Jamani salama nataka kujoin kwenye hii kitu nipeni procedure
wanandugu nawashukuru wote walioweza kufika kwenye mkutano.. kwa kweli ulikuwa mkutano mzuri. naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kuleta muhtasari ila naahidi kuuwakilishi si muda mrefu ujao.
Pamoja na hayo nawashukuru wote ambao walinipigia simu, PM au emai kuniambia kuwa hawatahudhuria. lakini nasikitika sana kuwa kuna watu wali-confirm kuja lakini hawakutoa taarifa kuwa hawaji.. sasa ndugu zangu naomba tujifunze kutoa taarifa tunapohairisha maanake isingekuwa uelewa wa wenye hoteli wangetu-charge hata wale ambao hawakufika (tulikuwa tumeweka order za watu 35 ila tukawa 23). Watu wa hotel walituelewa na wakawa flexible (baada ya kuwaomba) hivyo hawakutu-charge.
Ndg. Kanyagio au Malila,
Tafadhari tujulishe mara usomapo hapa lini tutakuwa na Chai Day ya kufungua mwaka 2012?
JF Marker anathibitisha kuhudhuria.
Mimi nitakuwepo
malila, hongereni sana kwa hilo na ninampongeza aliyetoa chachu ya wazo hilo. Napenda kutoa taarifa kuwa na mimi nihitaji kujiunga. Nitatuma mchango wangu kushiriki.Karibu tujumuike pamoja, naamini utafurahia kukutana na wajasiriamali chipukizi.
malila, hongereni sana kwa hilo na ninampongeza aliyetoa chachu ya wazo hilo. Napenda kutoa taarifa kuwa na mimi nihitaji kujiunga. Nitatuma mchango wangu kushiriki.
Malila na ndugu wengine, inabidi kutoa mfumo bora wa watu kufanya confirmation ili kuzuia watu wanao-confirm mtandaoni then wanapotea kabisa hawaonekani na hawatoi udhuru.
So cha kufanya ni kufanya makisio ya gharama na kujua kila mtu atoe ngapi. na ukumbi utafutwe kulingana na idadi ya watu watakaokuja ili kuondoa hasara au waandaji kukabwa mashati na wenye hoteli.
so mtu akonfrm kwa kutoa participation fee.
nawasilisha!!