa kanisa huku akimiliki Dar Live, ambayo kwa imani ya kilokole ni dhambi. Nimesoma ameandika sasa hivi amehama kanisa hilo yuko Victory Christian Centre, hili nalo ni kanisa la Kilokole, tena hili ndio kabisa liko chini ya Tanzania Assemblies of God-ni kanisa ambalo kwa msingi wa TAG linapaswa liwe la kilokole kwelikweli, na kumiliki "kiwanda" cha kuharibu akili za watu na kuwakutanisha na shetani huku ukijitambulisha kuwa ni muumini wa kanisa hilo ni tiketi ya kutengwa na baadaye kutapikwa kabisa kama utashupaza shingo!

Ukisoma katikati ya mistari katika andiko la Erick tunaweza kujiuliza maswali mengi, lakini machache miongoni mwake yanaweza kuwa: 1. Ninavyofahamu mimi, kwa hapa Tanzania mfanyabiashara kutolipwa malipo katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sio issue kubwa kivile (kuna halmashauri moja ya wilaya ninaidai fedha tangu mwaka 2014), ni nini kilichomsukuma Erick kuja hadharani, tena kwenye gazeti analolimiliki, kulia dhidi ya deni lake la mwaka mmoja, tena ambalo mwenyewe anasema amewahi kulipwa kidogo?

2. Erick amekiri kuwa ni kada wa CCM (hata asingekiri inafahamika kuwa amekuwa na mikakati ya kugombea ubunge huko kwao kupitia CCM), ni kwanini anajitia upofu wa kutoona kwamba chama anachokidai, ambacho yeye ni kada wake, kina hali ngumu kifedha? (Rejea madai ya wafanyakazi wa Uhuru). Swali hili halimaanishi kuwa asidai haki yake, lakini linalenga kutilia shaka sababu zake za "kutiririsha machozi" kwa sababu ya kutolipwa kwa wakati deni hilo kama matarajio yake yalivyokuwa.

3. Erick ana ubavu wa kusimama na kuthibitisha kuwa hakuna mtu binafsi au taasisi yoyote inayomdai? Kwamba katika biashara na mihangaiko yake hakuna mtu aliyemtoa machozi kwa "kumtia ndani"? Nauliza swali hili kwa sababu kuna taarifa kuwa kuna watu, wakiwemo waandishi wa magazeti yake ya udaku, wamekuwa wakilalamika kuhusu malipo na mambo mengine kama hayo.

4. Kama ana hofu ya Mungu kwelikweli, Erick anaweza kutuambia alifanya biashara na CCM kwa matarajio tu ya faida ya kifedha au CCM kama chama nacho kimsaidie kwa namna moja au nyingine? Kwamba Erick hakuwa na mipango ya siri ya kukitumia CCM kufikia malengo yake? Na jibu la swali hili pengine linaweza kuwa sababu ya mzee Kinana kuchoshwa na simu na meseji za Erick!

5. Je, Erick amekata tamaa kwamba hakuna tena mwanya wa kufanya biashara na CCM kama alivyozoea huko nyuma, hivyo ameamua kujilipua?
 
Shigongo alipigia kampeni watu ambao wanawaumiza watanzania,leo kaumia yeye,Mungu kamlipa na malipo ni hapa hapa duniani.

Ccm na utapeli ni synonym

Pia yeye hujifanya ni motivation speaker eti anawaelekeza watu kujikomboa kiuchumi,ajikomboe sasa tuone.

Bado clouds,kama shigongo hajalipwa,clouds pia hawajalipwa,wote wapiga dili wakubwa mjini.

Bahati mbaya kwa shigongo analitaka jimbo la Tizeba, akajua ccm watamsaidia kwa kuwa kuna tetesi mtukufu haziivi na tizeba,

lahaula,bahati mbaya kwa shigongo,tizeba akapata uwaziri hivyo kuongeza pumzi kisiasa.

