Chain Of Command: Dkt. Mpango hajui mipaka yake

"Atamsaidia Rais kufuatilia Utekelezaji wa Siku hata Siku na hata Mambo ya Muungano "

Vyema kabisa, unapomsaidia Mkuu wako wa Kazi, unatakiwa umpe ripoti. Yeye ndio ataiwasilisha kwa Waliomuajiri, ambapo kwa Rais, Waajiri wake ni sisi wananchi.

Hivyo VP akitumwa kazi na Rais, anatakiwa ampe breafing Rais, na Rais atatuhutubia Sisi. Hiyo ndio Chain Of Command ambayo Dr Mpango hajaijua.

Mwalimu Nyerere aliwahi kufafanua vizuri tofauti ya ujinga na upumbavu kama ifuatavyo:


Naye Professor Kabudi akaja kutoa ufafanuzi unaoshahibiana na ule alioutoa Mwalimu Nyerere (huku akiuongezea nyama huo ufafanuzi) kama ifuatavyo:
 
Tangu ateuliwe Kama Makamu wa Rais Dr. Mpango amekuwa akitoa kauli za Kiutendaji bila kujali Mipaka ya Majukumu yake.

Mara ya Kwanza alisikika akimuagiza Waziri wa Fedha akusanye Tilioni 2. Bila kujua kwamba Mamlaka hayo ni ya Rais kwenda kwa Waziri wa Fedha kisha Kamishna Mkuu TRA.

Pili, Tena kasikika akiwaagiza Wakuu wa Mikoa Masuala ya Kinidhamu bila kujua kwamba, Mamlaka ya uteuzi na maagizo ya Kinidhamu yako Ofisi ya Rais - Tamisemi.

Huyu Dr anasahau kuwa yeye ni reserve wa Rais endapo litatokea (Mungu aepushe mbali). Na kwamba Mamlaka yake ya Maagizo ya Kiutendaji yako kwenye Mazingira na Muungano.

Afundwe huyu.
Mpango hana mvuto wa kiuongozi yupo yupo tu kama bundi mchana wa jua kali.
 
Labda kaona Mama anapwaya na hatoi hayo maelekezo ipasavyo. Mwacheni Mpango afanye yake na atadeal na boss wake when need be.
 
Huyu yupo kwenye kundi la mwenda zake, Samia alikosea Sana kumpendekeza huyu...
Huenda mama Samia aliconsult mahali na wakampa hili jina hata kama hakuwa amelipenda kwa 100%. Kuna wakati flaniflani inabidi ku-compromise ili na wewe mambo yako yaende bila bughudha.

Waratin huwa wanasema "quid pro quo" - meaning a favour or advantage granted in return for something
 
Watu wa Kigoma ni shida,siku si nyingi Mama atajuta.
Nyie walimbwende, warembo, Wala vyepe daily, midebwedo wa pwani na Kaskazini kwa Mboowe mtakoma na wivu wenu kwa watu wa Kigoma. Kigoma ni kazi tu. Mkipenda hata wake zenu wape Waha wawafanyie kazi yenye weledi wa hali ya juu na iliyotukuka.

Upo hapo mrembo.
Hapa kazi tu.
Mwanaume kazi tu.
Kigoma kazi tu.
 
Dr Mpango ni Professor wa nadharia zaidi. Tukitaraji matendo kwake tutamuonea.

Mungu atuepushe asije ukwaa Urais wa JMT. Tutaumia!
Na ndio wasiwasi wenu kwamba huenda akawa Rais baadae ndio maana muda wote mnahangaika kumchafua. Tulieni.
 
Na ndio wasiwasi wenu kwamba huenda akawa Rais baadae ndio maana muda wote mnahangaika kumchafua. Tulieni.
Mkuu

Unamchafuaje Prof aliyeshiba nadharia vitendo nehi?

Tuombe uzima. Itajulikana nani anamchafua Nani.
 
Hofu yangu isije ikawa "mfumo dume" umegandamana naye... ni suala la muda tu...
kabisa. Kuna Changamoto nyingi sana za Mazingira na Muungano. Ajikite kuhakikisha tunapata Mazingira Safi na Salama ya kuishi. Takataka ziondolewe, Muungano uimalike tuishi kidugu zaidi.
 
Apewe mikasi akafungue makongamano na kufunga semina.
Afuatilie suala la Mazingira .
Aendeshe mijala ya Muungano wetu katika mambo yote yenye utata kwa pande zetu mbili.
Haya niyo majukumu yake kama makamo wa Raisi wakati raisi akiwa yupo ofisini.
Ama raisi akiwa nje ya ofisi mfano nje ya nchi au Likizo au Mgonjwa ,Makamo anaweza kuwa na Excutive order kwa niaba ya Raisi.
 
Apewe mikasi akafungue makongamano na kufunga semina.
Afuatilie suala la Mazingira .
Aendeshe mijala ya Muungano wetu katika mambo yote yenye utata kwa pande zetu mbili.
Haya niyo majukumu yake kama makamo wa Raisi wakati raisi akiwa yupo ofisini.
Ama raisi akiwa nje ya ofisi mfano nje ya nchi au Likizo au Mgonjwa ,Makamo anaweza kuwa na Excutive order kwa niaba ya Raisi.
Umenena.
 
Back
Top Bottom