Magazeti yake yanauwawa na facebook,twitta,wasap groups,instagram,zile habari alizotumia kuuza sasa zinapatika mkononi

nadhani na yeye ni mdaiwa wa Twiga bancorp
 
Unakumbuka baada ya kushidwa kwenye kura za maoni na tizeba jimbo la buchosa ulipewa kazi ya ku supply tishert nakofia inchi nzima iliwakupoze maana kipndi hicho kulitokea mvurugano mkubwa sana jimboni hapo ndipo mh kikwete akakuomba umuunge mkono mh tizeba kwenye kampeni za 2010 vingenevyo mh tizeba asinge toboa mwaka huo ndipo ukapewa kazi na kikwete yakusambaza vifaa hivyo sasa ngoja ukome hata uspo taja sisi tunajuwa madai hoya pole sana ila ukome kwanza ndipo upate Akili kwa heri
 
Ha ha. ha haaaaaaaaa... ha haaaaaa

Wee Eric, unajua kutunga weweee.. ha haaaaa..!

Wee umeingia CCM juziiiiii tu, je akina Lowassa waliotoa mabilioni na bado wamepigwa chini, na wanatembea hai, kuna mtu alipigania CCM kama Lowassa.? na bado amekosa hadi Urais.? wee umeingia CCM kichwa kichwa, acha kulia, ndio ujifunze.. na hutalipwa ng'oooooo nikuhakikishie, na utapigiwa mnada vitu vyako, na ukiendelea kukisema vibaya CCM yetu, tunakufilisi, na utakoma kutuchafua.. CCM si mama yako au baba yako, kama imekushinda ondoka hama, acha kutuchafua.. ha haaaaa, umeliwa bahati mbaya poleee poleee usiliee usilieee, ha haaaa poleee ha haaaa Ukiendelea kukichafua chama chetu TUNAKUFILISI KIMOJA.. ha aha haaa

Ukiingia ktk biashara ya siasa ww unajua kupata faida tu..? kuna hasara pia kubwa tu ktk siasa kama biashara nyingine, na nikupe tahadhari, ukiendelea na kulia lia na kutuchafua, tunakufilisi kabisa.. ha haaa, funga mdomo, na futa machozi haraka, keleb wee ha haa, unamdekea nani..? CCM sio mama yako udeke hapa, c.hizi nn, ha ha..

Safiiii, iwe funzo, usirudie, si umesema una mapenzi ya kweli na dhati kwa CCM, sasa unadai nn.? ha haa, keleb hukooo.. safii sanaa

Ndio ukome..!! ha haaaa
 
NIPASHE NEWS PAPER

Kwa kipindi cha Agosti hadi Oktoba mwaka jana, jumla ya nyumba 105 zilipigwa mnada kwa sababu ya mikopo wamiliki walioshindwa kurejesha wakati kipindi kama hicho mwaka 2016, nyumba 405 tayari zimepigwa mnada. Hii inaonyesha kuwa ni ongezeko la nyumba 300.

Baadhi ya majengo maarufu yaliyopigwa mnada ni pamoja na Hoteli ya Tamal iliyopo Mwenye jijini Dar es Salaam. Jengo hilo liliuzwa kwa TZS bilioni 1.1 huku thamani yake halisi ikiwa ni bilioni 2.2. Mmiliki alikuwa akidaiwa bilioni 1.6 na benki.

Kwa upande wa viwanja, kwa kipindi cha miezi hiyo mitatu mwaka 2015 viwanja 15 vilitangazwa kupigwa mnada. Kwa upande wa mwaka 2016 viwanja vilivyotangazwa kupigwa mnada imepanda na kufikia 127.

Wakati huo huo, magari 100 tayari yamepigwa manada mwaka huu katika kipindi cha mwenzi Agosti hadi Oktoba mwaka huu.

Chanzo: Nipashe
 
Mwaka 2005 mtu aitwaye Salva Rweyemamu alimwandikia barua ndefu Kikwete kumkumbusha makubaliano yao ya kupeana vyeo kama angempigia kampeni na kushinda. Salva akajipinda sana na ndiye mwasisi wa kifupi cha JK, mpaka jamaa akaelezea jinsi hizo herufi zilivyo na bahati. Salva alimkumbusha Kikwete makubaliano yao baada ya kuona mwenzake anachelewa kumpa cheo. Hatimaye cheo kilitoka, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu. Kwa hiyo, Shigongo, usingepiga kelele ungemwandikia kumkumbusha juu ya mkataba wenu.
 
Akiongea kwa masikitiko huku akitoa machozi, amesema amesikitishwa sana na Chama cha Mapinduzi kwan kwa muda mrefu amekua akikipigania Chama cha Mapinduzi kwa Hali na Mali Lakini leo kinamtoa machozi.

Akiandika kupitia Gazeti lake la Ijumaa Wikienda lakini Pia kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook amekilalamikia chama cha mapinduzi kuendelea kumzungusha kuhusu malipo yake zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa tangu Afanye Biashara na Chama hicho, aliendelea kulalamika kua Amefanya jitihada za ziada kumpigia Katibu mkuu wa Chama hicho Abdalah Kinana bila mafanikio kwani amekua hapokei simu zake wala kujibu sms.

Anasema Pamoja na kwenda ofisi za Chama hicho Lumumba alikutana na mweka hazina wa Chama hicho Mamma Zhakia Meghji lakini aliambulia kupewa Maji ya Kunywa Bila kupata Pesa zake.

Kinacho muuma Bw Shigongo ni alivyoacha Biashara zake na Kufanya Kampeni karibu Mikoa 10 huku akimpigia Kampeni Rais mstaafu wa wakati huo Dr. Jakaya Kikwete.

Akiongea kwa masikitiko amesema mpaka sasa Mali zake zipo Mbioni kupigwa Mnada wakati wowote kutokana na kwamba ndizo alizoweka Bond ili aweze kupata mkopo ambao alitumia ku supply baadhi ya materials kipindi cha Kampeni za Uchaguzi 2015.

Kwa maelezo zaidi ameahidi kutoa week ijayo katika ukurasa wake na kwenye Gazeti la Wikienda. Na Amesema ataweka wazi ni Kiasi Gani anakidai chama cha Mapinduzi.

Pole sana Brother Eric Shigongo, Endelea kupigania Haki yako ili wakulipe, ni Matumaini yangu Mwenyeketi wa Chama cha apinduzi amesoma Ujumbe wako na atalifanyia kazi ili uweze kulipwa Pesa zako

============================

NOVEMBA 19,2016 JUMAMOSI YA MCHOZI KWANGU

Nawaomba radhi sana wananchi wa Singida, sikuweza kuwepo Namfua baada ya waandaaji kuahirisha tamasha, ipo siku tutakutana.

Nimekwishasema mara nyingi kwamba, hata mimi, kama ilivyo binadamu wengine huwa nina siku mbaya na nzuri katika maisha yangu, kwa sababu kwa watu wengi tafsiri ya maisha bora ni kuwa na gari, nyumba, kazi, fedha nk. Ni rahisi kudhani kwamba ninaishi maisha ya furaha kila siku, si kweli, kuna siku natokwa na machozi kama binadamu mwingine, naomba nikushirikishe sasa siku yangu ya Novemba 19, 2016, siku ya Jumamosi iliyopita, ili upate uhalisia wa maisha.

Usingizi ulikata saa tisa na nusu usiku, nikaanza kuyapitia maisha yangu na changamoto ninazokutana nazo, mambo ninayoyafanya lakini pia kufanyiwa na watu. Mawazo yangu haya yananifikisha kwenye uhusiano wangu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kwa muda mrefu sana nimekuwa kada wake, mara kadhaa nikijitoa mhanga mimi mwenyewe kukitetea na kukipigania nikiamini ndiyo chama pekee kinachoweza kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli.

Naipenda CCM, nakiamini chama hiki hata kama kuna baadhi ya watendaji ndani yake natofautiana na jinsi wanavyofanya mambo kiasi cha kuathiri hatma ya chama hiki kama taasisi, wapenzi, mashabiki na wanachama wake.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara nimewahi kuacha kazi zangu na kuzunguka karibu nusu ya nchi yetu nikipiga kampeni na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, lakini kwa sababu mtu yeyote anayeonesha mapenzi kwa CCM hasa akiwa mfanyabiashara hutafsiriwa anajipendekeza au mwoga, pengine hivyo ndivyo ninavyoitwa, lakini kwangu mimi ambacho hunisukuma kufanya mambo haya ni mapenzi na imani niliyonayo kwa CCM kama taasisi na zilivyo sera zake.

Kama nilivyosema hapo awali, tatizo langu kubwa huwa ni watendaji wa CCM, ambao wakati mwingine hufanya mambo ambayo huathiri mapenzi yangu kwa taasisi yenyewe, hali hii imewavunja moyo watu wengi sana waliokuwa na mapenzi pamoja na imani kubwa kwa CCM.

Yesu ni mwokozi wangu, daima nitazungumza ukweli, hata kama utanigharimu! Nakumbuka huko nyuma nimewahi kuzungumza ukweli kuhusu CCM kwenye ukurasa huu, baadhi ya viongozi wa juu hawakufurahishwa na nilichokiandika, Katibu Mkuu Kinana nikiongea naye ofisi kwake aliniambia “Eric wewe ni kijana wa hapa, siku nyingine ukiwa na suala la kuzungumza tueleze sisi moja kwa moja, usilipeleke barabarani!”

Nilikubaliana naye na sikuwa tayari kabisa kusema maneno yaliyotokana na mawazo yangu ya usiku gazetini tena, kwani nilimuahidi nisingefanya hivyo, lakini nifanye nini, nisemee wapi? Kama katibu mkuu wangu nampigia simu kila siku hapokei? Namuandikia ujumbe kwa njia ya WhatsApp na unaonekana umesomwa lakini hanijibu, tafsiri yangu ni ya haraka ni kwamba ananidharau ingawa mimi namuheshimu kama baba na kiongozi wangu, angalau angekuwa anapokea simu hata kunipa tu matumaini, nisingefikia hatua ya kuzungumza hapa.

Kuanzia usingizi ulipokata saa tisa na nusu usiku, nilifikiria mambo mengi sana juu ya namna ambavyo baadhi ya watendaji wa CCM wamekuwa wakinifanyia pamoja na kujitoa kwangu kote kwa chama hicho, moyo unaniuma mno kwani sistahili hata kidogo kufanyiwa mambo ambayo leo natendewa na chama ambacho mimi binafsi naamini nimejitoa kiasi kikubwa mno kukitumikia kwa akili, muda na mwili wangu.

Inahitaji usiwe mtu mwenye hofu au uliyekata tamaa kufungua mdomo na kuzungumza nitakayoyasema leo, ndugu zangu, Watanzania wenzangu, moyoni mwangu pamejaa uchungu mwingi mno, acha niseme labda nitakuwa mwepesi! Sijui kitakachonipata, Mungu anajua, mimi ni msema kweli, nionavyo mimi ni bora kuzungumza ukweli ukapata matatizo kuliko ubaki hai ukiendeleza unafiki, NASHINDWA.

Mawazo haya juu ya CCM yananitoa machozi mke wangu akiwa usingizini kando yangu, sitaki kumuamsha, sitaki kumshirikisha kinachoendelea, mimi ni mtoto wa kiume mambo mengine natakiwa kukabiliana nayo mwenyewe, kwa muda mrefu naendelea kuwaza nikiwapitia viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia mwenyekiti mstaafu, mwenyekiti aliyeko madarakani, katibu mkuu na mweka hazina.

“Mama!” saa kumi na mbili na dakika kumi namuamsha mke wangu.
“Bee!”
“Tulikubaliana kwenda hospitali Muhimbili kusalimia mgonjwa.”
“Kweli.”
“Mzima lakini?”
“Naendelea vizuri, wewe?”
“Mimi mzima, nina mafua tu kidogo!” nilimjibu hivyo kwa sababu sikutaka agundue kilichokuwa kimetokea.

Kawaida ya wanawake ni kujiandaa taratibu sana, mpaka tunaondoka kwenda Muhimbili tayari ilikuwa ni saa moja asubuhi, tumechelewa muda wa kuona wagonjwa. Mbele ya Jengo la Mwaisela, alipolazwa mgonjwa ambaye ni mkamwana wa mama mmoja aitwaye Mama Swai, ambaye tulikuwa tukiabudu naye Kanisa la Word Alive kabla hatujahamia Victory Christian Center, tunakutana na mlinzi mkali kama pilipili.

“Muda wa kuona wagonjwa umekwisha.”

“Tusaidie kaka” nambembeleza kwa muda, hatimaye akionekana kunionea huruma, anasema “basi aende mmoja tu, tena mwanamke, maana hii wodi ni ya wanawake.”
“Mama nenda basi wewe!”

Mke wangu anaondoka na kuniacha nimesimama peke yangu nje ya wodi, mawazo yananirejesha tena kwa CCM baada ya kubaki peke yangu, najiuliza ni kitu gani nimekikosea chama hicho mpaka kunitendea mambo wanayonitendea! Roho inaniuma, nasikia huzuni kubwa moyoni mwangu, niko chini kabisa kiroho leo, sina furaha hata kidogo, mawazo ya CCM na mambo wanayonitendea, wakati mimi nilishafanya mema mengi kwao yamenivuruga.

Dakika ishirini baadaye mke wangu anatokeza kutoka wodini, alikuwa amepewa muda mfupi sana, pamoja tunaongozana mpaka kwenye gari, namfungulia mlango, anaketi nami nakaa kwenye usukani na kuanza kuendesha kuelekea ofisini, anawahi kazini kwake kwa sababu leo ana sherehe ya watu waliokodisha hoteli.

Njiani nasikia wimbo wa vijana kutoka Kenya waitwao Sauti Sol, uitwao ‘Kuliko Jana’ nilishawahi kuusikia wimbo huo kabla, lakini leo unaonekana kuwa wimbo mpya kabisa kwangu, maneno yake yananigusa sana moyo, namshikirisha Vene kwenye wimbo huo, anaonekana kama hanielewi au ninachokiongea hakimgusi, bila shaka anawaza sherehe inayofanyika hotelini kwake.

“Hawa vijana wanaimba sana, natamani siku moja niwaalike hapa Dar es Salaam, nifanye tamasha kubwa la vijana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu, bure! Nifundishe vijana wa taifa hili uzalendo na kupenda nchi yao.”

Natamka maneno hayo ingawa moyoni mwangu kuna uchungu mwingi;

Bwana ni mwokozi wangu,
Tena ni kiongozi wangu,
Ananipenda leo kuliko jana!
Baraka zake hazikwishi si kama binadamu habadiliki,
Ananipenda leo kuliko jana,
Kuliko jana, kuliko jana,
Yesu nipende leo kuliko jana,
Kuliko jana, kuliko jana,
Yesu nipende leo kuliko jana,
Nakuomba Mungu uwasamehe
Wangalijua jinsi unavyonipenda
Mimi wasingenisema
Na maadui wangu nawaombea
Maisha marefu wazidi kuniona ukinibariki
Ujue binadamu ni watu wa ajabu sana
Walimkana Yesu mara tatu kabla jogoo kuwika…

Safari inaendelea, wimbo uliokuwa ukipigwa redioni umefika mwisho, kwa kutumia simu yangu nilitafuta ‘You tube’ kisha kuuchagua wimbo huo ambao unaendelea kupiga mpaka namfikisha mke wangu ofisini kwake, kila unapokwisha naurudia tena, unanizidishia uchungu moyoni, namshusha mke wangu na kuendesha tena kuelekea ofisini kwangu.

Mawazo ni mengi, kichwa kimevurugika, Mariam, msaidizi wangu anaingia na kunitayarishia chai, nakunywa lakini haipandi. Baadaye anaondoa vyombo na kuniacha peke yangu, muda mfupi baadaye aliingia mzee Mbizo, sijui kama alinielewa kwa hali aliyonikuta nayo, nilikuwa kwenye siku yangu mbaya, niko chini sakafuni nawaza, baada ya salamu tu tofauti na siku nyingine zote ambazo mimi na yeye huongea mambo machache, anaaga na kuondoka.

Nabaki peke yangu nikiendelea kufikiria, naikumbuka siku ya mwisho nilipofika ofisi ndogo ya CCM pale Lumumba, ambako nilikwenda nikitarajia kulipwa fedha zangu ninazodai kwa kazi niliyoifanya (kwa leo sitataja ni kiasi gani) kama nilivyokuwa nimeahidiwa baada ya kuwa nimesubiri mwaka mmoja na miezi sita, hapo katikati nikiwa nimelipwa fedha kidogokidogo sana.

Tofauti na matarajio kwamba siku hiyo ningelipwa fedha zote, nikalipwa kiduchu tena! Nikiwa ndani ya ofisi ya mweka hazina wa chama, mama Zakia Meghji, yeye ni shahidi, kama nasema uongo au ukweli anajua, machozi yalinitoka! Hali yangu kibiashara ni mbaya, fedha nyingi ziko mikononi mwa CCM na nina madeni makubwa ninayodaiwa, baadhi ya wadai wanataka kupiga mnada mali zangu! Chama Cha Mapinduzi kimeniingiza kwenye matatizo makubwa.

Nakumbuka alichokifanya mama huyu ni kunipa chupa ndogo ya maji ya Kilimanjaro na kuniambia “Kunywa maji mwanangu, upunguze uchungu!” nikayapokea na kuyanywa, niliondoka ofisini hapo nikiahidiwa kwamba ningelipwa muda si mrefu, lakini haikuwa hivyo, siku zinazidi kusonga na hali inazidi kuwa mbaya na hakuna anayeonekana kujali.

Kwenye saa 5: 00 asubuhi hivi, naamua kuachana na mawazo hayo kwani maisha bado yanaendelea na kuamua kwenda kuungana na wenzangu kwenye kikao cha asubuhi kujadili maendeleo ya Gazeti la Ijumaa Wikienda ili nifute kilichokuwa kikiendelea kichwani, nafanikiwa kufanya kikao hicho bila mtu yeyote kugundua kilichokuwa kikiendelea akilini mwangu na baadaye narejea ofisini ambako naendelea kuusikiliza Wimbo wa Sauti Sol huku nikizidi kuhuzunika.

Muda mfupi baadaye anaingia Davina Lema, msimamizi wa kampuni yetu ya Blue Mark Real Estate ambayo inajishughulisha na upangishaji wa nyumba, tunaongea naye kuhusu biashara na namna ya kufanya biashara katika kipindi hiki kigumu, nampenda Davina, alianza kazi hii akiwa hajui chochote lakini sasa amemudu kazi, baada ya mazungumzo hayo ndiyo naanza kumweleza kidogo kuhusu maisha na namna ambavyo mtu unaweza ukatenda wema lakini ukalipwa ubaya.

Sikuweza kuzungumza hadi mwisho, machozi yananitoka mbele ya mfanyakazi wangu, si jambo jema lakini sikuwa na jinsi, siandiki haya ili nionewe huruma la hasha! Nawaeleza muone baadhi ya siku zangu ambavyo huwa zinakuwa, mtu asinione napita barabarani akadhani maisha yangu ni keki kila siku, kuna mateso na maumivu makubwa nyuma yake!

Alichofanya Davina ni kunitafutia tishu za kufutia machozi kisha kuondoka baada ya meneja wetu mkuu, Abdallah Mrisho kuingia na kunikuta katika hali mbaya niliyokuwa nayo, akaketi chini na kuanza kunidadisi ni kwa nini nilikuwa nalia! Kwikwi ilikuwa imenishika sikuweza kuongea, kuna jitu lilikuwa kooni ambalo nahisi ni hasira.

“Braza inaniuma sana, nimejitahidi maishani mwangu kuwa mtu mwema, nikikusanya senti tanotano kwa njia halali mpaka kufika hapa nilipo, mimi ni tofauti sana na wanasiasa ambao wanaweza kutia saini mkataba mmoja tu wa kifisadi wakaingiza bilioni ishirini au watoto wa viongozi wanaoweza kutumia majina ya wazazi wao kujipatia mikataba minono ya kuwatajirisha, kaka unajua mimi nadunduliza kila siku nikijinyima na kuishi maisha ya kawaida ili niwaachie watoto wangu urithi, leo hii nahisi kabisa nataka kunyang’anywa haki yangu niliyoitesekea kwa muda mrefu, inaniuma!

Kwa mwili huu nilikuwa na uwezo wa kushika bunduki na kuingia benki kuchukua fedha au kwenda Brazil kupakia mzigo mkubwa wa heroin au Cocaine na kuleta hapa nyumbani kuja kuharibu watoto wa watu akili, sikutaka kufanya hayo yote kwa sababu sitaki kufanya dhambi au kupata fedha ambazo baadaye nitajilaumu, nimechagua kufanya biashara halali kuanzia gazeti la shilingi mia moja mpaka leo shilingi elfu moja, kwa nini sasa kikundi fulani cha watu kininyime haki yangu? Sitakubali, ni bora nife kuliko kubaki hai wakati haki yangu inataka kuchukuliwa na wanaoona kwamba wana nguvu na hawawezi kufanywa chochote.”

Wakati nayasema maneno hayo yote nilikuwa nikilia kwa uchungu mno, meneja mkuu alijaribu kunituliza lakini alishindwa, roho ilikuwa ikiniuma sana, mimi mtoto wa maskini, niliyetoka chini kimaisha nikapambana mpaka hapa nilipo, unidhulumu kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo? (nitakitaja hivi karibuni). Hapana, ni bora kufa au kupigania haki mpaka tone la mwisho, huko ndiko kunaitwa kuwa mwanaume.

Baadaye nilitulia, tukazungumza na braza Mrisho kwa muda mrefu akinisihi nitulie wala nisichukue hatua yeyote, yeye akiamini haikuwa rahisi kudhulumiwa wakati tulikuwa na mikataba! Jambo moja ambalo hakulifahamu ni kwamba dhamana tulizoweka kwa waliotukopesha fedha zingeweza kuuzwa, hata kama baadaye tungelipwa na CCM ingekuwa haina maana kubwa, wazungu wana msemo usemao “Justice delayed is justice denied” yaani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki ambayo haikutolewa, wakati wa kulipwa na CCM ni sasa ili tuepuke kuuziwa dhamana zetu.

Alipoondoka meneja mkuu ofisini kwangu, aliingia Nyemo Chilongani, mmoja wa vijana wachapakazi ofisini kwangu ambaye husimamia ukurasa wangu wa Facebook, aliongozana na wasichana wawili ambao aliwatambulisha kwangu kama mashabiki wa ukurasa wangu ambao walikuja ofisini kununua vitabu na walitaka niwasainie vitabu vyao na pia tupige picha pamoja.

Wasichana hawa walikuwa ni Zainabu na Dina kutokea Kigamboni, mara moja nilibadilisha muonekano wangu kama vile kilikuwa hakijatokea kitu, tukaanza kuongea mambo mbalimbali kuhusu maisha, nikiwaeleza umuhimu wa kuthamini vipaji maishani, ambavyo kila mmoja wetu anavyo, “Mtu anaweza kufeli darasani kama nilivyokuwa nikifeli mimi, lakini kipaji kikamuinua na kumfanya awe mtu mwenye mafanikio!”

Mwisho wa mazungumzo yetu nilipiga nao picha na kwa kweli walifurahi kukutana nami ambaye ujio wao na mazungumzo tuliyoyafanya ulisaidia sana kubadilisha akili yangu na kunipa uwezo wa kuketi chini na kuandika haya unayoyasoma leo.

Hivyo ndivyo siku yangu ya Novemba 19, 2016, ilivyoanza, nifuatilie wiki ijayo nipate kukueleza kwa undani kilichotokea mpaka nikajikuta katika haya niliyoyaandika leo.

Endelea kuifuatilia wiki ijayo katika Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu

Hili ni igizo. Na anaamini ni silaha yake ya mwisho kuweza kulipwa pesa zake.

Jamaa huyu ni mjanja sana, anakuwa kama hajasoma anaonekana kama humwe.

Maskini hakuijua vizuri siasa za Tanzania. NAOMBA NIMSHAURI YAFUATAYO AMBAYO HAKUYAJUA:-

1. Pesa za uchaguzi huwa zinaisha zote pale mshindi anapotangazwa ni kama pesa za mbio za mwenge brother umesahau?

2. Hali ni ngumu kaka si wewe tu. humu humu serikalini tunatafutana hakuna kitu kabisa na matumizi ya ovyo ovyo eti nili supply vipeperushi or nilitoa page kwa kampeni za chama. (hakuna Muda wake ulisha kwisha).

3. Brother pole sana. Chama cha mapinduzi kilikuwa na mtandao wake wa kukiendesha, Kaka! ule mtandao umekatwakatwa kabisa si unajua bandarini palivyo kwa hiyo wote tuliokuwa tunafanya biashara kirahisi (kupiga dili hakuna tena kaka hali ni mbaya!!)

4. Na si unajua uchumi wa nchi ulivyo sasa si mzuri ni mbaya. Jipe moyo.
5. Lakini kaka si unamikataba halali nenda mahakamani dai chako. kakini pole kama ulitoa kama kusaidia chama.

Kwa ujumla ndugu geuza gea angani. Usitegemee sana madeni hayo. Mungu jalia kwa sababu umewachana hazarani tena wazi wazi watakulipa. Lakini gharama zake ni kubwa baadaye. Panga mipango yako upya songambele.

Siku nyingine usiwaseme watu wakubwa na chama kikubwa tawala kama ulivyo fanya unakosa adabu kwa maana wewe chama kilikuwa kinatutegemea.

Ninajua wengi watakuwa wamesikia hasa wazee wa chama na watamwomba Mwenyekiti arekebishe.

Hata hivyo chama si ndiyo serikali? na serikali si ndiyo chama? usiwe na wasiwasi tutaku skip kwenye kupiga mnada mali zako.
 
Si ulikuwa ukijipendekeza kwao kwa muda mrefu tu!! Sasa wao wamemwaga Ugali na wewe mwaga Mboga!!! ahahaaaa! Uhuhuuuu! Aliselema Halija!!! Hiki ni kichekesho cha kufunga mwaka 2016. Pole sana, karibu upinzani upate fursa ya kuwasuta na kuhubiri case study yako kwenye mikutano ya ndani ya vyama vya upinzani. Tumeipenda sana story yako itasaidia sana kuiangusha CCM kwenye sanduku la kura au kwa mabao ya mikono ifikapo Octoba 2020. Tena una kipaji kizuri sana cha kuhubiri na kushawishi, tafadhali vitumie vipaji vyako ili jina lako likumbukwe hata miaka milioni moja ijayo, toka huko CCM, Mwenyezi Mungu amekuonyesha ishara kwa kuwa wewe ni mtumishi wake mwaminifu. Sasa fanya mikakati mingine ya kulipa deni ili mali zako zisije zikapigwa mnada na wewe ukapata kiharusi kwa jinsi unavyofikiria mambo kwa undani sana! Take it Easy Shigongo!
 
Back
Top Bottom